TANZIA Dr. Sengondo Mvungi afariki Dunia

TANZIA Dr. Sengondo Mvungi afariki Dunia

kuna wakati naona adhabu ya kifo ingerudishwa maana hawa watu wanaoua wenzao nawenyewe wangekuwa wananyngwa jamani labda watu wataogoa
 
Mungu amlaze mahali pema peponi. Amen. Sasa ni jukumu letu tuliobaki kutimiza majukumu kwa taifa kikamilifu
 
Sasa bastola nayo ni mali ya Dr M. Hii haikuwa inasemwa, zaidi ni hicho kipakata. Hongereni sana nyinyi mnaotoa ushirikiana na Jeshi Ulinzi naUsalama kawapata maadui wakubwa wa Taifa letu. Achaneni na hawa waliokalia Siasa hata ktk Msba huu wa Kitaifa. Ni WAZALENDO WA UKWELI. MUNGU ATAWALIPA MEMA YENU. MSISITE HATA CHEMBE KUWAFICHUA MAJAMBAZI HAYA PO POTE YALIPO
 
Jamaniii! Sote tutakufa lakini Dr Mvungi ameondoka muda tuliokuwa tunauhitaji wa mchango wake zaidi ktk taifa hili.
Eeh Mungu umpumzishe mja wako; Amen.
 
Naishauri Serikali kuwa ione sasa ni wakati muwafaka wa kuanza na hawa wauwaji ili kumaliza mtandao wa Uhalifu nchini.
Wahojiwe vya kutosha na wale ambao hushiriki vitendo vya namna hii wasajiliwe endapo tukio likitokea tu, wawe wa kwanza kuhojiwa na kuonyesha wahusika kwani wanajuana sanaaa hawa.
Ajizi nyumba ya njaa. Tutahadhari na kamchezo haki kakupoteza WANATAALUMA, hawa watu wanapatikana baada muda mrefu kwa gharama kubwa sana. Kwa hili Serikali ijipange haswa. TANZANIA NA AMANI INAWEZEKANA SANA SANA TENA SANA. Mtaalamu ni wamuhimu kuliko kibaka muuaji. Ah, wajawasikia wanaojiita Haki za Binadam ktk hili, kushauri japo
...............
 
Kiukweli siwezi eleza lolote kuhusu wasifu wake kwani tulikuwa faculty tofauti mimi nilikuwa Biashara ila tulikuwa tunakaa hall moja. Labda niseme tu alikuwa mtulivu sana na mwenye kujenga hoja na mtu serious sana katika mambo ya msingi na alipenda sana vitu vya kitamaduni. Nimekumbusha kitu hapo alipokuwa mwaka wa tatu alifanya Birthday yake na badala ya kutuwekea keki alitulisha chakula cha kikwao (kipare) kinachoitwa KISHUMBA. Na ndio maana kila tulipokuwa tunakutana nilikuwa namwita Dr Kishumba au Mzee wa Kishumba.

Hakika Mola ailaze roho ya Mzee wa Kishumba pahala panapostahiki.

Hata hayo machache uliyoeleza hapo juu, yatosha!
 
Nimepokea habari hii kwa huzuni sana. Alikuwa mwalimu wangu, rafiki yangu na kiongozi wangu. Sisi wanadamu wenzake tulimpenda na mungu akampenda zaidi. Tumetoka kwa m mungu na kwake sote tutarejea. Kwa lugha nyingine bwana ametoa bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe
 
Kwa heri shujaa wa katiba mitego yako walishindwa kutegua wakaona uondoke
 
inasikitisha kuwa kazi yake iliishia kuharibiwa na kutupwa pembeni na akina Sita, lakini Mungu si athumani hata wao wameyalamba mavumbi
 
Back
Top Bottom