Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,192
- 1,972
Nami nimeona katika star tv magazeti. Pccb katika hili la kumkamata wamechemsha. Kwanza wabunge tuna kinga katika tunayosema si tu ndani ya ukumbi bali pia katika viunga vya bunge. Takukuru hawana mamlaka ya kumkamata mbunge kwa matamshi aliyoyatoa kwenye press conf iliyofanyika kwenye viunga vya Bunge. Wanajimwambafy tu, hawana uwezo huo. Jambo la msingi ni wao kuhakikisha wito wao unaitikiwa na wabunge na kupata maelezo yao. Ni muhimu wabunge kuonyesha jamii kuwa hatuna mawaa katika mienendo yetu. Kuhojiwa na kutoa ushirikiano ni hatua mojawapo ya kuithibitishia jamii kuwa tu wasafi.
Mheshimiwa Zitto tunaomba vifungu (kanuni za bunge, katiba au sheria nyingine yoyote) vinavyotoa hiyo kinga maana hapa kidogo mnatuchanganya, hasa mnapozungumzia kinga sasa hivi, huku hamkusema chochote kuhusu kinga ya mbunge hasa pale Mheshimiwa Basil Pesambili Mramba (kesi ya misamaha ya kodi) na Mheshimiwa Andrew Chenge (kesi ya kusababisha ajali) walipohojiwa na kesi zao kwa sasa ziko mahakamani!