makoye2009
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,638
- 1,218
Hilo halishangazi hata kidogo. Katika wale million 23+ waliojiandikisha:-
Kuna watu kwa sababu mbalimbali hawawezi kupiga kura (kusafiri, kuugua nk)
Kuna kundi kubwa waliochukua vitambalisho vya mpiga kura kwa lengo la kuwa na kitambulisho tu ili wakihitaji kwa mfano kusajili simu isiwe shida.
Kuna watu ambao shughuli zao za kuingiza kipato hazikuwapa nafasi ya kupiga kura. Baadhi ya waendesha bodada kwa mfano, wasingeacha kuchukua abiria eti akapange foleni ya kupiga kura.
Kuna watu huwa hawana sababu yoyote ya maana. Kama waliopiga kura wamefikia zaidi ya asilimia 60, ni kiwango kikubwa kwa vigezo vya nchi nyingi.
Sibonike;
Well said.
Hata hivo haiwezekani watu karibia milioni 10 wote wakawa na udhuru wa kibiashara au dharura za kifamilia achilia wale walioitwa kwenda mbele ya haki. Hatuna death rate ya mamilioni au malaki kwa kipindi kifupi kiasi hicho ukiangalia zoezi la BVR lilichukua muda gani.
Pengine idadi kubwa iliyoathirika kwa kukosa kupiga kura ni ya Wanafunzi wa vyuo Vikuu walionyimwa haki hiyo maksudi na NEC ili kupunguza kura za Wanamabadiliko ambao wengi walikuwa ni vijana hasa kutoka vyuo Vikuu na vya Kati.
Lakini pia takwimu za NEC kuhusu idadi halisi ya Wapiga kura zinahitaji uhakiki wa hali ya juu kupata idadi halisi.