nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,860
- 5,801
Wednesday, April 20, 2011
Na Mustapha Kapalata, Nzega
KATIBU MKUU wa chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)Dkt,Willibrod Slaa amemsimamisha kazi katibu wa wilaya ya Nzega wa chama hicho Sunny Yohana katika kikao kilichofanyika jana katika ukumbi wa chanel one uliopo wilayani hapa.
Dkt,Willibrod Slaa ambaye yupo mkoani Tabora akiendelea na Ziara yake ya kikazi ya Chama hicho akianzia Tabora mjini,Bukene,Nzega na leo akiwa hutubia wananchi wa wilaya ya Igunga na kuendelea na wilaya zilizo salia Mkoani hapa.
Dkt,Willibrod amefikia maamuzi hayo ya kumsimamisha kazi katibu huyo wa wilaya baada ya kupokea malalamiko mengi yautendaji kazi wake katika kikao hicho cha wanachama wa chama hicho ambacho kilikuwa kama hukumu ya katibu huyo kufuatia uongozi wake katika Ngazi ya wilaya.
Mambo ambayo yalichangia kuenguliwa kwa muda katika kiti hicho nipamoja na kutokuwa na ushirikiano na umoja wa vijana na baadhi ya wanachama ambao walikuwa wakimshutumu kwa kuwa na ubinafisi.
Wanachama hao walisema mbele ya Katibu Mkuu wa Chama hicho Dkt,Willibrod kuwa katibu huyo amekuwa akiukataza umoja wa vijana kufanya mikutano ya ndani na hata ile ya nje jambo ambalo lilimshangaza Katibu huyo Mkuu wa chama hicho.
Wakiendelea kubainisha wanachama hao juu ya utawala wa Sunny Yohana walisema alisubutu hata kusimamisha michango ambayo ilikuwa akitolewa na wanachama hao ilikupata mfuko wa chama hicho,hata hivyo chama hicho kwa sasa hakina hata akaunti ya kutunzia fedha.
Pamoja na hayo jambo ambalo liliochangia kwa kiasi kikubwa kumsimamisha katibu huyo nipale aliwasilisha hati ya bajeti ambayo ilighalimu maandalizi ya ujio wa msafara wa Katibu Mkuu wa chama hicho.
Akikabidhi hati hiyo yenyezaidi ya Tsh, laki 4 kwa mkurugezi wa msafara huo ndipo alipo anza kuuwasirisha kwa wanachama hao na kuonekana kunaubadhirifu mkubwa wa fedha hali ambayo ilimfanya Dkt,Willibrod kutoa tamko hilo la kumsimamisha kazi kwa muda usiofahamika mpaka pale tume ya taifa itakapo kuja kufanya uchunguzi zaidi juu ya tuhuma hizo.
Kwa upande Sunny alisema ameyapokea vizuri maamuzi hayo ya Katibu Mkuu kuwa ilichama kiendelee mambo kama hayo hutokea kuajibishana katika chama,akiendelea kusema kuwa bado yumwana chama na anamapenzi na chama hicho.
Alisema kwa Tamko hilo ingawa hakupewa hata muda kidogo wa kujitetea juu ya tuhuma hizo na kuuangushia mzigo kwa umoja wa vijana kumuundia njama za kumtengua cheo hicho.
Dkt,Willibrodi alimteua Peter Piusi kuwa katibu kaim wilaya wa Chama hicho mpaka pale tume maalumu itakapo fanya uchunguzi.
Katibu kaim wa chama hicho alisema ameipokea vizuri nafasi hiyo na ameahidio kutoa ushirikiano mkubwa kwa wanachama,hata hivyo aliuomba ushirikiano wa kutosha kwa wadau hao ilikuweza kukiweka sawa chama hicho ambacho kilionekana kukosa muelekeo katika medani ya kisiasa wilayani hapa.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa Chama hicho Omary Shaabani Omary alisema kusimamishwa kwa katibu hiyo nimoja ya pengo kwa chama hicho kulingana na utendaji kazi wake,
Amemtaka kaim Katibu wilaya kujitolea kwa nyakati zote ilikurudisha imani kwa wanachama pamoja na wananchi akiongezea alisema kuwa kuachana na makundi ambayo yanachangia kwa kiasi kikubwa kukigawa chama hicho.
Katibu Mkuu akitoa maagizo kwa wana Chama wake ni pamoja na kuachana na mambo ya kukigawa chama kwa njia ya udini ama ukabila hali ambayo inaweza kuhatarisha amani hapa nchini.
Alisema kwa kashifa hiyo ambayo ilikuwa imeenezwa na baadhi ya vyama vya siasa hapa nchini na sumu hiyo kuenea kote nchini ni vema ikatoweka mara moja na wananchi wakaendelea na mapenzi na vyama vyao kama jinsi ilivyo kuwa hapo awari.
Akiendelea kutoa maagizo hayo alisema kanda ya Mkoa wa Tabora nimoja ya kanda zilizo pangwa kuzishugulikia na kukieneza chama hicho hasa katika ngazi ya vijiji na ngazi ya kata huko ndipo kwenye mapungufu.
Alliwataka wana Chama hao kutoa ushirikiano kwa viongozi wa liowachagua na kuwa kitu kimoja ilikujenga chama bora na kuwa na imani kwa wananchi ambao wanatazama kujiunga na chama hicho.