Nimegundua hilo nitawajibu kwa hoja tu nawatakimbia kama yule mtetezi wa London school of commerce alivyoingia mitini. JOKA KUU kuishiwa, anasema Shayo alikuwa Lecturer wa uchumi Udsm kitu ambacho ni uongo mwingine kama ule wa yebo yebo kusema ni Associate Professor wa uchumi.
Nakupa challenge Joka kuu wewe unasema mimi mkabila na mdini nakueleza kuwa mtalaam wa uchumi ni DR.Chami ambaye ni kabila na dini moja na Shayo,namkubali DR.Chami kwa merits na namsema Shayo kwa tabia yake ya kujipata nafasi isiyo yake.sio mchumi PERIOD!
Kanda2, nilikwambia umeshinda. Pia USIDHANI ninasoma hapo ila hoja zako na mifano imekuwa zaidi kama habari za kwenye Kiu na Ijumaa.
Binafsi huwa sipendi hoja zinazotawaliwa na hisia, napenda tuwe neutral tukijadili kama watu wanaobadilishana mawazo SI TUJADILI KAMA WAHA au WAKINGA (samahani kwa hao watani zangu) kwa ubishi.
Naomba upitie hii website ya University of Wales, Institute
Cardiff University of Wales Institute, Cardiff click sehemu ya partnership
na uone walivyoifagilia LSC, Pia inarecruit students kutoka nchi 120 si Tanzania tu, na kwa taarifa yako Wales wanataka kuanza kupitishia Phd zao hapo.
Pia kumbuka vyuo vyote vya UK vilifanyiwa tathmini upya baadhi vilipewa kibali cha kurecruit students from abroad, vingine vilipewa vibali vya muda na vingine viliruhusiwa ila graduates wake hawataruhusiwa kupewa Visa ya kufanya kazi UK baada ya kuhitimu. Nadhani unafahamu MABADILIKO YALIYOANZA RASMI 31/03/2009 ili kupambana na bogus colleges. London School of Commerce imekuwa rated A.
Hoja ya walimu kwamba idadi ya wazungu haina maana katika academic platform ambayo inajali culture diversity. Pale wapo walimu wasehemu mbalimbali. Kumbuka pia vyuo vya kati vya UK vilivyo makini vimejitahidi sana kuwa vinawacontract lectures kutoka vyuo vikuu mbalimbali.
Hapo mimi nawajua malecture nguli wawili mmoja nilikutajia, na mwingine yupo aliyebuni mfumo wa IT unaotumiwa na magereza hapa UK (Ukihitaji details nitakutafutia details zake nikupe umuhoji mwenyewe.
Suala la intake si hoja, kumbuka hapo pana School mbili (1)London School of Commerce (2) London School of Technology ambayo iko affiliated na University of East London.
Hapa UK hasa London pana vyuo vingi sana vya kati, ni kweli vingi ni bogus na vingi vimenyimwa leseni ya kurecruit overseas students, ndiyo maana unatakiwa kabla ya ku apply uangalie hicho chuo kama ni miongoni mwa vyuo vinavyokubalika kurecruit overseas students.
Kuhusu ukubwa au udogo wa ada hiyo si hoja itakuwa hoja kama tutaijadili under market strategy perspective na siyo kama habari za kwenye KIU NA IJUMAA.
Labda tuwahoji Pinda na Mkuchika wenye hela kwa nini wamewapeleka hapo watoto wao na wasiwapeleke Havard university au Oxford University ila kwa wale wanaodunduliza kwa kuuza kuku, ng'ombe na bata usiwapotoshe. Pia usipende kuwa conservative sana.
Pia hapa nina website zaidi ya kumi zimerank vyuo vikuu vya UK, ila vinatofautiana nisingependa kurudia kwa sababu niliongelea awali accuracy ya hivyo vigezo na wanatofautiana vigezo.
Naomba nikuachie uwanja, ila naona post zako kadhaa umekuwa unanilazimisha nichangie japo sipendi kwa sababu nilizozianisha hapo juu. BILA SHAKA NAKUHAKIKISHIA SINA UBIA UWAO WOTE NA LSC ila si vema kupotosha.
Pia ujue vyeti vyao vya masters na digrii vinatoka moja kwa moja kwenye hizo universities hata mahafali ya masters na digrii yanafanyikia kwenye hizo universities.
Kwa heri nina kazi nyingine za kufanya tutaonana muda mwingine