Hapo suala ni straight forward, unaambiwa na wenzio umekosea, wewe unadinda bila sababu.
Unajikaribishia kula vumbi.
Nadhani kuna haja ya katiba mpya. Mara nyingi kumekuwa na ugomvi wa chinichini baina ya wakuu wa mikoa na mawaziri. Kwanza waziri wa kilimo au wengineo huwezi toa maelekezo ya moja kwa moja kwa Mkuu wa Mkoa. Kwa sababu kiprotokali hawa wako rank moja. Ndo maana unaona hata mkuu wa mkoa wa Dodoma alitunishiana na waziri wa Elimu kuhusu maagizo ya masomo ya ziada.
Miaka ya Nyuma kulishawahi kutokea hivyo hivyo vurugu baina ya wizara na Mkoa. Wizara inatoa maagizo mengine Mkoa nao unamsimamo wake.
Ilibidi waziri Mkuu Pinda aingilie kati kuitisha kikao ili kuwepo na utatuzi. Mkuu wa Mkoa alifanikiwa kuteteta hoja zake na hivyo Mkoa na halmashauri waliendeleza kutekeleza walichokuwa wanataka.
Dr. Sengati ni mtu wa misimamo, alijua wazi waziri hawezi muagiza. Ila ilitakiwa tu busara itumike, kujua kuna nini? Sidhani kama atajutia, bado ni kijana, na nimoja ya wakufunzi wazuri. Kuliko unabaki serikalini ktk siasa ati urambe miguu ya wanasiasa. Hii ndo inaitwa hakuna kujipendekeza.
Kama unakumbuka kuna DC fulani wakati wa Kikwete, alimgomea Lowasa na kumwita kijana. Kuna watu hawarambi miguu. Alikuwa ana msimamo huyu DC, kiasi Lowasa na kuogopwa kwake kwa huyo alisarenda!
Wanadai serikali za mitaa zinajitegemea na zinamaamuzi yake bila kuingiliwa kwa mujibu wa katiba, Lakini katiba uvunjwa kila siku. Serikali kuu ndiye amekuwa mwamuzi wa yote. Wanapanga wao kila kitu huko wizarani, serikali za Mitaa zenyewe ni kutekeleza tu. Hii ni kinyume na Katiba ya nchi.
Inafaa hata hawa Wakurungezi wasiteuliwe na Rais. Wakurungezi iwe ni kazi ya ushidani, watu waombe. Mkuu wa Mkoa nae iwe nafasi ya kugombea. Itaondoa huu ukiritimba.
Wewe katibu wa CCM nilikusikia unasema wananchi hatutaki Katiba. Nikuonye na samahani kusema ulitoka usingizini. Kuna mambo mengi yanaweka vipingamizi vya maendeleo kutokana na muundo wa Katiba iliyopo. Rais Kikwete hakuwa mjinga kuanzisha mchakato wa katiba. Anajua tatizo liko wapi.
Katiba hii ikibadilishwa itasaidia kuunda mifumo mingine ya kiutumishi, na kuwa na taratibu ambazo zitaondoa urasmu, na masuala ya rushwa. Halmashauri zinachangia pato la Taifa. Lakini wakati wabajeti, bajeti zao ukatwa na serikali kuu. Hii imefanya maeneo mengine kuzidi kuwa masikini wakati zinachangia pato.