Dr. Shayo wa UK si bingwa wa uchumi


Mheshimiwa nadhani umeamua kuwapotosha watu kama vile hawaijui UK.

Elephant & Castle kuna majengo mengi, ofisi nyingi hata hiyo South Bank University ipo hapo na kunavyuo vingi pamoja na hiyo shopping Centre ILA SI KWELI KWAMBA IMO NDANI YA SHOPPING CENTRE.

Campus ndogo ya London School of Commerce ipo katika jengo liitwalo HANNIBAL HOUSE lililopo hapo elephant & castle karibu na hiyo shoping centre.

Nilitegemea utaleta picha za majengo yaliyoungua kama ulivosema awali. SASA SINA SHAKA KWAMBA MAWAZO NA FIKRA ZAKO VIMETANGULIWA NA HISIA KULIKO HALI HALISI.

Hizo website zinazorank nimeeleza sana juu ya acuracy yake, na zipo zaidi ya 10 na zote zimetofautiana yaani hazina consistency.

Nakushauri ujitahidi kuwa unafanya Critical analysis.

Bandika hapa picha za campus zao pamoja na madarasa yao.
 
The Elephant & Castle Shopping Centre was closed on Tuesday evening and Wednesday morning after a glass cladding panel shattered at Hannibal House.

jengo limeezeeka, mtaua watanzania wenzetu.

map iliyo kwenye website ya LSC inaonyesha jengo liko ndani ya Elephant & Castle. nakuwekea link. Wakiitoa, tayari nimeshai-download lol.


Map of LSC showing it is within Elephant & Castle



Sehemu gani nimesema nitaleta majengo yameungua?


Wewe hujui kutumia hizo website ku-access data. Nimekupatia ranking ya masomo. Kuna ranking ya Funding, kuna ranking ya quality ya shule overall. Vyote hivyo, ina fail miserably. Tena nimekufanyia favour nimekuonyesha ranking ya somo (inclusive MBA) ambayo ingesaidia kuinyanyua hiyo UWIC. Even that, it is very poor. Unaweza ukakuta University nyingine katika overall ranking iko juu, ila ukija kwenye specific somo, wanaipita nyingine. UWIC ni 'wakali' katika MBA, sasa nimeweka link katima masomo hayo, wako 92!! How miserable is that? Nimekupa ranking ya University za Ulaya ambazo top companies wana-recruit. Kuna shule kama Erasmus ya Rotterdam, moto wa kuotea mbali. Kuna shule Norway. Ningekuwa napotosha, nisingetoa link hizo as alternative. I think I am being more helpful than you ganging-hoeing on a measly, pathetic, next-to-a corner shop, back of the envelope college. If you getting a commission, its cool. But we are here to educate Tanzanians to make better choices.

No one does better university ranking than Guardian or Timesonline. Wanapublish hadi kitabu kwa mwaka. Wao sio wajinga, makampuni sio wajinga.

Kuna university watu wanamwaga michango mamilioni every other week or monthly, kwasababu ya quality ya research.

Sina haja ya kupotosha watu. Kisomo ni kitu muhimu sana, if you gonna pay 4 it, pay for the best.

KAMA HUPENDIKI KISOMO NA UNATAFUTA NJIA YA KUINGIA UK KI-ULAINI, BASI PITIA LSC AND THE LIKES, AND HOPE MAISHA YAKUBALI UNAVYOONA WEWE.
KAMA UNAJIPENDA, NA UNAPENDA KISOMO, USIKANYAGE VI-COLLEGE HIVI. I CANT HATE, I LAY IT AS IT IS. SIWEZI NIKAPELEKA NDUGU YANGU KATIKA COLLEGE KAMA HIZI. MARA MIA NIMPELEKE VOCATIONAL TRAINING KAMA PLUMBING AU ELECTRICIAN, AKITOKA HAPO ANA CHANCE KUBWA SANA YA KUPATA KAZI.

