Dr. Ndalichako stand for your own dignity....

Dr. Ndalichako stand for your own dignity....

duocore

Member
Joined
Aug 27, 2012
Posts
55
Reaction score
5
Wana JF hivi karibuni matokeo ya kidato cha 4 yametangazwa tena na Waziri katika hali ambayo haikuzoeleka. Dr. Ndalichako kama mwanafalsafa na mama hakuonekana kuwa na furaha juu ya matokeo hayo. Kimsingi athari za matokeo haya ni kubwa, mf. ni wangapi watafaulu kwenda elimu ya juu? Udahili utakuwa mdogo vyuoni, fani zingine zitakosa wadahiliwa, wahadhiri watafanya nini? Dr. Ndalichako kama mwanafalsa na mama, simamia utu wako, pumzika mama yetu, wanasiasa watakupelekesha mwisho uonekane kuwa ovyo.
 
duocore kama anatenda na kufanya haki ,hana haja ya kupumzika.Sababu yeye ni kiongozi wa watunga mtihani na wasahihishaji.Ila mwenye dhamana kubwa ni waziri,naibu waziri na katibu wa elimu wanaojua hali halisi ya walimu wetu,na shule zetu.

Zamani mzazi wa mtoto alikuwa anapigania mtoto wake aende shule za serikali kwa kuwa na walimu wengi na wazuri lakini leo ni tofauti.

Watanzania kwa umoja wetu tupiganie haki za walimu ili watoto wa taifa hili wapate elimu bora na si bora elimu.Tuanze sasa tukisubiri tutakutana na jua la asubuhi.
 
kwanini apumzike?baraza la mitihani jukumu lake ni kutunga, kusimamia, kusahihisha na kutoa matokeo, kama wanafunzi hawakufunzwa huko mashuleni na hivyo wakafeli hilo sio kosa la Baraza.

Ni mpumbavu tu ndiye anaweza kulilaumu Baraza la Mitihani kwa matokeo haya.
 
Ni Kweli. Dr. Ndalichako simamia taaluma, na Falsafa ulizokabidhiwa kuzitekeleza. Watanzania tunakuamini katika utendaji wako. Waache wanasiasa waendeleze maneno yao.
 
I believe in Ndalichako anafanya haki kama umefeli that's it
 
Siwezi kuamini alichokise mhe. kuwa matokeo ya mitihani kidato cha 4 ni uthibiti bora wa mitihani, je katika kipindi cha nyuma kabla wizi haujaanza kutokea wanafunzi hawakuwahi kufeli hivyo. Matokeo haya ni muunganiko wa mambo mengi, mitaala isiyoeleweka, masilahi duni kwa walimu, mazingira magumu ya kufundisha na kujifunzia, walimu kutolipwa malimbikizo yao, kwa hiyo siasa ziwekwe kando, miaka 3-5 ijayo madaktari, wahandisi, nk watazalishwa wachache.
 
Dr. Ndally kadhibiti mambo mengine ikiwa ni pamoja na wizi wa mitihani. Mimi naomba shule zirudi zilikotoka kwenye misingi. Walimu waachwe wafanye kazi zao, na wazazi watimize wajibu wao. Kuna mengi ya kutisha ukiongea na walimu. Watoto nidhamu hawana wanawafanyia walimu vitendo vya ajabu ambavyo ni udhalilishaji. Wanafunzi watukutu wanapofukuzwa maafisa elimu wa wilaya na mikoa wanawarudisha hao watoto shule walizofukuzwa. Je mwalimu aliyedhalilishwa atafundisha tena kwa ari ileile? Walimu wakuu siku hizi hawana nguvu. Tumekosea mengi lakini nafikiri shule za sekondari zisingekuwa chini ya halmashauri. Hao maDED wengi wao sidhani kama wanaipa elimu kipaumbele.
 
Kweli hii inaonesha wizi umekomeshwa hakuna feki
 
duocore kama anatenda na kufanya haki ,hana haja ya kupumzika.Sababu yeye ni kiongozi wa watunga mtihani na wasahihishaji.Ila mwenye dhamana kubwa ni waziri,naibu waziri na katibu wa elimu wanaojua hali halisi ya walimu wetu,na shule zetu.

Zamani mzazi wa mtoto alikuwa anapigania mtoto wake aende shule za serikali kwa kuwa na walimu wengi na wazuri lakini leo ni tofauti.

Watanzania kwa umoja wetu tupiganie haki za walimu ili watoto wa taifa hili wapate elimu bora na si bora elimu.Tuanze sasa tukisubiri tutakutana na jua la asubuhi.
Comrade umeongea mambo ya maana sana asante sana mwenye kusoma na akaelewe hii hoja yako
 
Back
Top Bottom