Dr. Mwakyembe Vs. TAKUKURU

Dr. Mwakyembe Vs. TAKUKURU

Homework nimekwisha fanya. Ni kosa la jinai kukataa wito wa chombo cha dola kama Polisi, Mahakama na PCCB. Sababu alizozitoa hazina mashiko kisheria na ndio maana wenzake wote wakaenda.

Huyu jamaa yako, kama mtunga sheria na mwana sheria, anaonyesha mfano mbaya mbele ya jamii kwa kuvidharau vyombo vya dola. You get me now sir?

Jamaa anatakiwa kutii amri ya dola, PCCB ni chombo cha dola kama polisi na mahakama, huwezi kukataa wito wao, kufika kwako pale ni kuisaidia dola.

Jamaa kama mwanasheria anachemsha sasa, Richmond imempa kiburi.
 
Subiri Mahakama itaamua, sasa wewe unakurupuka na kuja na uamuzi wako inakuwa ngumu kukuamini...naona unahisia za kisiasa zaidi kuliko kwenye haki Mkuu tk (teddy kalonga)
 
Ni kutojua haki zako, siwezi kushangaa unakamatwa na traffic police unaambiwa nipe leseni unampa, nipe kadi ya gari unampa kisa na kuwekwa ndani eti ni polisi.....tujifunze haki na sheria ndogo ndogo.
 
Hivi wabunge wangine wote waliojiwa au kuna ambao walikataa kuojiwa kamwa mwakyembe?

Wengi wamehojiwa.
ni huyu fisadi mwakyembe ndiye aliyekataa,akitegemea msaada wa fisadi nyangumi-mengi na nipashe.

Sasa analia na magazeti ambayo ndiyo yamempa hizi sifa ambazo anazililia.tutaona mwisho wake
 
Zitto,
Tunafahamu mengi sana kuhusu tabia hii ya wabunge kupenda extras. Kamati za bunge ni nuisense.

Kama ni malalamiko juu ya tabia hiyo kwa kweli ofisi za serikali zinajieleza kwa mengi saana. Wabunge mulishakuwa sugu.

Kinachonishangaza juu ya hili ni PCCB kulitekeleza kama kulipa kisasi kwa kuwaita wabunge selectively na kuwaacha wale ambao ni mawaziri. Kuanzia 2006 naweza kusema ni Wabunge woote wamesha ramba double payments, Pinda inclusive. Hapo kwa binadamu kama mimi topic hugeuka na kuwa witch-hunting.

Hata kama sheria imefuatwa, kwa idadi ya wabunge lazima iwe random exercise na siyo selective implementation. Mbaya zaidi ni PCCB ya Hosea ambayo ina sifa za kutosema ukweli wa wazi. Mbaya zaidi PCCB pia ilichunguzwa na tume ya Bunge. Pia ni mbaya kwamba ni hatua inayochukuliwa wakati Bunge linaelekea kuanza vikao, ndani yake kukiwa na mambo ya Richmond ambayo PCCB ilikuwa accused kwa kuyaficha.

Do I need to be intelligent to express my doubts on the move?

Nani kakwambia ni random? Tunahojiwa Wabunge wote. Uchunguzi umeanza toka mwezi Mei kwa kuita wabunge. Isipokuwa ulianza toka mwezi Februari kwa kuhoji makatibu wakuu wa wizara na wakurugenzi wa mashirika.
This is not random. Who told you this? Are you just assuming it is random? Suala la timing sio la kweli na sijui ni nani kasema eti wameanza uchunguzi wakati huu.
Kwa nini tusiache uchunguzi umalizike na kama kuna hatua za kimahakama zifuatwe. Sielewi kabisa mjadala huu maana yake nini. Kwamba tusichunguzwe? Sielewi kabisa standards zetu mie. Kwani kuchunguzwa ndio kwamba umetenda dhambi?
 
Subiri Mahakama itaamua, sasa wewe unakurupuka na kuja na uamuzi wako inakuwa ngumu kukuamini...naona unahisia za kisiasa zaidi kuliko kwenye haki Mkuu tk (teddy kalonga)

Sikuizi mtu akisemwa tu,anakupiga dongo hata kama la ukweli au huongo na kwa kuwa wa-tz tunaogopa vivuri vyetu full kukimbilia magazetini.Kama mwakyembe kala pesa peleka mahakamani,TAKUKURU wanadhani Mwak kawadharau,waende mahakamani,Mwaki anadhani kadhalilishwa nenda mahakamani. Tatizo vivuri,kila mtu ana madudu.Takukuru wanakula rushwa,waogopa vivuri,Mwaki kala cha juu anaogopa mahakamani.Kazi hipo.Waoga watakwambia Hiundwe tume ya maridhiano.Kwenda zako,maridhiano na wezi!!!!!!!!!!! Sijui sasa tumuhamini nani!
 