Sasa ukitaka tuzichambue hizi college za chini ya miaka 20 zilizokuwa college za HND, ndio 'new universities', tutaanza kuzichambua, na utaona watu wengi wanaingia mkenge nazo. Wakati kama wanataka kuspend pesa hizo hizo, wanaweza kwenda Uni nzuri zaidi.
 
kanda2 said:
Kwa muda mrefu mdau wa UK Dr.Shayo amekuwa akiitumia blog ya Issa Michuzi na kujifanya kama ni mtaalam wa uchumi toka London Southbank university wakati ukweli ni kuwa Dr.Shayo ni bingwa wa mazingira na hana hata certificate ya uchumi.



..kuna wachangiaji wanadai Dr.Shayo ana 1st degree ya Economics.

..pia wanadai 2nd degree yake ni ya Development Studies. labda wangefafanua hiyo ilikuwa ni Masters in Economics au Masters in Sociollogy.

..kwa upande mwingine mimi nadhani tuweke msisitizo kwa mchango wa mtu katika jamii na siyo hayo ma-credential.

..tumefika mahali mtu anakatazwa asitumikie, hata kwa kutoa ushauri na mawazo, kwasababu ndogo-ndogo kama vile "siyo bingwa" -- hana credentials.

..naamini mazingira hayo ya kuweka premium kubwa kupita kiasi kwenye credentials na haswa ma-PhD, ndiyo imewasukuma wa-Tanzania kutafuta sifa hizo hata kwenye vyuo visivyotambulika. najua pia kuna suala la uaminifu na uadilifu.


..inaelekea hukuelewa tu. nitafafanua.

..sasa hivi kuna vigogo wako sehemu nyeti serikalini na wanatumia vyeti tuko vyuo visivyotambulika. wanalipwa mishahara na marupurupu mengine kutokana na fedha za walipa kodi wa Tanzania.

..kwa mtizamo wangu vigogo hao wana madhara kwa jamii yetu kuliko huyu Dr.Shayo. they are doing the damage right now as we speak/write. zaidi, "kosa" la Shayo ni kudai kwenye blog ya michuzi kwamba yeye ni bingwa wa uchumi, wakati ni bingwa wa mazingira. with the limited time and resources we have nilitegemea priority yetu itakuwa kuwashughulikia vigogo ili kutoa mfano kwa wale wanaofikiria wanaweza kufanikiwa kwa kutumia vyeti feki.

..
 
Last edited:
I don't know man. Hivi kuna vipimo vya kuonyesha mtu kabobea?
Viko vingi mfano awe na masters au PhD.lakini pia awe ameandika journals nyingi za somo lake.sio kutuma mada kwa michuzi ujiite bingwa.
 

Mkuu naona una klemua kama vile vijana wa kidato cha kwanza wanavyokalili.

Ramani inatoa direction na wamenoti alamu muhimu, mfano shoping centre ni alama muhimu, nimekwambia HANNIBAL HOUSE ipo hapohapo jirani kabisa na hiyo shoping centre. Katika picha uliyoweka hapo kuna majengo mawili moja ni mithili kama fullsuti ya jengo la mabati hilo ni tube station (Kumbuka pale ni pakubwa na pana EXIT nyingi) hiyo ni moja wapo ya exit ya tube station.

Hiyo shoping centre ninaifahamu vizuri kwa sababu nilishaitembelea.

LCS wanatumia jengo liitwalo hannibal house

Usifanye generalization, nimetahadharisha toka awali. Nimesema hapa UK zaidi London kuna vyuo vingi vya kati ni bogus, na 31/03/2009 si chini ya vyuo 130 vimenyimwa amma kunyang'anywa vibali vya kurecruit International Students. Rejea kwa umakini posting zangu.

Naujua sana uhuni wa vyuo vingi vya kati hususani vya hapa LONDON, kwani nilifanya survey ambapo nilibahatika hata kuwa interview baadhi ya wamiliki wao. Nikipata muda nitaanda thread niipost kwenye jukwaa la elimu.

