Dr. Nchimbi amejiuzulu mwenyewe kuokoa mafao yake.

Tumia barua yake kujua sababu zake za kujiuzulu, hizo nyingine ni speculations
Soma Katiba ili uzijue kazi za makamu wa Rais na majukumu yake. Wewe makamu huwezi kutoka hadharani na kusema anaekwamisha katiba ni boss wangu. Katiba hii inampa boss wangu nguvu nyingi zisizo na maana, mdaini katiba kwa nguvu. Huo ni nusu uhaini, kama Rais angekuwa ni Magufuli sasa hivi Nchimbi angekuwa yuko kolokoloni kwa matamshi yale. Wanadhani Rais samia ni mwepesi sana kwasababu ya jinsia yake, mavazi, sauti na lip stick zake tu na kusahau kuwa yeye ndiye Rais, Mkuu wa nchi, Amirijeshi Mkuu na mwenyekiti wa CCM kwa wakati mmoja. Wanasahau Katiba yetu inasema nini kuhusu Rais wa nchi.

Katiba hii ni halali kabisa, imetumiwa na marais wote, hata yeye anaweza kuamua kuitumia hiihii kama vile Magufuli alivyosema ataitumiaa katiba hiihii kuinyoosha nchi. Bila Katiba hii huenda tusingekuwa na SGR, bwawa la umeme, ndege wala kuhamia Dodoma. Kwakutumia Katiba hii Samia amefuta na kubadilisha seria nyingi sana ambazo zilikuwa zinatukwamisha tz. Nchi sasa ina kipato kikubwa. Mimi ninakwambia Tz kuna watu na taasisi ambazo hazitaki kabisa kuona serikali inakuwa na fedha nyingi za kuboresha huduma za umma kama afya, elimu na viwanda ili wao waendelee kuvuna fedha kwakutumia uduni na uhaba wa huduma za umma.
 
Unaamini kwamba kuna watu ambao walipanga Samia asiapishwe kuwa Rais baada ya Rais JPM kufariki? Unajua ni akina nani? unajua kwanini hawakutaka aapishwe yeye kuwa rais? Unajua ni nani aliuzuia mpango huo?

..kwa utendaji wa huyu Mama, huenda waliojaribu kuzuia asiapishwe walijua uwezo wake ni mdogo, na walikuwa na nia nzuri na taifa, lakini njia zao zilikuwa kinyume na katiba.

..Mama angekuwa kiongozi mzuri angesimamia 4R mpaka zikamilike. Lakini kwasababu hana uwezo ndio maana akaiga mambo ya Jpm ya kuteka, kutesa, na kuuwa.
 

..anayekwamisha 4R ni nani?

..anayekwamisha Katiba ni nani?

..aliyesababisha mauaji ni nani?

..nani aliwachochea Polisi wawe na chuki kiasi cha kuuwa wengi kiasi kile?
 
Sidhani...nijuavyo mimi miafrika ukijiudhuru ni sawa na kuhasi...mh. Humphrey polepole...alipojihudhuru...hakupewa stahiki zozote...yeye mwenyewe alikiri​
 
unateseka sana endelea kupulizia kinyesi manukato
 
Sidhani...nijuavyo mimi miafrika ukijiudhuru ni sawa na kuhasi...mh. Humphrey polepole...alipojihudhuru...hakupewa stahiki zozote...yeye mwenyewe alikiri​
Hakuwa na haja nazo kwakuwa alikuwa na uhakika wa 100% kuwa wanakwenda kumuondoa Samia na kujilipa wenyewe. Kaka ule ulikuwa ni mpango mkubwa sana kuliko tunavyodhani na kusimulia. Humphrey alikuwa na uhakika wa 300% kuwa serikali hii ingeanguka kama Samia akisupaza shingo ya kuacha kugombea Urais. Aliusahau ukubwa wa CCM katika kupambana na mizengwe kama ile ya akina Horace Kolimba, Kingunge, msindai, Membe, Lowassa, G55, Lyatonga, Oscar Kambona, mzee Jumbe, Kanali Bakari, Wareno, Makaburu, Salmin Amour, nk
 
unateseka sana endelea kupulizia kinyesi manukato
Dr. Nchimbi ni mkongwe ndani ya chama, anajua ni makosa gani ukiyatenda utafukuzwa.

