Ehhh,
Watanzania sisi ni watu wa ajabu sana. Mbona mnashabikia namna hii Mwakyembe kunyanyaswa? Kwani Mwakyembe hana makosa? Kwani wabunge wa CCM hawana makosa? Kwanza TAKURURU ianze na hii habari kuwa kila mbunge wa CCM wakati wa uchaguzi alimegewa 5M kutoka kwa mshika kapu la fweza, homeboy Rostam Azziz. Na homeboy alivyo na akili, akawasainisha wote ili wasimruke, hahahaaaaaaa........ Wote waliopokea 5M wahojiwe nao. Homeboy Hosea wembe ule ule.
Hosea (TAKURURU), weee fanya kazi yako bila kitisho kwa mtu yeyote. Hata nduguyo Sitta na yeye mlime tu madudu yake. Kama wao wanataka kukuDO basi na wewe ni kama wimbo wa P-Square yaani "If you do me, i do you". Maadamu walikuwa na muda wa kukudeal na wakawa wanazembea hiyo si tatizo lako sasa. Uchaguzi unakuja na wabunge wengi wa CCM wanataka pa kutokea na wa kumtoa MHANGA utakuwa wewe. Usikubali kabisa. AU mnakufa wote au WANYAMAZE MIELE na watafute kingine cha kutokea. Na kwa sababu hawana na Richmonduli inauzika kirahisi kwa wananchi na hasa kwa Mwakyembe, basi lazima atalia nayo ili Watanzania wamuoneehuruma.
Na nyie wabunge vipi? Mnakubali kuendeshwa na Hosea? Mlililea JINI mnaona sasa? Jini limeshakuwa kubwa sana na haliwezi kuingia kwenye chupa tena. Sasa lenyewe ndiyo litaanza kuwsulubu. Mlitakiwa kuwa mmeshamuondoa Hosea zamani sana ila tatizo huyu Ngosha ni NGOSHA kweli. Hamumuwezi kwa sababu amewakamata PABAYA na kumkolimba inakuwa ngumu maana huko yeye ndiyo maeneo yake ya kujidai. Sasa mmebaki kulialia kwa wananchi. Lenyewe liko kimya tu LINAFANYA VITU VYAKE, hahaaaaaa Safi sana.
Kama huna akili utakuwa hukunielewa. Ila kama una akili na unaipenda nchi yako ya TANZANIA, basi amini kuwa hii ni HABARI nzuri sana nchini. Ili nchi iende, inabidi Static Energy ibadilishwe na iwe kinetic energy. Na hii bahati mbaya kila siku inaleta FRICTIONS. Kukiwa na friction (msuguano) kunatokea JOTO ambalo sasa tunaliona akina Mwakyembe na Sitta wanatokwa. Ila bila friction, basi hakuna joto na hakuna movement. Ombi kwenu wahusika.
1. Wabunge, msipomuwahi Hosea, atawawahi nyie na kuwamaliza kisiasa na hata mkaenda Jela.
2. HOSEA (TAKURURU), usipowawahi wabunge na kuwanyamazisha, mwisho wako utakuwa mbaya. WANASIASA HAO!!