Wandugu,
Nashukuru sana...tena sana kwa kuona na kuthamini mchango wangu hapa JF sana katika jukwaa hili la JF Doctor. Ahsanteni pia kwa dua, Husninyo ahsante 'free style'! Najitahidi kila pale ninapoweza kuchangia na/au kushea nanyi elimu hii ya utabibu na afya nikiamini kuwa kuna matatizo mengi ambayo hata wengine hawawezi kuongea na daktari wake, lakini anayamwaga hapa na tunajadili. Najua jukwaa hili lina madaktari wengine, manesi na wadau wengine mbali mbali wa afya ambao wana michango mizuuri tu, nami mara kwa mara najifunza kwao na kwa wachangiaji wengine pia! kwa kifupi ni jukwaa nilipendalo...
Nilifanya kazi kama daktari kwa miaka kadhaa Muhimbili, nikapata matatizo na mwajiri wangu (Wizara ya Afya), nikawa frustrated sana na kupractice clinical medicine, nikahamia kwenye utafiti wa masuala mbali mbali ya afya. Nimejikita zaidi kwenye 'afya ya jamii' kwa sasa, sitibu tena...hivyo sina hospitali ninayofanya kazi kwa sasa.
Lakini mara zote unapohitajika ushauri/ufafanuzi ambao upo ndani ya uwezo wangu, au issue ambayo naweza soma zaidi ili kuweza kushea nanyi nijuacho, basi karibuni kwa kuanzisha thread hapa jukwaani...au hata kwa PM...ni furaha yangu pale ninapoweza kusaidia.