Kwa mtazamo wangu naona huu mjadala umeletwa ili kuwadivert watu kutoka kwenye masuala ambayo Bunge lilipaswa kupokea taarifa yake sasa. List za waliopewa posho bungeni na kwenye vikao sehemu nyingine inajulikana, wanawahoji ili nini, kama sheria inasema wazi posho ni moja tu? Nadhani tuanze kuwawajibisha kwanza wale waliolipa hizo posho huku wakijua hao wabunge wamelipwa walikotoka. Watasema wabunge wanashinikiza, hakuna sheria inayowalinda kuhusu hilo, tatizo mashirika mengi ya umma wanatumia hizo nafasi kuwanyamazisha wabunge kwa kuwalipa hizo posho ili wasiwabane, na pia ni loophole ya kufanikisha wizi wao. Huo uchunguzi kwa nini usifanyike kwenye nyaraka walizonazo? au hawana kumbukumbu kama kawaida yao?
Ikulu gani imeamuru uchunguzi ufanyike wakati Kagoda imeshikwa na kigugumizi kuichunguza? I doubt!

Unawawajibishaje hao watoa posho kama wao wanasema wabunge tuliwaomba? Si lazima wabunge tuhojiwe kama ni kweli tuliomba. Pili, mashirika yanasema tumelipa wabunge. CAG haoni ushahidi wa kulipa wabunge, anapeleka taarifa mbele na huko nako wanapeleka takukuru. Si ni lazima takukuru wawahoji wabunge kama kweli walichukua pesa?

Unajua hapa ni ulinzi wa fedha za umma. Inawezekana kabisa mashirika yakawa yanasema yanawapa pesa wabunge wakati hayawapi na wanazila wao. Sasa unathibitishaje? Ni lazima wabunge tuhojiwe ama kama mashahidi au kama watuhumiwa.

Mbona jambo hili dogo?
 
Hapa kazi ipo, "fisadi" anapomwita mwenzake "fisadi!" God bless Tanzania na watu wake wote!
 
Mimi nafikiri nimeelewa kwamba Dr Mwakyembe amekataa kuhojiwa na TAKUKURU kwa kuwa yeye si mhalifu.

Suala ni kwamba kachukua posho mara mbili na posho zenyewe zimewekwa na mfumo uliopo ambao unaruhusu hali hio.

TAKUKURU ipo kwa jili ya kudhibiti na kuzuia rushwa na sio kudhibiti na kuzuia posho.

Serikali inatakiwa kurekebisha hali hio ya posho kuzagaa kila kwenye taasisi yake na kusema hakuna posho zaidi ya mara mbili.

Ingekuwa DR Mwakyembe amechukua posho zaidi ya mara moja kutoka kwenye ofisi ya bunge basi kungeundwa kamati na hata kama angekuwa amechukua kwenye taasisi ingine pia taasisi hiyo ingefanya uchunguzi wake.

Na hata kama DR Mwakyembe angegushi hizo posho basi polisi ndio wangehusiswa na sio TAKUKURU.

TAKUKURU ilipaswa tokea ianzishwe iwakamate na kuwahoji macho kwa macho wale wote ambao wanahusika na matukio yote ya rushwa Tanzania kwa kuanzia na Andrew Chenge.
 
Wengi wamehojiwa.
ni huyu fisadi mwakyembe ndiye aliyekataa,akitegemea msaada wa fisadi nyangumi-mengi na nipashe.

Sasa analia na magazeti ambayo ndiyo yamempa hizi sifa ambazo anazililia.tutaona mwisho wake

Pumba!
 
Hapa kazi ipo, "fisadi" anapomwita mwenzake "fisadi!" God bless Tanzania na watu wake wote!

Nadhani Tuvunje kila kitu tuanze upya kabisa Tanzania na raisi Dictator, Hakuna Takukuru, Bunge wala Mahakama kila kitu kinaenda kwa kudra za mwenyezi Mungu!
 
Takururu: Kamata Mwakyembe na vibaka wenzake waliomlea Hosea na Chenge.

Wabunge: Kamata Hosea na Chenge kwa UFISADI wao.

