kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
- Thread starter
- #21
Soma Katiba ili uzijue kazi za makamu wa Rais na majukumu yake. Wewe makamu huwezi kutoka hadharani na kusema anaekwamisha katiba ni boss wangu. Katiba hii inampa boss wangu nguvu nyingi zisizo na maana, mdaini katiba kwa nguvu. Huo ni nusu uhaini, kama Rais angekuwa ni Magufuli sasa hivi Nchimbi angekuwa yuko kolokoloni kwa matamshi yale. Wanadhani Rais samia ni mwepesi sana kwasababu ya jinsia yake, mavazi, sauti na lip stick zake tu na kusahau kuwa yeye ndiye Rais, Mkuu wa nchi, Amirijeshi Mkuu na mwenyekiti wa CCM kwa wakati mmoja. Wanasahau Katiba yetu inasema nini kuhusu Rais wa nchi.Tumia barua yake kujua sababu zake za kujiuzulu, hizo nyingine ni speculations
Katiba hii ni halali kabisa, imetumiwa na marais wote, hata yeye anaweza kuamua kuitumia hiihii kama vile Magufuli alivyosema ataitumiaa katiba hiihii kuinyoosha nchi. Bila Katiba hii huenda tusingekuwa na SGR, bwawa la umeme, ndege wala kuhamia Dodoma. Kwakutumia Katiba hii Samia amefuta na kubadilisha seria nyingi sana ambazo zilikuwa zinatukwamisha tz. Nchi sasa ina kipato kikubwa. Mimi ninakwambia Tz kuna watu na taasisi ambazo hazitaki kabisa kuona serikali inakuwa na fedha nyingi za kuboresha huduma za umma kama afya, elimu na viwanda ili wao waendelee kuvuna fedha kwakutumia uduni na uhaba wa huduma za umma.