Dr. Shayo wa UK si bingwa wa uchumi

..Nyani Ngabu mimi nakuheshimu sana kwa michango yako hapa jamvini. lakini sina nguvu sana ya kuchangia posting hii kwasababu MUANZISHA MADA ana historia ya UDINI na UKABILA.

..naomba michango yangu ktk thread hii iishie hapa.

Hamna tabu ndugu yangu. Nakuelewa.
 

Naomba historia yangu ya udini na ukabila? huwezi kusema unaishia hapa hutachangia kitu kwenye mjadala huu baada ya kunituhumu kuwa mkabila na mdini.unaninyima uhuru wa kuwa mwanachama humu JF na kuchangia ninachokijua.ni kweli watu wakifanyiwa jambo baya kutokana na ukabila au dini nitasema sitaogopa,kama Obama alivyowaeleza waIsrael juu ya Palestine.

Nimekiponda sana chuo cha London School of Commerce wakati Marketing officer wake ni Ally Abdallah,nimeiponda blog ya michuzi kwa kuweka vitu bila kuhoji wakati mmiliki wake ni ISSA MICHUZI wote ni waislam.

najua Dr.Shayo nimemjengea hoja nzito ambazo hawezi kuzijibu,sasa unataka kutumia mwamvuli wa udini na ukabila kumnasua.

Vyovyote itakavyokuwa ukweli unabaki kuwa DR.Shayo ni mtalaam wa mazingira.ningekuwa na nia ya kumchafua ningesema ana phD feki,nimesema sana kuwa jamaa ni msomi na mtalaam wa mazingira hilo halina shaka ila kujiita Associate professor wa uchumi wakati hana hata certificate ya uchumi siwezi kukubali hata ukitumia kinga ya udini na ukabila.

Joka kuu sidhani ngao ya ukabila au udini itakusaidia kitu tunapohoji mambo ya msingi kwa maslahi ya Taifa.

una maana kamala,Nchimbi,Nagu,MATHAYO David,mahanga wanasakamwa kwa dini zao na si phD feki zao?Basil Mramba,Kweka,Mgonja,Yona Daniel,liyumba n.k wanasakamwa kwa kabila na dini zao?

Huna hoja ndugu yangu njoo tushindane kwa hoja unakimbia nini? kama uliona mjadala huu umegubikwa na ukabila na udini kwanini umechangia?michango yako kwa watu wa dini tofauti na wewe huko nyuma umeweka kwa msingi huu wa kidini?
 
mkuu kanda2 hapa JF kama hujapajua watu wakishindwa hoja huwa wanakimbilia ati udini,ukabila.....hilo joka limeshindwa hoja.....
 
Hakuwahi kuwa Lecturer wa uchumi Udsm hii unasema wewe hakuna rekodi hiyo Udsm.
 
mkuu kanda2 hapa JF kama hujapajua watu wakishindwa hoja huwa wanakimbilia ati udini,ukabila.....hilo joka limeshindwa hoja.....

Nimegundua hilo nitawajibu kwa hoja tu nawatakimbia kama yule mtetezi wa London school of commerce alivyoingia mitini. JOKA KUU kuishiwa, anasema Shayo alikuwa Lecturer wa uchumi Udsm kitu ambacho ni uongo mwingine kama ule wa yebo yebo kusema ni Associate Professor wa uchumi.

Nakupa challenge Joka kuu wewe unasema mimi mkabila na mdini nakueleza kuwa mtalaam wa uchumi ni DR.Chami ambaye ni kabila na dini moja na Shayo,namkubali DR.Chami kwa merits na namsema Shayo kwa tabia yake ya kujipata nafasi isiyo yake.sio mchumi PERIOD!
 
swa mkuu unajua JF siku hizi watu wanashindwa hoja wanakimbilia kwa mods kwa kisingizo cha ati udini,ukabila na ubaguzi wa rangi.....