Sasa hapa inakuwa kama kupigana. Mwenye speed KALI ndiyo atashinda.

NB: Ila narudia tena. Chenge na Hosea hawa Ngosha wameshika nchi na they are UNTOUCHABLE. Who say NO?????
 
Viongozi wa Kitanzania na wananchi wake wote bure kabisa!......ni bendera kufuata upepo!......
 
Ni kutojua haki zako, siwezi kushangaa unakamatwa na traffic police unaambiwa nipe leseni unampa, nipe kadi ya gari unampa kisa na kuwekwa ndani eti ni polisi.....tujifunze haki na sheria ndogo ndogo.

Watu kama hawa ndio wale ambao wanakamatwa kwa kutolipa kodi ya maendeleo na kisha wanapelekwa mahakamani kwa kesi za wizi - wakati ndugu zao wakichangisha pesa za kuwawekea dhamana (na kumhonga jaji, mwendesha mashtaka, askari magereza, nyapala mkuu nk nk nk).
 
Si ndio maana Takukuru wanataka wawahoji wahusika ili wapate majibu ya maswali yote hayo? Watajuaje kama hawakuwahoji wabunge waliopokea ili wajue waliomba hizo fedha kwa madhumuni gani?

Wakitosheka kuwa ilikuwa si rushwa bali "kuwalainisha tu wasiingi ndani zadi katika uchunguzi wao" basi wataachiwa.
lakini unatakiwa uangalie kinacho chochea takukuru kuchukua hatua hizi sasa ni nini, nia nzuri ya kuondoa tatizo hilo au kwa kuwa wabunge wanataka kumshugulikia Hosea (Takukuru)
kuna neno moja lina tumika katika sheria inaitwa kuchukua hatua kwa minajili ya ku-defeat kkutenda haki.
Move ya takukuru ni ya kutaka ku-defeat utoaji wa haki au kuficha matatizo yao.
Kisheria hili halikubaliki.
eg wewe unapo mzuia polisi kufanya kazi yake wakati anapotaka kumtia nguvuni mtuhumiwa au unapoharibu ushaihidi, sasa hata timing ya takukuru kwa hili ni ili kuwazuia wabunge wanaokazania issue ya richmond wasifanye kazi yao. Wangekuwa fair basi wangeacha hili kwa sasa wamalize hilo la richmond, na kama wana moto kama huo leo hii nafikiri wangeisha kuwa wameulizia TRL, TICTS, vitambulisho vya taifa, ununuzi wa magari ya sirikali na kwa ujumla manunuzi mengi tu tanzania yetu ni ya rushwa rushwa.
kwa hivyo takukuru wafuatilie vitu vya msingi ndipo wafuate haya hapo baadae au wwqanzie kwa hao walio toa .
 
Unawawajibishaje hao watoa posho kama wao wanasema wabunge tuliwaomba? Si lazima wabunge tuhojiwe kama ni kweli tuliomba. Pili, mashirika yanasema tumelipa wabunge. CAG haoni ushahidi wa kulipa wabunge, anapeleka taarifa mbele na huko nako wanapeleka takukuru. Si ni lazima takukuru wawahoji wabunge kama kweli walichukua pesa?

Unajua hapa ni ulinzi wa fedha za umma. Inawezekana kabisa mashirika yakawa yanasema yanawapa pesa wabunge wakati hayawapi na wanazila wao. Sasa unathibitishaje? Ni lazima wabunge tuhojiwe ama kama mashahidi au kama watuhumiwa.

Mbona jambo hili dogo?

Kwa nini watu wanaogopa Kuhojiwa, kwa nini watu wanatumia Vita dhidi ya Ufisadi kama Mwamvuli dhidi ya Taratibu za kisheria juu ya Matendo yao? Acha wahojiwe kama wamechukua posho mara mbili sheria iangaliwe inasemaje katika hilo kama ni haki yao ama la! Hiki ni kipimo kizuri sana cha nani mnafiki na nani ana uchungu kweli na Akina mama wanaokufa kwa kukosa gloves za kujifungulia, wanafunzi wanaosoma chini ya miti, Akina mama wanaotembea kilomita kumi kuchota maji kwa Ndoo za Kichwani halafu wao wanaramba posho tatu tatu. Acha Uchunguzi huru ufanyike as far as haumhusu Mwakyembe peke, Achunguzwe Zitto, achunguzwe Slaa, Achunguzwe Pinda na Ripoti iwekwe Hadharani. Ebo
 
Back
Top Bottom