Dr. Mwakyembe Vs. TAKUKURU

Dr. Mwakyembe Vs. TAKUKURU

Hivi kwa nini Dkt Mwakyembe amesikia maumivu zaidi (hata kutetemeka wakati anaongea na waandishi wa habari) kuliko Wabunge wenzake waliohojiwa? Au yeye (Dkt Mwakyembe) alikwapua nyingi zaidi ukichanganya na zile fedha za matibabu hewa alizotia ndani?
 
Buchanan,

hivi umeshawahi kufanya kazi Serikalini? Mbona mambo ya kupokea mgao mara mbili kwa kazi moja wakati wa warsha, semina, kongamano, mikutano, mafunzo kazini, ziara n.k ni mambo ya kawaida sana.

kama kuna tatizo katika hili basi takukuru ilipaswa kuchukua hatua kuanzia zamani zile, vinginevyo kuna kila dalili ya kutaka kukomoana katika hili.

Ndo mambo yaleyale, ukininyima jua, mimi nakunyima mvua.

Wewe nawewe nimbunge au? nawewe unapokeaga bahasha (posho) marambili kwa kazi moja? Hapa nikuwapongeza hao TAKUKURU kwakutake initiative za kutokomeza hayo 'mazoea' ya wabunge kufanya mambo kinyume na sheria, Pili nadhani huo nimwanzo mzuri wa TAKUKURU kutekeleza majukumu yake ya kusafisha hali ya rushwa ambayo nimbaya sana Tanzania, wabunge hawalioni hili kwasababu linawagusa wao moja kwa moja
 
Hao TAKUKURU....do they really mean business? Or something is to happen at the background?
 
Hao TAKUKURU....do they really mean business? Or something is to happen at the background?

Nafikiri angalia uhalali wa hizo posho zaidi! Otherwise, jiulize pia kama "wapambanaji" nao wako serious kwa kupokea malipo zaidi ya mara moja kwa kazi moja! Ni sawa na kulipwa mishahara miwili kwa kazi ile ile! Kanchi ketu kazuri jamani, wakati kuna watu wanapokea malipo mara mbili kuna wengine hawana uhakika na mlo mmoja kwa siku! Ukitaka kuwajua wabunge wetu gusa maslahi yao! Tunakumbuka juu ya hoja ya Dkt Slaa juu ya kupunguziwa posho zao! Hapa hakukuwa na Kilango, Seleli, Mwakyembe au nani! They were totally against the idea! Kaazi kweli kweli!
 
Unamkumbuka Dr. Masumbuko Lamwai- unakumbuka alivyokuwa anatesa na Sheria zake za Kidokta yuko wapi.

.
Huo sasa ni uonevu kwa kuwataka watu wasiseme hata kama ni sheria. sasa tutaendekeza hali ya kuogopa mpka lini?
 
Hawa MPs bado hawajakoma kuimba wimbo wa takrima? Wameuhamisha toka kwenye uchaguzi wameuingiza kwenye vikao ili kupata posho mara mbili kwa kazi moja? Ndio maana vikao vinaendeshwa kila siku: too much talking for Tanzanians! Kaazi kweli kweli!
 
Kwenye gazeti la Mtanzania leo kuna habari kwamba Mbunge wa Kyela atakamatwa na TAKUKURU ambayo imesema kwamba mbunge huyo hayuko juu ya Sheria! Kwa kuwa habari niliyo nayo ni ya kusikia toka kwenye Redio (RFA) naomba mwenye nakala ya gazeti hilo amwage data zaidi!
 
Ndugu zangu,

Muhimu zaidi ni kuwa PCCB sio Hosea. Hosea anaweza kuwa mtuhumiwa lakini kuna vijana wazuri tu pale wazalendo ambao wanafanya kazi vizuri sana. Vyombo hivi vinafanya kazi kwa maandishi, hivyo ni dhahiri kuwa ni vigumu kupindisha ukweli mahakamani.

..........

Du! kazi kwelikweli, PCCB wameanza kuonekana wanajua kazi kwa kuanzia bungeni!! mangapi yamelala pale............. majibu hakuna.
 
Kwa maoni yangu, Mwakiembe hakamatiki kwa ajili ya matamshi yake ya Dodoma, unless PCCB walimtaarifu spika kwa maandishi kuwa wanamuhitaji Mwakiembe kwa mahojiano, huku Mwakiembe mwenyewe amepelekewa samansi ya PCCB kuitwa kwa mahojiano,akakaidi, ni kweli anakamatika.
 
