Buchanan,
hivi umeshawahi kufanya kazi Serikalini? Mbona mambo ya kupokea mgao mara mbili kwa kazi moja wakati wa warsha, semina, kongamano, mikutano, mafunzo kazini, ziara n.k ni mambo ya kawaida sana.
kama kuna tatizo katika hili basi takukuru ilipaswa kuchukua hatua kuanzia zamani zile, vinginevyo kuna kila dalili ya kutaka kukomoana katika hili.
Ndo mambo yaleyale, ukininyima jua, mimi nakunyima mvua.
Hao TAKUKURU....do they really mean business? Or something is to happen at the background?
Huo sasa ni uonevu kwa kuwataka watu wasiseme hata kama ni sheria. sasa tutaendekeza hali ya kuogopa mpka lini?Unamkumbuka Dr. Masumbuko Lamwai- unakumbuka alivyokuwa anatesa na Sheria zake za Kidokta yuko wapi.
.
Ndugu zangu,
Muhimu zaidi ni kuwa PCCB sio Hosea. Hosea anaweza kuwa mtuhumiwa lakini kuna vijana wazuri tu pale wazalendo ambao wanafanya kazi vizuri sana. Vyombo hivi vinafanya kazi kwa maandishi, hivyo ni dhahiri kuwa ni vigumu kupindisha ukweli mahakamani.
..........
Nani kakwambia ni random? Tunahojiwa Wabunge wote. Uchunguzi umeanza toka mwezi Mei kwa kuita wabunge. Isipokuwa ulianza toka mwezi Februari kwa kuhoji makatibu wakuu wa wizara na wakurugenzi wa mashirika.
This is not random. Who told you this? Are you just assuming it is random? Suala la timing sio la kweli na sijui ni nani kasema eti wameanza uchunguzi wakati huu.
Kwa nini tusiache uchunguzi umalizike na kama kuna hatua za kimahakama zifuatwe. Sielewi kabisa mjadala huu maana yake nini. Kwamba tusichunguzwe? Sielewi kabisa standards zetu mie. Kwani kuchunguzwa ndio kwamba umetenda dhambi?
Nami nimeona katika star tv magazeti. Pccb katika hili la kumkamata wamechemsha. Kwanza wabunge tuna kinga katika tunayosema si tu ndani ya ukumbi bali pia katika viunga vya bunge. Takukuru hawana mamlaka ya kumkamata mbunge kwa matamshi aliyoyatoa kwenye press conf iliyofanyika kwenye viunga vya Bunge. Wanajimwambafy tu, hawana uwezo huo. Jambo la msingi ni wao kuhakikisha wito wao unaitikiwa na wabunge na kupata maelezo yao. Ni muhimu wabunge kuonyesha jamii kuwa hatuna mawaa katika mienendo yetu. Kuhojiwa na kutoa ushirikiano ni hatua mojawapo ya kuithibitishia jamii kuwa tu wasafi.
mzee kyela haiwezi fika uko, we subiri hio 2010 utaprove kuwa Mwakyembe ni simba wa kyela.muda si mrefu wataanzisha kyelastan hawa ... teh teh teh teh
Nakumbuka hili lilitokea Karatu (ambako Halmashauri inaongozwa na Chadema) madiwani walikataa kulipia malazi ya ujumbe wa Makamu wa Rais kwa vile tayari walisha lipwa posho na ofisi zao walikotoka.Mawaziri wanaongoza kuchukua posho mara mbili. Kama mnabisha nendeni halmashauri mkaulize.
nilijua kuwa lazima roho itakuuma kuona mwakyembe anasimama yeye kama yeye na kuonyesha njia, huo ndio uongozi na sio kufuata mkumbo tu. Tungekuwa na rais kama mwakyembe tungekuwa mbali.Ehhh,
Watanzania sisi ni watu wa ajabu sana. Mbona mnashabikia namna hii Mwakyembe kunyanyaswa? Kwani Mwakyembe hana makosa? Kwani wabunge wa CCM hawana makosa? Kwanza TAKURURU ianze na hii habari kuwa kila mbunge wa CCM wakati wa uchaguzi alimegewa 5M kutoka kwa mshika kapu la fweza, homeboy Rostam Azziz. Na homeboy alivyo na akili, akawasainisha wote ili wasimruke, hahahaaaaaaa........ Wote waliopokea 5M wahojiwe nao. Homeboy Hosea wembe ule ule.
Hosea (TAKURURU), weee fanya kazi yako bila kitisho kwa mtu yeyote. Hata nduguyo Sitta na yeye mlime tu madudu yake. Kama wao wanataka kukuDO basi na wewe ni kama wimbo wa P-Square yaani "If you do me, i do you". Maadamu walikuwa na muda wa kukudeal na wakawa wanazembea hiyo si tatizo lako sasa. Uchaguzi unakuja na wabunge wengi wa CCM wanataka pa kutokea na wa kumtoa MHANGA utakuwa wewe. Usikubali kabisa. AU mnakufa wote au WANYAMAZE MIELE na watafute kingine cha kutokea. Na kwa sababu hawana na Richmonduli inauzika kirahisi kwa wananchi na hasa kwa Mwakyembe, basi lazima atalia nayo ili Watanzania wamuoneehuruma.
Na nyie wabunge vipi? Mnakubali kuendeshwa na Hosea? Mlililea JINI mnaona sasa? Jini limeshakuwa kubwa sana na haliwezi kuingia kwenye chupa tena. Sasa lenyewe ndiyo litaanza kuwsulubu. Mlitakiwa kuwa mmeshamuondoa Hosea zamani sana ila tatizo huyu Ngosha ni NGOSHA kweli. Hamumuwezi kwa sababu amewakamata PABAYA na kumkolimba inakuwa ngumu maana huko yeye ndiyo maeneo yake ya kujidai. Sasa mmebaki kulialia kwa wananchi. Lenyewe liko kimya tu LINAFANYA VITU VYAKE, hahaaaaaa Safi sana.
Kama huna akili utakuwa hukunielewa. Ila kama una akili na unaipenda nchi yako ya TANZANIA, basi amini kuwa hii ni HABARI nzuri sana nchini. Ili nchi iende, inabidi Static Energy ibadilishwe na iwe kinetic energy. Na hii bahati mbaya kila siku inaleta FRICTIONS. Kukiwa na friction (msuguano) kunatokea JOTO ambalo sasa tunaliona akina Mwakyembe na Sitta wanatokwa. Ila bila friction, basi hakuna joto na hakuna movement. Ombi kwenu wahusika.
1. Wabunge, msipomuwahi Hosea, atawawahi nyie na kuwamaliza kisiasa na hata mkaenda Jela.
2. HOSEA (TAKURURU), usipowawahi wabunge na kuwanyamazisha, mwisho wako utakuwa mbaya. WANASIASA HAO!!