.....kule kwenye jukwaa la siasa GT kaumbuka sana alishaanza kusambaza chuki zake......
wanasema eti alifundusha udsm hakuna aliekataa wala kubisha na hakuna aanebisha kuwa Dr shayo hana Phd ina tunasema hivi sio bingwa wa uchumi...
 

Hakufundisha Udsm kwani hakuna rekodi hiyo.Joka kuu yeye ndio mdini ameshindwa kuwatetea school of commerce kwa vile country marketing office ni muislam na mwenye chuo ni muhindi muislam.

USDM kuna school of business wakati London southbank hawana kitu hicho. watu waliokwenda shule kama DR.ASSAD waliopo UDSM ni nadra kuwaona London southbank.

unajua hata Cambridge university kuna anga sio wazuri sana mfano MBA ukipata cranfield university na Cambridge nenda CRANFIELD wako juu ya Cambridge.

London Southbank wanaweza kuwashinda UDSM kwenye kitengo cha mazingira na construction.
 

Kanda2, nilikwambia umeshinda. Pia USIDHANI ninasoma hapo ila hoja zako na mifano imekuwa zaidi kama habari za kwenye Kiu na Ijumaa.

Binafsi huwa sipendi hoja zinazotawaliwa na hisia, napenda tuwe neutral tukijadili kama watu wanaobadilishana mawazo SI TUJADILI KAMA WAHA au WAKINGA (samahani kwa hao watani zangu) kwa ubishi.

Naomba upitie hii website ya University of Wales, Institute Cardiff University of Wales Institute, Cardiff click sehemu ya partnership
na uone walivyoifagilia LSC, Pia inarecruit students kutoka nchi 120 si Tanzania tu, na kwa taarifa yako Wales wanataka kuanza kupitishia Phd zao hapo.

Pia kumbuka vyuo vyote vya UK vilifanyiwa tathmini upya baadhi vilipewa kibali cha kurecruit students from abroad, vingine vilipewa vibali vya muda na vingine viliruhusiwa ila graduates wake hawataruhusiwa kupewa Visa ya kufanya kazi UK baada ya kuhitimu. Nadhani unafahamu MABADILIKO YALIYOANZA RASMI 31/03/2009 ili kupambana na bogus colleges. London School of Commerce imekuwa rated A.

Hoja ya walimu kwamba idadi ya wazungu haina maana katika academic platform ambayo inajali culture diversity. Pale wapo walimu wasehemu mbalimbali. Kumbuka pia vyuo vya kati vya UK vilivyo makini vimejitahidi sana kuwa vinawacontract lectures kutoka vyuo vikuu mbalimbali.

Hapo mimi nawajua malecture nguli wawili mmoja nilikutajia, na mwingine yupo aliyebuni mfumo wa IT unaotumiwa na magereza hapa UK (Ukihitaji details nitakutafutia details zake nikupe umuhoji mwenyewe.

Suala la intake si hoja, kumbuka hapo pana School mbili (1)London School of Commerce (2) London School of Technology ambayo iko affiliated na University of East London.

Hapa UK hasa London pana vyuo vingi sana vya kati, ni kweli vingi ni bogus na vingi vimenyimwa leseni ya kurecruit overseas students, ndiyo maana unatakiwa kabla ya ku apply uangalie hicho chuo kama ni miongoni mwa vyuo vinavyokubalika kurecruit overseas students.

Kuhusu ukubwa au udogo wa ada hiyo si hoja itakuwa hoja kama tutaijadili under market strategy perspective na siyo kama habari za kwenye KIU NA IJUMAA.

Labda tuwahoji Pinda na Mkuchika wenye hela kwa nini wamewapeleka hapo watoto wao na wasiwapeleke Havard university au Oxford University ila kwa wale wanaodunduliza kwa kuuza kuku, ng'ombe na bata usiwapotoshe. Pia usipende kuwa conservative sana.

