Dr. Shayo wa UK si bingwa wa uchumi

kanda2,

..kama unaona hoja za Dr.Shayo zinazohusu Uchumi zina mapungufu ulichopaswa ni kuzivunja-vunja hoja hizo. siyo kuanza kumshambulia tu kuwa yeye binafsi.

..ni sheria gani za Tanzania inayomkataza mwanamazingira kumkosoa mchumi, ktk masuala ya uchumi?

..kama Dr.Shayo ana interest na masuala ya uchumi kuna makosa gani akiamua kujichanganya?
 
Mimi nilikimbia umande. Lakini kama sikosehi John von Neumann, Alan Turing walikuwa wamesoma math, physics na walitoa mchango mkubwa katika field zingine kama vile computer science na uchumi.

Kinachotakiwa ni mchango katika jamii.
mkuu unajua maana ya "aliebobea" na mtoa michango/mawazo? yeye dr shayo anajiita aliebobea kwenye uchumi ina maana kausoma vema.....
 
mkuu unajua maana ya "aliebobea" na mtoa michango/mawazo? yeye dr shayo anajiita aliebobea kwenye uchumi ina maana kausoma vema.....

I don't know man. Hivi kuna vipimo vya kuonyesha mtu kabobea?
 

Naomba kwanza ufute usemi kuwa mimi ni mkabila na mdini baada ya kukuomba mara kadhaa uthibitishe na umeshindwa kufanya hivyo.

Hakuna sheria inayomkataza DR.Shayo kama mtalaam wa mazingira kuchangia mjadala wa uchumi ila tunachokataa kujivika joho la UNGULI wa uchumi wa level za kina Lipumba na Ndullu.

wewe ni sheria gani uliyotumia kumzuia Nyani Ngabu asichangie mjadala huu? umemzuia yeye na ukasema na wewe hutashiriki lakini wewe unajadili.ulimzuia ukiamini kuwa Ngabu hana uwezo wa kujua ukabila wangu ukihisi ana uwezo mdogo kuliko wewe.
Nasi tunamzuia Shayo kujiita mtalaam wa uchumi tukijua kuwa upeo wake ni mdogo sana kwenye uchumi.

BBC Swahili mara kadhaa wanapokuwa na hoja ya kiuchumi wanamuhoji DR.shayo na anazungumza anachokijua juu ya uchumi,fikiria mamilioni ya watu wanasikiliza BBC inapotokea Shayo anapotosha hakuna anayeweza kujua kwani waandishi wa BBC sio watalaam wa uchumi,unafikiri Flora Nducha anaweza kujua kuwa Shayo anachokisema sio kweli?

uzuri wa mjadala kama huu utawapa nafasi ya BBC LONDON kujua kuwa kumbe DR.Shayo ni nguli wa mazingira na wakiwa na jambo la climate change wanampigia simu na kumuuliza.

sijamjadili binafsi DR.Shayo kwani simjui zaidi ya kuona kazi zake.na hakuna nilikoandika personal life yake.umekimbia kwenye ukabila sasa unakuja na maisha binafsi ya dr.shayo?sijui na wala sitaki kujua maisha yake binafsi.
 
...inaelekea ni mgumu wa kuelewa nilichokisema............

wewe ulisema

.....unajua ilikuwaje hadi mzungu akapewa ukurugenzi wa hospital ya Muhimbili? kwa vile kulikuwa hakuna daktari mzalendo mwenye elimu ya uongozi mzungu alikuwa na MD plus MBA.....

Nami nikasema..........

......puuulizzzzz.......acha UONGO!!....kwa hiyo walioongoza huko nyuma kabla na baada ya huyo Mzungu waliteremshwa na Malaika!!........nilifikir una point kumbe........anyway ngoja niendelee kukusoma.........i hope sitakuwa napoteza muda.........

...halafu unakuja kusema.............


..........nilichosema ni kuwa SI KWELI KUWA yule Mzungu alipewa uongozi Muhimbili kwa kuwa hakuwepo Daktari Mtanzania mwenye MBA...............acha UONGO........na acha kuchanganya mambo ya TENGA.............
 

Wakubwa zangu, hapa ni forum lazima uwepo mgongano wa kimawazo ili maana halisi ya kauli mbiu yetu "THE HOME OF GREAT THINKERS" iwe halisi.

Mjadala huu naamini umewasaidia wengi wanaotarajia kupeleka watoto nje na wanaotarajia kwenda kusoma nje. UMAKINI WA VYUO NI MUHIMU NA HALIPINGIKI, nadhani hata nchi nyinginezo ila hapa UK hususani London ni balaa usipokuwa makini.

Si sahihi kukimbilia kumjengea mtu hoja ya UKABILA amma UDINI. Hayati J.K. Nyerere aliwahi toa hotuba nzuri sana akiwashangaa watu wanao jitambulisha kwa udini amma ukabila.

Naomba kwa pamoja tuzipige vita kwa nguvu zote hoja amma shutuma zozote zitakazotolewa kwa kuhusisha udini. Hii itaishushia hadhi JF. Mfano mimi ni Mkristo siku nikimkosoa mchangiaji ambaye ni mwislamu amma mbudha waislamu ama wabutha waliopo hapa wataanza kuninyooshea vidole vya udini. In fact itakuwa ni UPUNGUANI WA KUPINDUKIA katika ulimwengu wa sasa wa utandawazi kung'ang'ania udini na ukabila ni kufilisika kifikra.

