Ni dhahiri kwamba kutatokea mabadiliko kwenye uwiano wa nguvu za vyama hivi kwenye visiwa hivi viwili. Kama walivyosema baadhi ya wachambuzi hapo juu, wapo Wapemba wengi ambao si wana-CUF, lakini walikuwa wakikiunga mkono chama hicho kutokana na kujihisi hawatendewi haki; kura zao hazitabiriki. Vivyo hivyo, sio wakazi wote wa Unguja ni wafuasi wa CCM; kura zao zinaweza kuangukia popote.
Sitashangaa sana iwapo hata uwiano wa viti vya ubunge na uwakilishi kati ya CCM na CUF ukawa tofauti sana safari hii.
Kama wakiendelea kuwa makini, naamini kete waliyoicheza CCM safari hii itasaidia kupunguza mivutano isiyokuwa na maana. Kitendo cha Waasisi wa mapinduzi kutangaza wazi kumuunga mkono Shain kabla hata ya uchaguzi, nacho kinaongeza chachu kwenye mwelekeo mpya wa Zanzibar.
Kila la heri Zanzibar