Ndugu Jafar,
Nilishiriki ktk Awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere, wakati huo tukiwa na Five Year Plans. Mbona hizi ahadi za J.K. zinaonekana kana kwamba hakuna mpangilio wowote? Chini ya serikali ya CCM hakuna Mpango unaohakikisha mapato ya Taifa, pamoja na mikopo ambayo tunaweza kupata, yatatumika vipi? Did Five Year Plans lapse with the death of Nyerere?
J.K. akiwa Kanda ya Ziwa aliahidi Vivuko, Meli na barabara za lami, akiwa Kigoma aliahidi Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa. Juzi ameahidi Bagamoyo kiwanja cha ndege kingine cha kimataifa pamoja na Bandari ya kisasa. Matumizi ya viwanja hivi wakati Air Tanzania iko mahtuti, hayaeleweki.
Hospitali za Rufaa zimeahidiwa huko Ruvuma na sijui wapi tena. Sasa Dar es Salaam inaahidiwa Machinga complexes tano na Fly-overs ktk kila manispaa. Hivi vyote viko ktk Five Year Plan au ni vya jukwaani tu?
Katika 5Year Plans za siku hizo zetu, tulikuwa tuna-forecast pia upatikanaji wa wataalam wa kikwetu kuendesha miraji tuliyojiwekea. Tulitazama nchi nzima, sio kwa mahitaji ya fedha za maendeleo tu, bali pia kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya Serikali na taasisi zake. Hizi ahadi za J.K. endapo atashinda zikitekelezwa, si lazima sehemu nyingine zisubiri? Tusimchague huyu? Amechanganyikiwa!!!!!!!!!
Makwaiya wa Kuhenga ktk kipindi chake katika Runinga anauliza "Je Tutafika?"