Wakuu zangu,
Mimi nilikaa pembeni kusikiliza wachangiaji lakini kuna maswali ambayo nashindwa kuyajibu ikiwa kweli tutatafsiri hizi sheria kwa jinsi tunavyojisikia..
Ningependa kujua ni wakati gani TAKUKURU wanaruhusiwa kuwahoji Wabunge?..Mathlna Takukuru wamewahi kufanya uchunguzi wa Richmond kabla ya kamati ya Mwayembe (kama Mnakumbuka) Je, ni Mawaziri ganmi waliohojiwa na TAKUKURU kama sio hao hao Wabunge!..
Pili tusichanganye makosa ya mbunge ktk utendaji akiwa nje ya Bunge, mathlan Mbunge ambaye ni waziri akifanya wizi wizarani sidhani kama sheria inakataza asihojiwe kwa wizi huo kwa sababu ni Mbunge hilo moja, ila sheria inakataza Mbunge asihojiwe maswala yoyote yanayohusiana na BUNGE..(kama sikosei).
Mfano ni kuhojiwa kwa Mramba, huyu kweli aliikuwa Mbunge lakini kesi yake ilihusioana na utendaji kazi wake akiwa waziri wa wizara na sii Mbunge.. hivyo inakubalika kisheria..Tukipinga hili ni lazima tujiuliza je ni wakati gani wabunge wanaweza kuhojiwa.. mathlan kina Rostam, who's to question them..maanake hata Rostam ni mbunge!
Swala la Mwakyembe kuhojiwa lipo wazi kabisa kuwa ni makosa...kwa sababu lipo ktk kifungu cha pili..Kazi zote za kamati za Bunge zilipewa baraka za Bunge pamoja na rais mwenyewe..sote tunakumbuka hili, hivyo kama kulikuwepo na malipo ya posho mbili -mara zote sheria za uhasibu mkosa ni yule aliyelipa posho hizo kinyume cha sheria..iwe ni muidhinishaji wa malipo ya posho za Bunge, shirika, wizara au taasisi husika kwa sababu kabla hujalipa poshi au fedha zozote ni lazima kuwepo na suppoting document ambayo huidhinishwa kulingana na tumizi tarajiwa..Ni kazi ya Auditors kufanya uchunguzi huo na kuwakilisha mahesabu yao, kulipwa posho mara mbili sii kosa la kukihusisha chombo kikubwa kama TAKUKURU kama vile wamekosa kazi..
Hao waliolipa waliweka mahesabu ya posho hizo ktk kifungu gani na iliidhinishwa na nani?..Na ikiwa sehemu zote za kikazi ziliidhinisha posho hizo kimakosa hili sii kosa linalotakiwa kufikishwa mahakamani isipokuwa ni chombo husika (i.e Bunge) kukata (as a refund) fedha zote walizolipa kwa mbunge huyo kama ziada ya malipo.. Unless Bunge lenyewe ndilo lipeleke malalamiko haya TAKUKURU na kuomba uchunguzi ufanyike.