Dr. Nchimbi alikuwa anajua siku nyingi kuwa lazima atafukuzwa kwa alichokifanya, na alijua kuwa akifukuzwa atakwenda kuunga juhudi vyama vya upinzani. Hata hotuba yake ile yenye ukakasi ililenga hilo na aliitoa kama sehemu ya kujua kuwa atafukuzwa. Ndiyo maana aliwaambia wananchi wadai katiba mpya ili itumike kwenye chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2030. Kauli ambayo inataka katiba mpya itumike kwenye chaguzi zijazo haina tofauti na kauli za wapinzani; maana yake CCM ianguke ikibidi kwa kutumia Tume Huru ya Uchaguzi kwenye chaguzi zijazo.

Amekikosea chama kwelikweli kwa kumbembeleza mwana wao kwa wimbo mbaya wa "OOOh, oyo oyo oyo CCM shindwa, CCM shindwa CCM shindwa kwakutumia katiba mpya chaguzi zijazo kwa Tume Huru na Katiba mpya". Maana na yeye kama Polepole anajua CCM inashindaje kwa kutumia katiba hii na anazifahamu nguvu alizokuwanazo Rais kwa katiba hii ya 1977.
 
Walikua wanaenda kulifanikishaje hili la kumuondoa?
 
Kwani si mmesema Katiba iko kwenye ilani ya chama cha Mapinduzi ugumu uko wapi kutekeleza kile mlichoahidi?
 
Kauli ambayo inataka katiba mpya itumike kwenye chaguzi zijazo haina tofauti na kauli za wapinzani; maana yake CCM ianguke ikibidi kwa kutumia Tume Huru ya Uchaguzi kwenye chaguzi zijazo.
Kwa hiyo kumbe mnajua katiba mpya ikipatikana CCM inaanguka?
 
Kwa hiyo kumbe mnajua katiba mpya ikipatikana CCM inaanguka?
Uhuru wa Tume ya uchaguzi ni x-factor kwenye kushinda uchaguzi. Hata Marekani kuna wakati wana mashaka na tume yao ya uchaguzi kuwa haiko huru. Kuna wakati walishawahi hata kuituhumu Russia, kuna wakati wanatuhumu zile kura za posta kuwa zina namna zinainufaisha Democrats kupitia tume.

Mh. Nchimbi alikuwa na kila sifa na sababu ya kufukuzwa uanachama, alikuwa na "nia ovu kwa CCM" na "nia njema kwa wapinzani" kuwatanulia njia yao ya kwenda Ikulu hata kama hawana sera za maana na tofauti na CCM. Maana ni mtu mpumbavu tu ambae ataamini kuwa Katiba mpya itasambaza maji kila nyumba nchini.
 
Kwa hiyo kumbe mnajua katiba mpya ikipatikana CCM inaanguka?
Watu wetu hawana elimu kubwa, hawajui nani anasema kweli na nani anawadanganya wakati wa kampeni za uchaguzi. Hii ni hatari sana kwakuwa nchi inaweza kurudishwa kwa mkoloni tena kupitia njia ya tume huru sana na demokrasia. Mwl. Nyerere alilidahamu hilo ndio maana baada ya kuona Lyatonga Mrema anawadanganya wananchi wakati wa kapeni na wananchi kuonekana kama vile kumuamini ndipo Mwl akaamua kusimama na kumpigia kampeni Benjamin Mkapa. Na watu walipomuuliza kwanini wewe ni baba wa taifa lakini unapigia kampeni CCM tu akawajibu kwa kiingereza kuwa "I can't let my country go to the dogs" huku mimi nikiwabnimejifungia chumbani na kusema mm ni baba wa Taifa.

Mwl alijua wananchi bado hawezi kumjua anaewadanganya.
 
Una akili timamu we kolo kolo?
 

Uongo mtupuuu.
 

Haswaaaa, hata huyu Ndejembi akika vibaya atafurushwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…