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA IMEFIKIA UAMUZI WA KUMKAMATA MH Dr H. MWAKYEMBE KWA KUKAIDI WITO WA KWENDA KUOJIWA KWA KUPOKEA POSHO MARA MBILI KWA KAZI MOJA.... DUH KAMA NI KWELI BASI MWAKYEMBE HATA JIMBO UTAKOSA SASA
 
Nani kakwambia ni random? Tunahojiwa Wabunge wote. Uchunguzi umeanza toka mwezi Mei kwa kuita wabunge. Isipokuwa ulianza toka mwezi Februari kwa kuhoji makatibu wakuu wa wizara na wakurugenzi wa mashirika.
This is not random. Who told you this? Are you just assuming it is random? Suala la timing sio la kweli na sijui ni nani kasema eti wameanza uchunguzi wakati huu.
Kwa nini tusiache uchunguzi umalizike na kama kuna hatua za kimahakama zifuatwe. Sielewi kabisa mjadala huu maana yake nini. Kwamba tusichunguzwe? Sielewi kabisa standards zetu mie. Kwani kuchunguzwa ndio kwamba umetenda dhambi?

Can you revisit my posting?
Nilisema nilitegemea zoezi liwe random. Majibu yako yanonekana kama umeelewa kinyume cha mambo.

Uchunguzi ulianza February, OK! Kwa nini? Utasema PCCB wanaruhusiwa kisheria, Fine! But what a coincidence in its happening?

You are possibly right, hebu niambie tangu waanze wamekwisha muhoji waziri yupi?

Lakini pia bila kujali kisingizio cha uchunguzi unaoendelea, unaweza kutueleza ni kwa nini kulipwa posho hizi imekuwa ni notorious habit among the so called waheshimiwa?
Tusitetee uzembe wowote hata kama tumeshaukubali. iwe ni kupokea posho za ziada au hata kutojua na kujukuta ukihojiwa kwa kudhalilishwa.

Ni tabia mbaya na hasa ukizingatia kwamba mashirika na ofisi zinazotoa posho hizo, zinawategemea hao hao wabunge kuweza kupata utetezi bungeni.

Hata hivyo tatizo langu hukulieleza. Kwa nini sasa? Kwa nini kwa wabunge baada ya kuwa na mijadala ya RICHMOND? Baada ya kuitaka mara nyingi serikali ichukuwe hatua juu ya tabia ya PCCB over Richmond. Whatever sense you may make out of the exercise, it can’t defeat a normal human common sense.
 
Nami nimeona katika star tv magazeti. Pccb katika hili la kumkamata wamechemsha. Kwanza wabunge tuna kinga katika tunayosema si tu ndani ya ukumbi bali pia katika viunga vya bunge. Takukuru hawana mamlaka ya kumkamata mbunge kwa matamshi aliyoyatoa kwenye press conf iliyofanyika kwenye viunga vya Bunge. Wanajimwambafy tu, hawana uwezo huo. Jambo la msingi ni wao kuhakikisha wito wao unaitikiwa na wabunge na kupata maelezo yao. Ni muhimu wabunge kuonyesha jamii kuwa hatuna mawaa katika mienendo yetu. Kuhojiwa na kutoa ushirikiano ni hatua mojawapo ya kuithibitishia jamii kuwa tu wasafi.
 
RA yeye huwa hasaini "viposho" hivi. Alishajizolea zake nyingi mapema. Zitto msiwaache MAWAZIRI wetu. Wao wanachota nyingi zaidi. Ni kufuru!
 
Nami nimeona katika star tv magazeti. Pccb katika hili la kumkamata wamechemsha. Kwanza wabunge tuna kinga katika tunayosema si tu ndani ya ukumbi bali pia katika viunga vya bunge. Takukuru hawana mamlaka ya kumkamata mbunge kwa matamshi aliyoyatoa kwenye press conf iliyofanyika kwenye viunga vya Bunge. Wanajimwambafy tu, hawana uwezo huo. Jambo la msingi ni wao kuhakikisha wito wao unaitikiwa na wabunge na kupata maelezo yao. Ni muhimu wabunge kuonyesha jamii kuwa hatuna mawaa katika mienendo yetu. Kuhojiwa na kutoa ushirikiano ni hatua mojawapo ya kuithibitishia jamii kuwa tu wasafi.


Mkuu Zitto nimekupata hapa, lakini pia hili linawezekana tu pale PCCB watapofuata utaratibu unaokubalika sio kukurupuka tu kwamba leo tunamtaka fulani basi wanapiga simu kumuita.

Nina amini msimamo wa Mwakyembe kukataa kuhojiwa ni sahihi na kwamba utafungua njia mpya ya hawa watu kuacha kutaka kunyamazisha watu fulani eti kuwa tu wana mamlaka ya kuwanyamazisha
 
Mawaziri wanaongoza kuchukua posho mara mbili. Kama mnabisha nendeni halmashauri mkaulize.
 
