Dr. NDODI: Kuvaa suruali kuna madhara kwa wanawake

Dr. NDODI: Kuvaa suruali kuna madhara kwa wanawake

mtanzania ukitaka kumficha kitu weka kwenye maandishi, kamwe hatayagudua. We kama maneno ya ndodi hayakufai yapotezee, si kwamba wote hayatufai. Ukiyafanyia utafiti kwenye maandishi utakuta Ndodi yuko sahihi. Sasa we unayebishi umeisaidia nini jamii ya watanzania ambayo inahitaji kuelimishwa na ninyi mnaojiita wasomi? Ikiwa hata mkutano wa hadhara hujawahi itisha hata mtaani kwako, jamii yateseka na ujinga
 
kuhusu mwanamke kuvaa suruali inakuwa ni kosa tu iwapo jamii anayoishi haina utamaduni huo,na ni kukosa adabu iwapo jamii yako haikubali hilo.na kuhusu madhara ni kuwa wewe unaevaa suruali kinyume cha utamaduni biblia inaeleza kwenye torati kuwa " na haimpasi mwanaume kuvaa vazi la mwanamke na wala haimpasi mwanamke kuvaa vazi limpasalo mwanaume" maandiko haya yanaruhusu mavazi yote kwa watu wote isipokuwa yasigongane na utamaduni wa kwenu na wala yasigongane na utamaduni wa kule unakotembea nje na kwenu.uwe makini kwenye mavazi kwa kuwa mavazi hutambulisha tabia zako.kwa mfano kuvaa nguo zinazoonesha viungo vya ndani ni wazi wewe kama ni msichana ni mgawaji mno na ndio maana unatangaza hiyo biashara yako.
 
Naweza kuamini kuhusu kitambi lakini maji si kweli maan tokea nianze kuvaa mpaka leo ingekuwa bwawa na si maji tu.
 
Uchina, vietnam, Laos, Japan, Taiwan, Korea, Singapore, Mynamar, Karibu kila mwanamke katika nchi hizi huvaa suruali kwa muda mrefu katika maisha yao. Hapo bado hujarudi wa Wazungu Kuanzia Urusi hadi Ireland, Nenda kwa wamarekani na canada, pamoja na utaalam wao wote wa kisayansi, hakuna hata siku moja zimeonekana kuhusiha vitambi na suruali. Ndodi ni Mzushi kwenye suala hili. Mbona Ma"miss" wengi Tanzania wanavaa suruali na matumbo yamenyooka?
Bora angesingizia bia na chips kwenye suala la vitambi, lakini sio suruali. Kuhusu suala la maji "kusini", Ni UONGO mtupu.
 
Kuuliza si ujinga: Dr Ndodi ni daktari wa nini? Yaani specialist au GP au AMC? Maana kwa kum-judge based on the above, udaktari wake unaendana na ule wa Prof Majimarefu.
Mwanamke kuvaa suruali inaweza kumwepusha na madhara mbali2 ya kiafya na kijamii sasa anapojaribu kurudisha wanawake into stone age naona ni vyema ikiwekwa bayana kuwa ana utaalam gani.
 
Jizi na tapeli lililo kubuhuu hiloo, tena serikari ilisha piga marufuku matangazo ya waganga wa kienjeji lakini hili jizi bado linaendeelea kujitangaza kwenye ma tv kila kukicha, sijui ni kwa nini linajiita dr. Wakati ni ligagula tuu lililokubuhu tena linajitangaza ohooo natibu ukimwai, mara ohoo natibu kisukari, mara ohoo natibu pressure kumbe linawatapeli watu tuu hivi wizara ya afya imelala wapi jamanii ?
 
Lakini huyu dr ni nouma... Mungu kamjaalia kweli ulimi wa kutudanganya na kuyakubali..mmh sijui science ya chuo gani ile!!
 
kweli duniani kunawatu wenye vipaji vya kuongea yaani utasema wamechanjia. Lakini lisemwalo lipo...
 
ndodi ni mzushi,mwaka juzi alianzisha mjadala kwenye redio free akiwataka wakristo wanaokula nyama ya nguruwe iwapo kama yupo mwenye aya ya biblia inayoruhusu mkristo kula nguruwe asomewe aya hiyo nayeye ndodi atamzawadia gari mwenye kutoa hiyo aya,basi mimi nikamwandikia meseji nikimtaka na yeye ndodi anipe aya kutoka ndani ya biblia hiyo hiyo inayosema kuwa mkristo asile nyama ya nguruwe hajanijibu hadi leo.jamani huyu ndodi ana sumu kali kwenye mdomo wake na watu wengi sana wanamkubali.je jamani tufanye vipi ili tuuokoe huu umma na nabii huyu wa uongo ambaye ni ndugu ndodi? ndodi ana ujumbe wa hatari na anasonga mbele huyu.
 
Jamani kama mtu una chuki binafsi usiziweke humu, kama mtu haujafanya utafiti wa kisayansi ya vyakula usilete siasa hapa, eti aya ipi inasema usile nguruwe hata kama ipo inaonekana hautafuata maana sio wote tunafuata mafundisho ya kidini, tusiwaite wengine waongo au wazandiki bila kuwa na justfication. Kama vipi nenda kinyume na ulaji anofundisha uugue kisukari ndio uende kwake akupe dawa na masharti ya mpangilio wa chakula uufuate alafu mwisho usipopona ndiyo hapo umkosoe.