Nadhani umeona sijajikita sana kwenye vyuo unavyovitaja pamoja na hicho Norway maana hapa issue ni kwamba LSC NI BOGUS COLLEGE AU SIYO? JE KINA UBORA AU HAKINA? Sasa ukitaja hivyo vyuo na hicho Norway lazima tuwe na criteria ambazo tumekubaliana ndiyo zinatugaidi OTHERWISE NAMWINGINE ATAIBUKA NA CHA JAPANI tutapoteza mwelekeo NA TUTAKUWA TUNAJADILIANA KAMA VILE WALEVI KILABUNI.

Nimetahadharisha kuhusu generalisation, Ukisema hivyo basi nitakwambia twende na vyuo vipo kumi kwa mujibu wa taarifa ya 2008 ambavyo mtu alikuwa akimaliza MBA kwenye hivyo vyuo ALIKUWA ANARUHUSIWA KUOMBA VISA YA KUFANYA KAZI UK BILA YA KUPITIA VILE VIGEZO VILIVYOKUWA VIMEWEKWA (Sina hakika kwa mabadiliko ya 31/03/2009) Miongoni mwa vyuo hivyo ni London School of Economics na Bradford University jumla vilikuwa 10 kwa mujibu wa home office 2008. Japo kati ya hivyo chuo chenye gharama ya chini ilikuwa si chini ya GBP 20,000.00 na cha juu ilikuwa GBP kati ya 44,000 na 45,000. Binafsi nilivipitia vyuo vyote hivyo katika mitandao yao.

Nadhani tusichanganye hoja, tustiki kwenye ISSUE, tuwe na uwigo, Tusifanye generalization.

Kama ni hivyo basi hata TZ tunavyuo vingi tu vya kihuni, je itakuwa sahihi kugeneralize kwamba vyuo vyote vya kati Tanzania ni bogus, havina ubora??? Tutakuwa tumechambua kisomi kweli?

Siajikita pia kwenye hizo link zako kama nilivyoeleza kuwa wanatofautiana katika criteria wanazotumia na pia Accuracy and consistence zao ni more debatable. Nadhani unauelewa mzuri kuhusu tafiti makini inatakiwa iwaje.

KWA MSINGI HUO MIMI NASTICK KWENYE ISSUE ILIYOPO MEZANI, na si generalization na kutokuwa na mwelekeo ndiyo maana sibandiki vyuo vinginevyo si kwamba sivijui vipo nivijuavyo na vipo nisivyo vijua.

Na kwa taarifa yako wanaosoma LSC hawapati hata muda wa kubeba maboksi, nimeeleza system yao ya attendance monitoring ilivyo strictly na ratiba yao ilivyojaa. Kilio kikubwa cha vijana wa LSC ni ratiba ngumu na high digree of monitoring. Nimekwambia pale wanatumia fingerprint, usipo hudhuria mtambo utakutumia SMS automatically kwamba hujahudhuria na Home Office wanapata taarifa automatic kupitia huo mtambo. Sasa hapo muda wa kutafuta unachokiita maisha utaupata wapi?

PENYE UKWELI TUWE WAKWELI, NA PENYE KUKOSOA TUKOSOE, kama ukiniambia kwamba kujazana kwenye kumbi zao za mihadhara kama Bongo japo wanatumia speaker hapo nitakuelewa. Pia ukiniambia wanakabiliwa na changamoto ya kupanua maktaba ili iwiane na idadi ya wanafunzi nitakuelewa.

Na kwa taarifa yako kwa Africa wanafungua Campus Nairobi, Kenya, Asia walishafungua wanayo. Ni chuo kinachokua na kupanuka.

NAHITIMISHA KWA KURUDIA TENA HAPA UK HUSUSANI LONDON PANA VYUO VINGI VYA KATI AMBAVYO NI BOGUS ILA SI VYOTE.
 

Kazi ya mkurugenzi mkuu ilitangazwa masharti uwe na Medicine na sifa ya utawala,kweli wako madaktari wengi wana hadi PhD lakini za udaktari sio uongozi.mzungu alikuwa na medicine na MBA yaani sifa ya uongozi iliyotangazwa.Mfano DR.LEma hana qualification ya uongozi kama MBA au MPA.hivi karibuni imeanza kuna kozi Maters in Public Health inatakiwa madatari wetu wachangamkie.