Hakuna Mtanzania ambaye hana umuhimu kwa Taifa/Tanzania. Pia tunahitaji kujenga jamii iliyostaarabika, kuwa mkweli ni moja ya ustaarabu; kama mtaniona mimi niliye kidampa tu leo najiita profesa wakati si kweli na mkakaa kimya bila kunikosoa ATI KWA SABABU SI WAZIRI, NAIBU WAZIRI AMMA SI KIGOGO WA TAASISI itakuwa ni janga kwa taifa. Na itakuwa ni utamaduni kwani nitagombea ubunge na nitateuliwa Naibu Waziri ndiyo muanze kupiga kelele. Nadhani hapo tutakuwa tunakosea.

MUHIMU NI KUANZA KUHARIBU VYANZO, AMMA TUKATE SHINA BADALA YA KUKATA MATAWI NA MASHINA KUYAACHA.

Kwa habari ya MBA in our labour market MBA is a multdisciplinary field, huo ni ukweli usiopingika kwa yeyote ambaye amekuwa akilifuatilia kwa umakini soko la ajira la Tanzania.

Nahitimisha kwa kushauri na kuomba tutofautiane, tupingane na tujadiliane kwa hoja iliyopo na sisi kuokoteza historia kama wenzetu Wazanzibar (SAMAHANINI) wakati wa uchaguzi akigombea mfano Dr Salm (ni mfano tu) wanaanza kumpinga ati aliwahi kuwa mwanachama wa chama cha UMMA hivyo atasaliti nchi. Huko ni uvivu wa kufikiri NA NDIYO MAANA MAHAKAMANI MTU HATIWI HATIANI KWA HISTORIA YAKE BALI ANATIWWAKATI HUO..

Kuhusu Dr shayo nilishatoa maoni yangu, na siko kwenye position ya kukomenti chochote mpaka nijiridhishe na CV yake in details. Members hapa A HATIANI KWA HOJA ILIYOPO MEZANI wamesema ana digrii ya uchumi kama ni hivyo sisiti kumuita Mchumi. KUHUSU BINGWA WA UCHUMI HILO SIJUI KWANI SIJUI POSTGRADUATE STUDIES ZAKE KASOMA NINI. Ifahamike mtu kuitwa BINGWA (kwa kiswahili) au EXPERT (kwa kiingereza) ni lazima awe na kuanzia SHAHADA YA UZAMILI AMMA UZAMIVU

Idumu JF, Idumu michango sahihi ya wana JF na ZIDUMU FIKRA SAHIHI ZA WANAJF
 
Pia wanaomba admission kwenye vyuo vya UK zikiwamo universities nawashauri kabla ya kuomba waangarie kwanza kama chuo anachoomba kimo kwenye orodha ya vyuo vinavyoruhusiwa kurecruit international students.

Pia hivyo vyuo vina magredi, kunavingine ukimaliza hautaruhusiwa kupewa visa ya kufanya kazi UK hivyo anayetaka kumleta mwanaye au anayetaka kuja mwenyewe aangalie kwa umakini grade ya chuo anachoomba

Orodha zote hizo zimetolewa 31/03/2009 baada ya kufanyika ukaguzi

VINGINEVYO HATA VISA ATANYIMWA
 
Thanks for the informtion about dr shayo. kama ni kweli anadanganya then hana sababu ya kuishi uk tena. Ninachojua kuhusu kuishi uk na nchi nyingine za ulaya ni kuwa mkweli aslimia mia. The level of intergrity ni kubwa ninamashaka kama anayamudu maisha yake huko. Bra aje bongo tuendelee kubababa nae. GOOD RESARCH?? MAKE SURE YOU HAVE DONE A GOOD RESEARCH ABOUT HIM OTHERWISE ATAKUPELEKA MAHAKAMANI
 
Hay, Jamiiforums,

Nashangaa, hawa watu wanaopenda kujiita bingwa Wa uchumi, hali wanajua sio. Kwanza, kuwa Mchumi wa Nchi maskini kama Tanzania inasaidia nini?

Tafadhali Watanzania, tuwe wakweli wa kuaminika. Utapeli sio mzuri.

Mkony H. J. N
 
Huyu bwana ni PhD holder kweli lakini sio wa Economics, kafanya first degree ya Economics lakini masters na PhD kafanya za Development Studies kwahiyo sio sahihi watu wakisema ni bingwa wa uchumi.....unless mtu akiwa na first degree anakuwa mchumi aliyebobea
 
Bonyeza hapa http://www3.uwic.ac.uk/English/Partnerships/UniversityAlliance/Pages/LSC.aspx uone UWIC wanasemaje kuhusu London School of Commerce
 
We Lussadam utaweka link zote.
Sasa kwanza hiyo UWIC hata haijulikani kihivyo, labda huko Wales. Ila kwa UK ranking;
University guide 2010: Business and management studies

Iko namba 92, imejitahidi kuizidi South Bank.
Sasa, kama UWIC yenyewe ni mbofu, wakati ndio inaspecialise kwenye hayo mambo, itakuwaje College uchwara ya LSC?

Moja ya 'Campus' (if you can call it that) za LSC iko ndani ya Shopping Centre Ya Elephant & Castle. Yaani Shopping Centre imechoka afadhali hata ya JM Mall sijui J Mall



London's least favourite building 'Elephant & Castle Shopping Centre'




EUROPE'S TOP MBA SCHOOLS

Kama unataka kisomo, kwanini usiende Norway, Holland au Belgium? Bei chini, maisha poa tu. Kisomo cha hali ya juu. Why the hell study at LSC?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…