Mafundisho ya ndodi kuhusu lishe na dawa ni sahihi kabisa. Kuhusu kuvaa suruali ndodi hajasema wanawake wasivae suruali bali wasivae suruali za kubana mtu anasema wazungu na wachina wanvaa suruali lakini hujaweka wazi ni za aina gani wachina wanavaa cotton na si za kubana wazungu asilimia kubwa wanavaa kaptula au suruali nzito wakati wa baridi. Hebu angalia wale black Americans wanaovaa tight trousers walivyo na vitambi na maumbo mabaya. Mwingine anadiriki kusema tangu ameanza kuvaa suruali za kubana mpaka sasa ingekua ni bwawa nakushauri uwe unasikiliza vizuri siyo kwamba maji yanatoka wakati wote bali wakati mahsusi pale unapopata mguso au unapokua faraga sasa endelea siku usipoachwa kwa kumfanya samaki mzee wakati anaingia ikulu.

Nawashauri ndugu zangu kama mtu unataka kupinga kitu kilichofanywa kiutafiti fanya utafiti wa aina ile ili uone matokeo ni yaleyale au tofauti? Tuache blabla watanzania, hasa pale maslahi yetu yanapoguswa vibaya. wachina wanaleta dawa zao, wazungu wanaleta wala hatuongei kitu ingawa zina kemikali zenye madhara mwilini sasa mwenzetu kaja na dawa isiyokuwa na side effect mnamtukana. Jamani ingia google search omega wash
 
Kwa hiyo ndodi ndio kafanya utafiti kuhusu uvaaji suruali? Umeuona huo utafiti? Hao wazungu na wachina wanaovaa suruali zilizopwaya wanavaa wakati gani? Ninachojua mimi ni kuwa most of the time kwanzia majira ya autumn, winter na spring suruali wanazovaa zinabana kama wanazovaa mamiss wa Lundenga na hakuna vitambi. Wakati wa summer ndio labda wanavaa zilizopwaya.

Na chakula mwilini kinasafirishwaje? Kinapita kwenye ngozi kama kinavyopita kwenye phloem ya mimea? Hapana. Kinapita kwenye damu, na mishipa ya damu haizuiliwi na nguo yoyote, labda ufunge kamba kama unavyofunga mzigo wa kuni na tena ufunge muda mrefu haswa mpaka sehemu zingine zivie. Hao blacks wa marekani uliowaona na vitambi wakiwa wamevaa suruali, una uhakika gani kuwa ni kwa babu ya suruali? Unajua wanavyofakamia junkie food pamoja na ulabu? Unajua life style yao, dieting, excercising? Au kwa vile Ndodi kasema? Halafu unakubali kabisa kuwa uvaaji suruali unaongeza maji kule kusini? My brother, unahitaji kusoma zaidi kuhusu human physiology and anatomy....

Hata kama Ndodi amewahi kuongea vitu vya ukweli, ukavikubali, haimaanishi basi kila kitu tu anachoongea uamini. Mengine anayoongea hayako based kwenye sayansi, badala yake yako based kwenye HISIA. Kuna siku nilimsikia akisema wazungu wana akili kwasababu wanakula ngano! Na hilo unalisemaje? unaamini tu kwa vile ndodi kasema? Na akikuambia ukila sukari nyingi utapata kisukari utaamini tu kwa vile ni Ndodi kasema? Mambo mengine anayoongea yanafanana na ushauri uchwara unaokuwepo kwenye magazeti ya Shigongo....
 
Nanren simaanishi kuwa lazima mtu ukubaliane na kila jambo au kila kitu anachosema ila unapokosoa na kusema huyu Ndodi ni jizi mzandiki na kila iana ya tusi ndipo kosa linapoingia. Mfani mzuri ni hapo ulivyoeleza against my observation umetoa ufafanuzi wa kisayansi yaani mtu anawezasoma akelewa tatizo hili dawa yake ni hii na mbadala wa dawa ni nini. Ambapo kwa kumpinga ndodi kwa kusema tu huyu jamaa mwivi etc utakuwa hujasidia jamii bali tutona unachuki fulani tu, sema ndodi anasema mwanamke ukiwa na kitambi kusini kutajaa maji, hapa kwa utafiti wangu Nanren siyo maana ndodi hajasema saikolojia au anatomy inachanganuliwa vipi katika hili.

Nadhani kwa stlye ya kuweka mbadala wa uongo wa mtu yaani ukweli wa jambo ni bora kuliko kumtukana au kukashifu mtu. Unapoweka ukweli jamii itamdharau na kuachana nae au nyendo zake.
 
Sawa ndugu yangu. Nakubaliana nawewe, matusi na kukashifiana hakufai. Ni bahati mbaya tu naona ubishani ukizidi, mtu anastukia keyboard imetema matusi au kashfa. Bahati nzuri, nafikiri mimi binafsi nimejitahidi kuji-control.
 
wanaume simngekuwa mnavaa pumpus??????
 
Back
Top Bottom