Land Rover East Africa nao walitangaza nafasi ya kazi ya mkurugenzi awe na digri Ya Engineering na pia awe na ya uongozi. si siri mainjinia wetu wengi hawana sifa(qulification) za uongozi zaidi ya Uinjinia. Tenga alikuwa na vitu vyote viwili vinginevyo kazi ingekwenda kwa wageni. ukitizama MBA umeanza kuchukuliwa na watu wengi hivi karibuni huko nyuma haikuwa rahisi kwa injinia au daktari kuacha kazi yake kwenda kuchukua MBA.
kaka/dada hata ukiniita muongo siumii kwani naweka data na facts ambazo ni somo kwa wengi.
 

Hutakiwi kutoa ushauri kwa jambo usio na ujuzi nalo,unatakiwa ukae na usikilize watalaam wanasema nini? ukinunua dawa ya kichwa labda panadol imeandikwa maumivu yakizidi muone Daktari yaani mtalaam wa fani.huwezi kuongelea uchumi kwenye BBC watu milioni ishirini wanasikiliza wakati unachoongea ni pumba,mfano John Mashaka sio mtalaam wa Finance amekuwa aki pose kama mtalaam wa Finance na kuhojiwa na BBC wakati hana anachokijua.IFM yuko bingwa wa Finance DR.Suleiman.

unaweza kuwa unafanya kazi WALL STREET lakini unapokea simu au uko mapokezi.kuna watu wanafanya kazi mahakama kuu lakini ni ushers wa mahakama.likija suala likija suala la kitalaam la mahakamani hawezi kulitolea maamuzi.
Waswahili wanasema tusipoziba ufa tutajenga ukuta.
 


Zilikuwa zinaitwa POLYTECHNICS au maarufu vyuo vya Margaret Thatcher alichokifanya ni sawa na shule za kata.vyuo kama Westminster,Southbank,middlesex nk lakini Westminster wame improve sana.

mjadala huu kwa wenye kuutizama vizuri ni kati ya mijadala bora JF imepata kuwa nayo.mimi nina mtu alimaliza Phd akaja kuambiwa chuo alichosoma ni feki. wako wengi wameibiwa ndio maana nina uchungu kuona watu wanaibiwa.
Nzoka hayu mabegi mbona kama machinga complex ya Karume? ina maana ukisoma business LSC unapewa practical training ya kuuza mabegi hapo shopping centre?Mzonya una lolote juu ya hilo?umekuwa kama msemaji wa LSC.

by the way kuna mtu kaniPM kuwa Yebo yebo nae ni Doctor wa PhD wenye data tupeni au naye amekuwa associate professor?
 

Hatuwezi tukaukataa ukweli kuwa MBA ni ina uwigo mpana, na kama huna background ya Management kwenye managerial position MBA ni added advantage.

Ni ukweli usiopingika kuwa hivi karibuni hata madaktari wameanza kuifukuzia MBA kwa ajili ya kujiimarisha kwenye magerial position.

Ni kweli MPH imelenga kuwapa health practioners uwezo wa kumudu managerial positions ila haina UWIGO mpana kama MBA.

Wahasibu wengi pia wamekuwa wakifukuzia MBA sababu kuu ni hiyo.

Niliwahoji wahindi flani wako hapa London wanasoma MBA, japo wanazo Masters mbalimbali nikawauliza kwanini wanakuja kusoma Masters ya pili ya MBA? Majibu wote niliowahoji walisema kuwa Kwao ukiwa na MBA unakuwa na value kubwa na wanakuwa na uwezekano mkubwa wa kupata kazi nzuri.

TUNAWEZA TUKAAMUA KUJIPA KAZI YA KUPITIA MATANGAZO YA KAZI YOTE FOR TWO WEEKS IN TANZANIA, nauhakika utakuja na jibu kuwa MBA imekuwa ikihitajika zaidi nao hao wanachance kubwa ya kupata kazi zilizo kwenye managerial.

Mtu asije akadhani naitetea hiyo kwa sababu ninayo (wala Sijasoma MBA) LA HASHA, bali ina high demand in our labour market NA HUO NDIYO UKWELI.