Pia hapa nina website zaidi ya kumi zimerank vyuo vikuu vya UK, ila vinatofautiana nisingependa kurudia kwa sababu niliongelea awali accuracy ya hivyo vigezo na wanatofautiana vigezo.

Naomba nikuachie uwanja, ila naona post zako kadhaa umekuwa unanilazimisha nichangie japo sipendi kwa sababu nilizozianisha hapo juu. BILA SHAKA NAKUHAKIKISHIA SINA UBIA UWAO WOTE NA LSC ila si vema kupotosha.

Pia ujue vyeti vyao vya masters na digrii vinatoka moja kwa moja kwenye hizo universities hata mahafali ya masters na digrii yanafanyikia kwenye hizo universities.

Kwa heri nina kazi nyingine za kufanya tutaonana muda mwingine
 
Hii hoja imekaa kama inamlenga mtu na siyo hoja zake. Ni ile wanasalsafa wanaita ad hominem (attacking the person instead of attacking his argument).
 
LOL. Kwahiyo Pinda na Mkuchika wakipeleka wanafunzi hapo ndio shule nzuri?? They are seriously badly advised.
 
Kuna thread nyingine inamuelezea Dr. Kamala!

who is next???? kuna watanzania wengi wenye Phd, sipati picha tungekuwa milioni 300 kama USA au 100 kama Nigeria!
 
LOL. Kwahiyo Pinda na Mkuchika wakipeleka wanafunzi hapo ndio shule nzuri?? They are seriously badly advised.

Msiba mkubwa kama mtoto wa waziri mkuu anasoma shule kama hiyo, pia ni kosa kwa waziri mkuu kusomesha watoto wake nje ya nchi kwani yeye ndio mtendaji mkuu wa serikali bungeni anashindwa kutengeneza sera zitakazoboresha elimu yetu? anamkimbizia ulaya mtoto wake sasa sisi wanyonge vipi?

kusoma mtoto wa Pinda au Mkuchika sio hoja kama commonwealth open university wakasema chuo cha kinatambulika kwani kilikuwa na wanafunzi mawaziri wawili-KAMALA na Nchimbi.

Chuo alichosoma Mary Nagu nacho kitasema kuwa kinatambulika kwa kumpa PhD Mary Nagu waziri mzoefu.

Ushauri kuweni makini mnapochagua vyuo yasije kuwakuta ya kina Kamala mbele ya safari.kusoma ni pamoja na kutengeneza History wa kizazi kijacho, isije kutokea watoto wako wanauliza baba/mama ulisoma chuo gani UK yaani eneo gani utabaki kusema kuna chuo kimefungwa ILA kilikuwa afilliated na CARDIFF.

kama ni kweli Pinda na Mkuchika wamepeleka watoto wao hapo basi wameingizwa mjini kama mikataba ya buzwagi n.k
Kwanini mtu usome Afilliated? kama huna pesa ya kutosha nenda India,MALAYSIA au South Africa ukachukue elimu ya maana sio Afilliated college,hata kama mahafali yanafanyika CARDIFF bado mwanafunzi hatumii Library na walimu wa CARDIFF,huko ni kujidanganya.
 
Unajua hawa jamaa wanafikiria hatujui hii college.
Kuna wanafunzi wanakuja hapa, wakifika wanashitukia wanaenda shule za maana zaidi. Ilishawahi tokea shule ilitaka kung'ang'ania pesa za wanafunzi fulani nawafahamu. Wakapigwa biti kwamba walichotangazia bongo, sio hicho walichokikuta hapo. Wahindi ilibidi watoe hela, si unajua ukijua sheria huku haikutupi.
Nimeshawahi toa mawaidha kwa watu wanataka kuja, ukiwaambia ukweli wanafikiria unawazibia. Wakifika hapa ndo wanasikitika hawakusikiliza. What do I say? Si wabongo hamuelezwi, mawazo kila mtu anawazibia tuu.
LOL.

