Bhbm
JF-Expert Member
- Oct 31, 2009
- 714
- 210
Katika nchi zenye democrasia changa kama Tanzania na nchi nyingine nyingi za Africa, maamuzi kama hayo ni muhimu sana kufanyika kwa haraka kama kuna ushahidi wa kutosha wa tuhuma na wenye kuridhisha. Ni vizuri sana kuwa na uwazi kwa mambo yanayohusu uwajibikaji kwa wananchi au wanachama pia. Mkimsoma vizuri Dr. Slaa kwa maelezo yake yuko sahihi kwa nafasi aliyonayo kufikia maamuzi kama hayo ili kuepusha hali ya mashaka na sintohamau kwa uma. Huyo katibu hajavuliwa madaraka bali amesimamishwa kwa muda ili uchunguzi ufanyike na haki itendeke, na kama akionekana hana hatia basi chama kitamsafisha kwa njia hiyohiyo iliyotumika kumsimamisha.
Tukumbuke pia kuwa uimara wa serikali ya ccm chini ya Mwalimu Nyerere mambo kama hayo alikuwa akiyafanya sana yeye pamoja na Hayati Sokoine, na hiyo ilisaidia sana kuleta nidhamu ya utendaji na kuepusha ubadhilifu wa mali na madaraka pia. Maamuzi kama hayo pia yanasaidia sana kuchuja wale mamluki walioingia katika chama ili kutumiwa kukiua chama kujiondoa wenyewe kama siyo kuogopa kabisa kujiingiza katika chama.
Nashauri sana chama kizingatie umuhimu wa kuendesha semina za mara kwa mara kwa viongozi wa kazi zote kuanzia mashina juu ya uwajibikaji na uadilifu katika uongozi ili kuzidi kukiimarisha chama na kukijengea uaminifu kwa wananchi.