Ni kweli mtu aliye kuwa anatafutwa by then pale Muhimbili mojawapo ya sifa mojawapo ilikuwepo hiyo ya Utawala pamoja na remarkable experience
 
Darasa kamili kwa OGAH.kama hajaelewa nitamuelimisha zaidi hapa ni kisima cha elimu.
 

Nimemjibu rejea post zangu hapo juu. Nimetoa majibu kwa kirefu pamoja na observation zangu juu uchambuzi wa Nzoka (jina lake gumu) Na ametoa pia PICHA YA JENGO LA STESHENI YA TRENI (UNDERGROUND) pamoja na hilo la Shopping Centre hatoa jengo hajaitoa hiyo Hannibal House. Haiyamkini kwa sababu wako jirani na majengo ya London mengine yameungana basi amefanya assumption kama wachumi.

REJEA POSTI YANGU NILIYOMJIBU AMBAYO NIMEWEKA MAONI YANGU JUU YA HOJA ZAKE.
Ni kweli nimekuwa kama PR wa LSC na nilikomenti kwenye moja ya post zangu ILA KIBAYA NI MTU KUTOA HOJA KWA GENERALIZATION.

Muda mfupi uliopita nimewapigia SIMU LSC watoe ufafanuzi ili watu wasiendelee kupotosha, wakiona ipo haja watatoa.
 
kanda2 said:
kuna watu wanafanya kazi mahakama kuu lakini ni ushers wa mahakama.likija suala likija suala la kitalaam la mahakamani hawezi kulitolea maamuzi.

..kuna watu wana vyeti feki na sasa hivi wana nafasi nyeti na very public. wanatoa maamuzi ya kitaalamu lakini hao huwaandami unawaandama hawa watoto wanao-chat kwenye michuzi blog.

..pia umedai Dr.Shayo hana hata certificate ya uchumi, wakati kuna wachangiaji wanaeleza kwamba ana 1st degree ya Uchumi na masters in development studies.
 

Suala la uamini na uadilifu halipo kwani DR.Shayo anagawa business cards aki pose kama Associate professor wa uchumi.Hawa vigogo waliopo huko juu kama KAMALA,NAGU,MATHAYO,MAHANGA,NCHIMBI,MREMA N.K kuna watu walijua wanadanganya wakanyamaza.ndio sisi tusilale na SHAYO tumwambie mapema ili kizazi kijacho kisitulaumu.

MNOZYA.
inabidi wakulipe LSC jee hapa wajiunga kama LSC au watuma statment kwako halafu utaipaste hapa?

ni vyema waje kuweka wazi shutuma hizi kuliko kunyamaza kama Shayo ambaye alitakiwa aje kujibu ukweli wa elimu yake.

swali ina maana chuo kimo ndani ya shopping centre? ukimaliza kusoma unapewa practical training ya kuzaa mabegi hapo chuoni?mimi niliambiwa eneo la Southbank lina wajamaica wengi na si wasomaji mnozya unaweza kunipa jibu?maana tusitegemee sana habari za mitandao wewe uliopo kwenye ground unaweza kutupa habari nzuri zaidi.

Nakushuru Mnozya umekuwa ukijitahidi kutuelimisha,wewe ni asset kwetu na LSC.niliona tangazo gazeti la mwananchi kama sikosei kuwa Marketing officer wao ni ALLY ABDALLAH unamjua? kama unamjua aje kujibu hoja hapa asikuache wewe peke yako wakati yeye analipwa na LSC.

Pinda ilkuwaje akapeleka watoto hapo kwenye shopping centre?yeye anajiita mzalendo angewapeleka Tumaini university au Muslim university of Morogoro kuliko kuwapa tabu watoto kwenye chuo hicho.lakini sawa kama walishindwa kujua kuwa RICHMOND haina ofisi marekani watajua habari ya chuo?
 

Waziri Nchimbi au Nagu si watalaam,maamuzi yao kuna washauri waliobobea kwenye fani ndio wanawashauri na kuwaelekeza.wao ni wanasiasa sio watendaji Phd zao feki hazina athari kubwa kuliko DR.Shayo anavyofanya.