Naombeni kuuliza vipi kuhusu ile tume/kamati aliyounda Mh Mwakyembe ya sakata la rushwa la Richmond???iliishia wapi?nadhani siko off point sana wadau mnisamehe kama niko off point.
 
muda si mrefu wataanzisha kyelastan hawa ... teh teh teh teh
mzee kyela haiwezi fika uko, we subiri hio 2010 utaprove kuwa Mwakyembe ni simba wa kyela.
Hivi tangu lini mtu mwizi, huyo aliyeshindwa kuchunguza richmond leo aje awachunguze wale waliomgundua kuwa yeye ni mwizi na mbabaishaji. Hapa ndio utangundua jinsi viongozi wetu walivyowasanii, unaona kuwa mambo ya richmond kimya sasa yameanza ya akinamwakyembe. nafikiri tumalize kwanza richmond halafu mengine yaje yafuate. halafu hata mawaziri pia wahojiwe maana nao ni wabunge. hapa waanzie kwa pinda mwenyewe.
 
Mawaziri wanaongoza kuchukua posho mara mbili. Kama mnabisha nendeni halmashauri mkaulize.
Nakumbuka hili lilitokea Karatu (ambako Halmashauri inaongozwa na Chadema) madiwani walikataa kulipia malazi ya ujumbe wa Makamu wa Rais kwa vile tayari walisha lipwa posho na ofisi zao walikotoka.
 
Ehhh,
Watanzania sisi ni watu wa ajabu sana. Mbona mnashabikia namna hii Mwakyembe kunyanyaswa? Kwani Mwakyembe hana makosa? Kwani wabunge wa CCM hawana makosa? Kwanza TAKURURU ianze na hii habari kuwa kila mbunge wa CCM wakati wa uchaguzi alimegewa 5M kutoka kwa mshika kapu la fweza, homeboy Rostam Azziz. Na homeboy alivyo na akili, akawasainisha wote ili wasimruke, hahahaaaaaaa........ Wote waliopokea 5M wahojiwe nao. Homeboy Hosea wembe ule ule.

Hosea (TAKURURU), weee fanya kazi yako bila kitisho kwa mtu yeyote. Hata nduguyo Sitta na yeye mlime tu madudu yake. Kama wao wanataka kukuDO basi na wewe ni kama wimbo wa P-Square yaani "If you do me, i do you". Maadamu walikuwa na muda wa kukudeal na wakawa wanazembea hiyo si tatizo lako sasa. Uchaguzi unakuja na wabunge wengi wa CCM wanataka pa kutokea na wa kumtoa MHANGA utakuwa wewe. Usikubali kabisa. AU mnakufa wote au WANYAMAZE MIELE na watafute kingine cha kutokea. Na kwa sababu hawana na Richmonduli inauzika kirahisi kwa wananchi na hasa kwa Mwakyembe, basi lazima atalia nayo ili Watanzania wamuoneehuruma.

Na nyie wabunge vipi? Mnakubali kuendeshwa na Hosea? Mlililea JINI mnaona sasa? Jini limeshakuwa kubwa sana na haliwezi kuingia kwenye chupa tena. Sasa lenyewe ndiyo litaanza kuwsulubu. Mlitakiwa kuwa mmeshamuondoa Hosea zamani sana ila tatizo huyu Ngosha ni NGOSHA kweli. Hamumuwezi kwa sababu amewakamata PABAYA na kumkolimba inakuwa ngumu maana huko yeye ndiyo maeneo yake ya kujidai. Sasa mmebaki kulialia kwa wananchi. Lenyewe liko kimya tu LINAFANYA VITU VYAKE, hahaaaaaa Safi sana.

Kama huna akili utakuwa hukunielewa. Ila kama una akili na unaipenda nchi yako ya TANZANIA, basi amini kuwa hii ni HABARI nzuri sana nchini. Ili nchi iende, inabidi Static Energy ibadilishwe na iwe kinetic energy. Na hii bahati mbaya kila siku inaleta FRICTIONS. Kukiwa na friction (msuguano) kunatokea JOTO ambalo sasa tunaliona akina Mwakyembe na Sitta wanatokwa. Ila bila friction, basi hakuna joto na hakuna movement. Ombi kwenu wahusika.

1. Wabunge, msipomuwahi Hosea, atawawahi nyie na kuwamaliza kisiasa na hata mkaenda Jela.
2. HOSEA (TAKURURU), usipowawahi wabunge na kuwanyamazisha, mwisho wako utakuwa mbaya. WANASIASA HAO!!
nilijua kuwa lazima roho itakuuma kuona mwakyembe anasimama yeye kama yeye na kuonyesha njia, huo ndio uongozi na sio kufuata mkumbo tu. Tungekuwa na rais kama mwakyembe tungekuwa mbali.
 
Back
Top Bottom