Dr. Slaa Apata Pigo!



Sikutarajia JF senior expert member kufanya analysis ya kiwango duni kama hii!! Aibu tupu.

Yote yanayozungumzwa nchi hii kuhusu mitaala, mishahara na mazingira duni ya kazi ya walimu, kudharauliwa, kushitakiwa, walimu kubakwa, kupigwa na mengine mengi ambayo yameshusha ari na motisha wa walimu kufanya kazi; bado JF senior expert member huelewi kitu!? lawama ni kwa dr. Slaa?!!

Hiyo shule inabeba jina lake kama heshima, je shule yenyewe ni mali yake? je shule hiyo inafundisha mitaala ya Dr. Slaa? yeye ndie mwenye dhamana ya kuwalipa walimu?

Husaidiki wewe kalagabaho!!
 
Serikali hii ya ccm iruhusu shule ya serikali iitwe Dr W. Slaa?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
kuna mahusiano yapi kati ya mshahara wa dr slaa na hiyo shule kufelisha?? tatizo la mitaala hulioni unakodolea mimacho slary slip za wengine, wivu wa kiiiiik.......................eeeeee
 
Angalia na hii na uwe objective katika ku comment kwako.

Yaani shule yenye jina la Rais Kikwete waliofeli ni 110, lakini wewe unaona waliofeli 22 Shule yenye jina Dr. Slaa ndio issue.


kwa motokeo haya ya fastjet ni slaa 3.2 ili amfikie fast jet kwa ufaulu huu wanaoita wizara ya elimu
 
Swala la ubora wa elimu ni swala la kitaifa na si la kibnasfi, kwahiyo ni juu ya serikali kuwezesha kiwango cha elimu kiwe cha kukidhi, tukianza kuangali majina kwenye mashule ni upuuzi na ufinyu wa fikra, swala la elimu katika nchi hii ni kubwa kuiliko unavyo dhani...Kipindi cha nyuma wakati Sumaye akiwa waziri mkuu alikuja barozi kutoka nchi ya nje akamwambia elimu ni ya Tanzania ni mbovu, Zero akaanza kubisha kama juha....nayaona...Elimu pia na mazingira ya shule, unadhifu wa walimu na mambo mangi tu
 
Watu bwana, tunajua unawaza zile hela ambazo huwa mnaongelea za dr milion 7, hivi hi shule ingafaulisha watoto gata wote hii aibu ingetutoka kweli,
 
Nakupongeza kwa majibu mazuri ya kumjibu huyu mwazilishi wa mada hii hongera


Angalia na hii na uwe objective katika ku comment kwako.

Yaani shule yenye jina la Rais Kikwete waliofeli ni 110, lakini wewe unaona waliofeli 22 Shule yenye jina Dr. Slaa ndio issue.

 

Hii shule iliyopo Basodawish, Karatu nadhani ni mtihani wao kwanza na kutokana na mazingira naona ni bora ukilinganisha na zile shule kongwe.
 

Wewe ni mropokaji. Kwa Dr Slaa ndo MTAALA wa Elimu (Usokuwepo)?
 
Ni nini maana ya kuwa mlezi?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Shule kutumia jina la mtu haimaanishi mtu huyo kuwa mlezi wake.........Sidhani kama Robert Mugabe anajuwa kuwa kuna shule inaitwa Mugabe pale Sinza
 
Mmmhhh kumbe hivi!!
Kwa hio hata mtoto wako ukiamua kumuita dr. slaa basi dr atakuwa anawajibika kumlea mtoto yule ili aendane na taswira yake...............basi kama hivyo kuna vyuo vinaitwa oxford, harvard nao wanapaswa kulea hizo shule au wanale??

na kuna baadhi ya barabara pia zina majina ya viongozi wakubwa mfano barabara ya sam nujoma kumbe sam nujoma anapaswa kuilea ile barabara eehhh................i didn't know that!!

Thank you for this!!
 
Hizi Shule cha muhimu ni kuwa na walimu wazuri na siku hizi sababu ya Serikali kupuuza Elimu hatutaweza kuwa na walimu wazuri na wanafunzi wazuri hadi hapo mikakati mizuri itakapokuwekwa vizuri na elimu ipewe kipaumbele kusaidia kwa pesa na posho hakuwezi kumfana mwalimu awe na akili nzuri wakati na yeye hana kitu kicwani cha kufundisha wanafunzi

la muhumu ni kuwasomesha kwanza walimu wapikike kisawa sawa ndipo wafundishe wanafunzi bila hivyo blah blah hazitaisha
 
Angalia na hii na uwe objective katika ku comment kwako.

Yaani shule yenye jina la Rais Kikwete waliofeli ni 110, lakini wewe unaona waliofeli 22 Shule yenye jina Dr. Slaa ndio issue.


Huu ndio ujinga wenyewe. Yaani unafananisha uozo wa fulani kuwa ndio kigezo cha fulani kuoza! Ipo siku utasema, mbona Zimbabwe fedha zao hazina thamani na nchi Yao masikini kwa hivyo na kwetu ndio maana pako hivi. Ujinga huo.
 
Hakuna haja shule za sec.za kata kuitwa majina ya watu mashuhuru kwani nikuwadhalilisha.
 
Huu ndio ujinga wenyewe. Yaani unafananisha uozo wa fulani kuwa ndio kigezo cha fulani kuoza! Ipo siku utasema, mbona Zimbabwe fedha zao hazina thamani na nchi Yao masikini kwa hivyo na kwetu ndio maana pako hivi. Ujinga huo.
1. Kuheshimiana ndio jambo kubwa kabisa ninalolithamini, na sioni kama usingeweza kujenga hoja yako bila kutumia maneno uliyotumia.

2. Nashangaa umeona huo ujinga wangu usione ujinga wa mleta uzi. Je Slaa ni mmiliki wa hiyo shule? Je Slaa ni mfadhili wa hiyo shule? Kama shule kuwa na jina la kiongozi ni lazima ifanye vizuri kwa nini usitumie kipimo hicho hicho kwa shule zenye jina la Kikwete?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…