Nchimbi kasomea wapi ulinzi au silaha za jeshi?anawashauri ndio wanamuongoza. unataka niwaandame vipi? ktk michango yangu sijawahi kuandika kuwa DR.Kamala AU DR.Nchimbi always nawaita kwa majina yao.lakini tizama posts zangu zote ninamuita DR.SHAYO au mtaalam wa mazingira.nampa heshima yake ya UDOKTA.Tizama posts zote toka mwanzo.

kuna wachangiajia kama yebo yebo wanaeleza DR.Shayo ni associate professor wa uchumi,jee tumwamini wa First digrii ya uchumi au associate professor wa uchumi? au mimi niliyesema hana certificate ya uchumi?

unajua mimi nilinunua gazeti mtaa wa samora linaandikwa na ubalozi wa Tanzania Uk nikaona makala za DR.shayo kama kadhaa na baadae kwenye michuzi blog niliamini ni bingwa wa uchumi hadi mwezi uliopita alipokuja Tanzania na kufanya interview na michuzi,

ndio jamaa yangu akanipa ukweli kuwa DR.Shayo si bingwa uchumi ilinichukua muda kukubali jamaa akanipa vielelezo vyote.lakini Nchimbi hawezi kupose kama mtalaam wa mambo ya jeshi na kuanza kuandika makala za kijeshi.
 


Ally namjua sana Kamaliza hapo MBA in International Marketing of UWIC, na kwa sasa anamalizia disertation yake ya Msc in Consultancy Management ya UWIC. Pia ni Marketing Officer wa LSC na LST.

Nimeshawaambia wafafanue wenyewe. Nadhani nitamshawishi Ally ajiunge hapa Jamvini.

LSC haimo ndani ya shopping centre, kama ni hivyo na hiyo basi na stesheni ya underground trains nayo imo ndani ya shoping Centre maana jengo lake limeungana kama mnavyoiona picha iliyowekwa.. LSC wapo karibu sana na hiyo shopping center. NYUMBA ZA HUKU ZIMEUNGANA (SI ZOTE).

Nimesema awali hapo Elephant & Castle ni eneo kubwa na lina EXIT nyingi maana lina subways (underground), pana vyuo mbali mbali na bus stop nyingi. Pia pana ofisi nyingi. Kikanda hapo ni kati kati ya zone 1 na zone 2.

Kwa habari ya wajamaica sina hakika na nimesikia hapa JF ila nijuavyo ni eneo aghali.

Labda ikawa kweli, ila ni mpakani mwa Zone 1 na zone 2. NI mjini kabisa.

Mengine wasubirini wenyewe ila chuo hicho kinaviwanga na kina mtambo maalumu wa kumonitor mahudhurio, umeanza kutumika April 2009 na ni chuo pekee kwa UK chenye huo mtambo mpaka dakika hii. Hiyo ni indicator ya ubora.

Ila ukisema hakina viwanja vya kuchea mipira hapo sawa, Pia hapa London mtu unamiliki jengo kama umemaliza kulipa morgaji NA SI ARDHI. Naomba nisiibue mjadala mwingine TUBAKI KWENYE HOJA YA MSINGI
 
kanda2,

..hivyo vielelezo ulivyopewa na jamaa yako vinaonyesha Dr.Shayo ana 1st degree gani na toka chuo kipi? what about his masters and PhD?
 

Mkuu:

Are you Shayo in disguise? Anyway, Shayo ana haki ya kujiita atakavyo. Kujiita ni uchaguzi halali wa mtu. Vilevile Phd. zingine ni Inter-discipline. Anaweza kuwa ana Phd. ya Mazingira lakini ni nani aliyesema kuwa hiyo sio ya Uchumi?

Mtu anaweza kusomea Mazingira lakini concentration yake ikawa ni uchumi. Huwezi kupinga taaluma ya mtu kwa kuangalia tu Title ya digrii. Inabidi uangalie concentration ya kile anachofanya.

