Dr Nchimbi apongeza Kasi ya Uokoaji Kariakoo na kusema iongezwe zaidi, asema CCM iko tayari kutoa Msaada wowote utakaohitajika!

Dr Nchimbi apongeza Kasi ya Uokoaji Kariakoo na kusema iongezwe zaidi, asema CCM iko tayari kutoa Msaada wowote utakaohitajika!

Salaam za Katibu Mkuu wa CCM Dr Nchimbi:

1. Shukrani Kwa Wananchi kwani Wao ndio walikuwa wa kwanza kufika na kuanza Uokoaji

2. Shukrani Kwa Vyombo vyote vya uokozi vinavyoendelea na kazi ya uokozi

3. Shukrani Kwa Waziri Lukuvi Kwa kusimamia zoezi muda wote Bila kuchoka

4. Shukrani Kwa RC Chalamila ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi Kwa kazi kubwa

5. Shukrani Kwa Watendaji wote wanaendelea na Uokoaji

6. Shukrani Kwa Watanzania wote Kwa michango yao mbalimbali, Dua zao na Sala zao Ili Mungu wa mbinguni atufanyie Wepesi kwenye zoezi hili

Dr Nchimbi amesema Chama Kiko tayari kutoa msaada wa aina yoyote inayohitajika Ili kuipa Wepesi Serikali yake katika zoezi hili

Ahsanteni sana

Soma Pia: Live Updates Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Watu 7 wengine waokolewa

===============
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt Emmanuel Nchimbi amevishukuru vyombo mbalimbali vya uokozi Kariakoo kwa namna vilivyopambana kuhakikisha maisha ya Watanzania waliokwama chini baada ya ghorofa kuporomoka, yanaokolewa na ametaka kasi zaidi ya uokozi iendelee ili wale waliosalia watoke salama.

Dkt. Nchimbi ameyasema hayo leo November 17,2024 alipofika eneo la tukio Kariakoo na kutoa pole kwa Familia zilizopoteza Wapendwa wao na wale waliojeruhiwa na kuwaombea wapone haraka pia amewashukuru Watanzania walioanza zoezi la uokozi baada ya maafa kutokea na ameipongeza Serikali ya CCM na timu mbalimbali zinazoendelea kuchukua hatua mbalimbali za uokoaji.

Credit: Ayo

Huyu ndio Kiongozi 🐼
Watu wanapoteza maisha mpuuzi analeta siasa unataka chama kiombwe msaada na hali mna macho mnaona leteni whinch clain za bandari ongeza exctor za kupangua vifusi sio unatwambi chama
 
Chawa umehama reli mara hii
No gentleman,
ni katika kushauri na kurejesha chadema kiungane tena kiwe kimoja ili hatimae huenda wakapata moyo na wakaona umuhimu wa kuja kutoa faraja kwa waTanzania, kama ambavyo CCM wametangulia kufanya kwa niaba ya waTanzania wote.

Au nimesema vibaya ndrugu zango wadau?🐒
 
No gentleman,
ni katika kushauri na kurejesha chadema kiungane tena kiwe kimoja ili hatimae huenda wakapata moyo na wakaona umuhimu wa kuja kutoa faraja kwa waTanzania, kama ambavyo CCM wametangulia kufanya kwa niaba ya waTanzania wote.

Au nimesema vibaya ndrugu zango wadau?🐒
Chawa mpambe
 
UOKOAJI KARIAKOO NI USHUHUDA WA MOYO WA UTANZANIA: NCHIMBI .

Apongeza wananchi wa kawaida kwa kujitokeza haraka kuokoa watu

Serikali, vyombo vyake na taasisi binafsi zapewa heko kwa mwitikio wa mfano

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amepongeza utayari na mshikamano ulioonyeshwa na Watanzania mara baada ya tukio la kuanguka kwa jengo Kariakoo, akisema kuwa hatua hizo zimeonesha uzalendo na moyo wa udugu uliojengwa ndani ya Taifa letu.

Akizungumza leo, tarehe 17 Novemba 2024, alipotembelea eneo la tukio, Balozi Nchimbi alitoa pole kwa familia za waliopoteza maisha na kuwapa faraja waliojeruhiwa, huku akisisitiza umuhimu wa mshikamano katika nyakati za dharura.

“Kwa namna ya pekee, napenda kutoa pole zangu za dhati kwa familia za wenzetu waliopoteza maisha. Maisha ya kila Mtanzania yana thamani kubwa. Tunaomba Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi,” alisema Balozi Nchimbi.

Aidha, aliwafariji majeruhi akisema:,’Kwa walioumia, walioko hospitali na hata waliotoka, tunawaombea uponaji wa haraka. Mwenyezi Mungu awajalie nguvu na afya njema ili muweze kurejea katika shughuli zenu.”

Shukrani kwa ushirikiano wa haraka

Balozi Nchimbi alitoa shukrani za dhati kwa wananchi wa kawaida waliokuwa mstari wa mbele mara baada ya tukio hilo kutokea.

“Shughuli za uokoaji zilianza mara moja, zikiongozwa na wananchi wa kawaida. Hii inaonesha moyo wa Utanzania wa kweli, ambapo unapomwona mwenzako kwenye shida, unaacha kila kitu na kumsaidia. Nawashukuru kwa moyo huo wa kipekee,” alisisitiza.

Serikali, vyombo vyake na taasisi binafsi zapewa heko

Katika hotuba yake, Balozi Nchimbi aliipongeza Serikali na vyombo vyake, hasa Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), pamoja na timu zake zikiongozwa na Waziri William Lukuvi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, na taasisi mbalimbali zilizoonesha mshikamano wa dhati katika kuhakikisha maisha yanaokolewa.

“Serikali inafanya kazi yake kwa ufanisi. Hiki ndicho tunachotarajia kutoka kwenye Serikali za CCM—kuwa na uwepo wa karibu wakati wa matatizo. Nawashukuru wote mnaoendelea kuwa hapa kushughulikia hali hii kwa ari kubwa,” alisema.

Aliongeza kuwa juhudi za vyombo vya ulinzi na usalama, taasisi binafsi, na wadau wengine zinapaswa kupongezwa kwa moyo wa kujitolea.

CCM yaahidi ushirikiano zaidi

Balozi Nchimbi alihitimisha hotuba yake kwa kusisitiza kuwa Chama Cha Mapinduzi kinaunga mkono juhudi zote za uokoaji na kiko tayari kutoa usaidizi wowote utakaohitajika.

“Uokoaji huu haupaswi kusimama. Kila maisha yanahesabika. Kama chama, tupo tayari kushirikiana ili kuhakikisha watu zaidi wanaokolewa,” alihitimisha Balozi Nchimbi.
 

Attachments

  • IMG-20241117-WA0396.jpg
    IMG-20241117-WA0396.jpg
    420.3 KB · Views: 1
Ni ufedhuli uliopitiliza kujenga platform ya siasa kwenye roho za watu.
 
Back
Top Bottom