Elections 2015 Dr. Pombe Magufuli, Rais mteule wa Tanzania awamu ya 5

Elections 2015 Dr. Pombe Magufuli, Rais mteule wa Tanzania awamu ya 5

Niliisha andika huko nyuma kwamba CCM ikishinda ktk uchaguzi mkuu wa mwaka huu na Chadema chini ya Lowassa ikashindwa, hakuna kingine kitakachofuata na huo utakuwa ndio mwisho wa Chadema.

Kwa msingi huo itakuwa ni ndoto kwa Chadema kushika dola ndani ya miaka 50. Subirini muone.

Wabunge wa cdm hawatakuwa na makali tena bungeni ya kukemea ufisadi na watakapojaribu kufanya hivyo watazomewa na wabunge wa ccm. kupoteza makali ya kukemea ufisadi kutawafanya wanachama wa cdm kuangalia chama mbadala. wanachama wanapokikimbia chama ndio mwanzo wa kufa hicho chama.
 
Hahahahaaaaaa CCM haihitaji serikali ya mseto maana inajitosheleza mkubwa. Cha mwisho, issue ya madaraka ni ya kikazi zaidi na si kufurahishana au ulaji kama inavyotamkwa na wengi. Hapa ni kazi tu na si kufurahishana wala kujuana. Na Magufuli akitaka afeli basi ni rahisi sana. Atengeneze serikali ya kujuana na si kufanya kazi za watanzania kwa weredi na uaminifu. Namfahamu vyema na naamini hilo halitakuwepo.

Nyangomboli,

Kuna swali moja kwenye Biblia wale Mitume 11 walimwuliza Bwana Yesu baada ya kufufuka kwake kama alikuwa yeye ni mgeni katika Yeruselamu baada ya kumwona kama alikuwa haelewi habari za Kufufuka kwake.

Sasa na mimi nakuuliza wewe ni mgeni katika Tanzania hii?? Kule Zanzibar tuna Serikali gani kama siyo Serikali ya MSETO wa CCM na CUF??? Hivi kwanini watu huwa mnakurupuka kujibu hoja nzito kwa hoja nypesinyepesi?
Angalizo hapa ni kwamba KURA ZA CCM pamoja na kuiba zinazidi kupungua UCHAGUZI mmoja hadi mwingine, Kiwete aliingia kwa kishindo cha 80% mwaka 2005 na mwaka 2010 zikawa 62% na leo ni 58%.

Kule Visiwani wanmekuwa wakitofautiana kwa kura chace sana 0.2%, 1 au 2%. Sasa kama mpinzani ana 42% na wewe CCM una 58% unaona ugumu gani kuwashirikisha wennzako kuungda Serikali? Kuna dhambi gani hapo? Hivi watu mnafikiri 42% ya wapiga kura unaweza kuipuuza tu kwa vile umejitengenezea mazingira na sheria za kibabe kama za Komandoo wa Zanzibar kuwa ushindi ni ushindi tu hata kama ni nusu mtu kama yupo?? CCM wanatia jeuri kwa sababu ya hii sheria ya SIMPLE MAJORITY ambayo kiukweli siyo sheria nzuri maana si ya kidemkrasia baali imekaa kibabe na kidikteta zaidi.
 
Kuanzia diwani mbunge na hatimae raisi sikuipoteza kura yangu kwakweli. Nilikaa kwenye foleni wakati wakujiandikisha, nilikaa foleni kupiga kura, nilikeshe kwenye maombi kuombea amani nchi na kiongozi bora, kwa hakika hakuna ambacho hakikuzaa matunda. Neema imefunguliwa tanzania heko kwenu nyoote sas na turudi kulijenga taifa kwa umoja.
 
katika watu waliompigia johni magufuli na kushinda wameiokoa tanzania katika makuja ya ufisadi.
nchi hii ingeingia kwenye makucha ya dhahama ya tanzania kundi la lowasa kubwa kwa kujinufaisha kwa kundi hilo asanteni sana mmeiokoa tanzania
 
alaumiwe aliyewasababishia watanzania ujinga na umasikini maana ndivyo vitu viwili vikuu vinavyowasababisha watanzania waichague ccm

Nasema kama ukawa tutamsimamisha fisadi mna haki ya kutukata!
Mh. Mdee
 
Nimemwambia mwenyekiti wangu wa kule kijijini ajipange kupokea mil 50 na pia mwwenyekiti wangu wa mtaa kupokea mil 50. Ni raha tupu

Nami nimemshauri mzee wangu mwalimu Chacha ambaye alitegemea kustaafu mwaka huu asubiri apate laptop kwanza ndio astaafu.
 
Magufuli ndio wale wale hawezi kutubu kwani kutubu in lazima ukawaombe msamaha uliowakosea
 
Ushindi wa magufuli ni ushindi wa ccm ambayo ni ile ile tusitarajie mabadiliko. Miaka mitano au kumi ya elimu duni, ukosefu wa huduma bora za afya na umasikini. Tutarajie ndioooooooo pale mjengoni.

wengi wenu hamumjui magufuli vizuri.. either way ni haki yenu kuongea mnachojickia
 
Leo nina Furaha sana mzee Magufuli kachaguliwa kua Rais wa Tanzania..Upinzani umejikaanga kwa mafuta yao wenyewe kama yule mnyama yule anaitwaje sijui.
 
Kinana apewe viti maalumu tuone alafu apewe uwaziri mkuu tuone kama hatakuwa waziri mzigo wa karne.

we humjui kinana ndugu yangu ila wapinzani wanaomfaham vizuri waliogopa sana walivosikia ndo ataongoza ile timu ya watu wa kazi 32 iliyoundwa kumkabili lowassa... pumzika tuu rafik yangu
 
Hivi unajisikiaje, hasa pale unapogundua kiuhalisia kuwa mkeo au mmeo hakukubali, hakupendi, ila basi afanyeje hawezi kuondoka maana umemuwekea walinzi wa kumzuia asiondoke kwako.
Kwa hali kama hiyo unapotoka na kurudi hapo kwenu; unafurahi kumkuta yupo? Au je yeye anafurahi kukuona umerudi kwake?

Nikijielekeza kwenye uchaguzi mkuu uliomalizika sasa; fikara yenye kufanana na mfano huo halo juu ilipita akilini mwangu.
Kuwa ccm hii yenyewe inajua fika kama haikuwalazimisha watanzania kuendelea kuwa nayo! Kama vile watanzania walio wengi wanavyojua ndani ya nafsi zao mapenzi yao kwa chama tawala kwamba ni ya hiyari au ni ya lazima!

Aghalabu ni vyepesi kama nini kuwadanganya watu wengine kuliko kufanya hivyo kwa nafsi yako mwenyewe.
Ndiyo maana baada ya uchaguzi huu unaweza kukuta mtu anashangilia nje lakini kwa ndani nafsi yake inamkanya ikisema muongo wee!

Mungu ni shahidi mwaminifu amina!
 
Back
Top Bottom