Kwa mfano kuna mGhana alichukua digrii ya uchumi huko Penn State. Lakini research yake ilikuwa kwenye impact ya ujenzi wa Lake Volta.

Hapa Phd. imechukuliwa kama kubobea taaluma fulani. Lakini hiyo ni sehemu moja tu. Sehemu nyingine na ambayo imesahaulika ni kuwa mtu mwenye Phd. anategemewa kuwa independent thinker, mwenye kuweza kujifundisha na kufanya research mbalimbali independently.
 


Zakumi,

..mimi siyo Shayo.

..naona kanda2 anataka kuwa cyber-bully ndiyo maana nimeamua kufunga kambi hapa.

..anajua kabla hajatoa madai yake alipaswa kutueleza huyo Shayo amehitimu katika fani gani kwa shahada zote tatu alizonazo.

..kila ukimuuliza hatoi jibu la uhakika kama kweli anamjua Shayo kiasi cha kuweza kumtolea lawama za kiwango hiki.

..maelezo yako ni kuhusu hizi credentials ni mazuri sana. binafsi nimemuuliza kanda2 kwamba inasemekana Shayo ana masters ya development studies, sasa masters hiyo ilitolewa na dept ya economics au sociollogy?

..pia hivi mtu hana ruhusa ya kuchangia mjadala wowote ule hata kutokana na uzoefu wake? kwa mfano mtaalamu mwenye masters ya foundation eng, hana ruhusu ya kuchangia ktk mjadala wa stuctrural eng hata kama huko ndiko alikospend muda mwingi wa kazi. je, huyo utamwita mtaalamu/bingwa wa foundation eng, au structural engineering?

NB:

..nadhani Mnozya na Nzoka wana point za maana sana kuliko haya mambo trivial aliyoleta kanda2.





 
Watetezi wa LSC,
Na wewe unayekataa Times Guide.



Chukua brochure ya LSC yenye picha ya kijengo chenu (main campus, kilichobanwa katikati ya majengo fulani. Ukipita lazima upite garden ya Pub (ambayo wanafunzi hamruhusiwi kukaa unless mnanunua vinywaji). Halafu unaona wamejitahidi kukata meza za Pub, ila zinaonekana tu), kati kuna picha ya msichana na mvulana wamevaa majoho, kulia kuna picha ya katikati ya piccadily circus (ili muwaingize watu mkenge). Brochure ina rangi nyeupe kwa juu, na nyekundu/damu ya mzee kwa chini.

Sasa basi, kwa maneno yao wenyewe, katika ukurasa wa 5. Wanaongelea UWIC. Imesifiwa na 'The Times Good University Guide 2004' kwamba ni the best 'NEW UNIVERSITY' in the UK.

Wameandika pia hapa; Ranking New University

Please, notice 'TIMES...' ambayo ndio tumekuwa tunatoa links hapa.
Notice the year is 2004 (ina maana, brochure yenu ya 2009, bado mnang'ang'ania 'glory' days za 2004).
Notice 'New University', ambazo ndo former 'polytechnics' hizo (shelf life haifiki 20 years), ina maana hata kuchanganya na University zilizobobea hawawezi. Hao hao Times unaowaponda, list yao nimekuwekea hapa, EMPLOYERS wako LSC, wanawakubali, na katika overall ranking ya Business related studies kong'oli tena hapa;

BUSINESS MANAGEMENT STUDIES RANKING

Kwenye overall ranking ilikuwa 65 mwaka jana, imeshuka hadi 77.

OVERALL RANKING

Mwisho kabisa, kwenye hiyo page 5, inasema;

'LSC is an Associate College of the UWIC and offers students from all around the world the opportunity to study programmes of this internationally renowned University'

Hawana library. Mna floor 4, mbili ziko katika matengenezo. Main campus haina Library, eti library iko elephant & castle (sijui duka la WH Smith ndo Library?)

Kitu kingine, huwezi ku-join shule, lazima upitie kwa huyo agent wao ili atengeneze commission.

Madarasa yenu yamebanana, inachukua watu si chini ya 100. Compyuta lab ni ya kubanana nayo. Nina wasiwasi na Fire safety ya jengo lenu lililo karibu na Pub.