Anyways, Mwanafunzi yeyote wa PhD lazima aandike paper, prof. yeyote yule, lazima aandike papers ili iwe scrutinised na wasomi dunia nzima. Valentine plagiarism na kuandika kwenye blog sio ubingwa wa kisomo (kama haujawa criticised na wasomi wenzako). Kuandika article kwenye journal unalipwa anything above £10 mtu aki-download paper yako. Namshauri msomi huyu aandike articles alipwe kwa kuchemsha kichwa chake na wasomi wenzake.

Sijui huyu associate prof anawaambia nini wanafunzi wake kuhusu plagiarism. Maana mwanafunzi akifanya, anafukuzwa shule.
 

...........Unaweza ukawa na argument nzuri zaidi bila kuweka huo UPUUZI hapo juu.........
 

......puuulizzzzz.......acha UONGO!!....kwa hiyo walioongoza huko nyuma kabla na baada ya huyo Mzungu waliteremshwa na Malaika!!........nilifikir una point kumbe........anyway ngoja niendelee kukusoma.........i hope sitakuwa napoteza muda.........
 
..................magazeti yote yamekiweka chuo cha mwisho kwenye league table. kwanini mtu aje kusoma chuo kisicho na reputaion wakati Uingereza wana mamia ya university..........!

what is your argument?....ya kwamba Dr. Shayo si mchumi na hajui Uchumi au Chuo alichosoma ranked mwisho kwenye hizo rekodi ulizoziona??
 
LOL. Kwahiyo Pinda na Mkuchika wakipeleka wanafunzi hapo ndio shule nzuri?? They are seriously badly advised.

Kama utasoma vizuri hoja yangu sikuijenga kuwapo kwa hao watoto ndiyo ubora. Nilijenga kutokana na Kanda2 kusema kuwa kwanini uende kwenye chuo chenye ada ndogo. Nimeanisha kuwa ni watanzania wachache wenye uwezo wa kulipia watoto wao kwenye vyuo vikubwa mfano si wengi wawezao kumudu gharama za Oxford ama Havard au London School of Economics. Nimeeleza wengine wanaenda Europe kwa kuuza ng'ombe, kuku na bata n.k.

Nimeshauri Kanda2 awahoji hao ambao ingalau wanaweza mudu hizo gharama kuwa kwanini wasiwapeleke hao watoto wao kwenye hivyo vyuo vikubwa. Ila wengi wa watanzania affordability yao ya kulipa hizo ada anazotaka Kanda2 hawawezi.

PIA NAOMBA NITOE SAHIHISHO NILIPITIWA KUMTAJA MKUCHIKA, NILIYEKUWA NAMTAJA NI JAKA MWAMBI. Naomba samahani kwa usumbufu uwao wote uliojitokeza. Pia namuomba samahani ndugu Mkuchika kwa usumbufu wowote alioupata.
 

Wanafunzi wengi wanakuja Europe wakiwa na dhana ya kufanya kazi (part time) wakifika hapo LSC wanakuta taratibu na sheria zao ni kali na Madarasa ni takribani kila siku. Ukikosa kipindi home office wanafahamu kwa sababu wamefunga mtambo ambao automatic unatoa taarifa home office.

Pia wakikulima barua kopi wanawapa home office, hivyo wengi ratiba inawabana tofauti na vyuo vingine vingi.

Unachosema inawezekana ni kweli au siyo, binafsi sina hizo data ila na data za watu kutaka kukimbia kwa ajili ya ratiba na msimamo wao mkali kuhusiana na mahudhurio.

BINAFSI KWA MTU ANAYEKUJA KUSOMA HALAFU ANATARAJIA ADA NA GHARAMA ZA MAISHA ATAMUDU KWA KAZIN ZA PART TIME NAMSHAURI ATAFUTE VYUO VINGINE ILA KATIKA VYUO VYA KATI TO BE HONEST LSC na LST ni the best.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…