Kuhusu kufanya kazi, shule zote zile, hauzuiwi kufanya kazi zaidi ya masaa ishirini kwa wiki. usijifanye hapo wanasoma sana kuliko hata University. Dude I have done my homework.

Brochure ninazo hapa, nimeuliza maswali, nimeshatembelea, napajua.

Kuna mshikaji aliinginzwa mkenge, siku anakuja nilifikiri anaenda LSE. Nikasema Yes, kaamua kusoma. Kuja kungundua yuko LSC. Nikamwambia ndugu tafuta shule ya maana. Kijana kasoma City, degree inaeleweka popote dunia hii. Sasa aliwezaje ku-afford City wakati alikuwa ameenda LSC? Sometimes sio kwamba watu hawana hela, its jus mis-information!!

Now decipher all of that, mimi nina mambo muhimu ya kufanya. Nadhani nimewasaidia waTanzania vya kutosha. Endelea kupotosha, nina info zaidi, ila nazikalia for now.
 

Mheshimiwa nakutimia moyo kwa kuwasaidia Watanzania. Naomba nikusahihishe kwa kifupi na kwa ujumla ili usichelewe kufanya hayo mambo muhimu.

1. Unapoingia haupiti katika hiyo PUB nadhani hujawahi enda ila umefanya assumption tu. Pub ipo kwenye square area. Nakushauri uendee ili ulete taarifa zilizo sahihi. NA KAMA UMESHAFIKAPO KWA NINI UNADANGANYA? Kwamba ili uingie LSC ni mpaka upite kwenye hiyo PUB (Kwenye hivyo viti? Au tafsiri ya kupita inajumuisha na kuona?

2. Kuwepo kwa PUB si hoja, always penye haya learning ni vitu vya kawaida. Nenda mlimani utaona pia nenda Mzumbe ipo inayo milikiwa na student association.

3. Sidhani kama ni ustaarabu uende eneo la biashara mfano Mgahawa au Pub kisha ufike na kukaa na kuanza kupiga soga tu. Huo si ustaarabu katika ulimwengu ulio staarabika.

4. Nilisema tukisema hawana viwanja vya kuchezea mipira hapo sawa. kwamba imebanwa na majengo nadhani si hoja kwa central London na pia wamepakana na Kings College. Pia nilihighlight kwenye mojawapo ya post niliyokujibu.

5. Kama kuna mtu alifikiri LSC ni LSE huyo ni mzembe maana majina ni tofauti kabisa hata na program pamoja na Location. Pale karibu na Aldgate kuna chuo kinaitwa London School of Commerce & IT, hivi itakuwa sahihi kudhani hicho ni LSC? Huo ni uzembe.

6. Pia wengi qualification zao amma wakimisi experience ina wabidi wasome foundation 4 month ili waendelee na kozi yao. Wengi wanalalamikia hicho ila wao LSC wanasema hivyo ndio viwango vyao.

7. Sijaongelea kuhusu masaa, nilichosema ni muda wa kufanya kazi kufuatana na ratiba zao. Rejea post zangu vizuri. NA UKATAE USIKATAE UKWELI UNABAKI KUWA STUDENTS WENGI (wakiwamo WTZ) wanapenda wafanye kazi sana kuliko kusoma NA wengi wakuwa wakijikuta wanafanya supplementary amma kurudia mwaka. Wengi walikuwa wanapenda ku extend viza NA NDIO MAANA KUANZIA MARCH 31, YAMEONGEZWA MASHART MAGUMU ILI URUHUSIWE KU EXTEND VISA.

8. Kuhusu kubanana kwenye kumbi za mihadhara hilo nimelisema ni kama bongo hususani UDSM, MU na SUA kidogo. Rejea post zangu, hapo tunaweza tukasema.

9. NASISITIZA KWA HERUFI KUBWA KUWA MIMI SI MWANAFUNZI WA HAPO NA WALA SINA INTEREST IWAYO YOTE ILA TUACHE GENERALIZATION NA TOO MUCH OF ASSUMPTIONS.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…