Dr. Slaa: Daftari la wapiga kura liboreshwe kabla ya kura ya maoni!

Dr. Slaa: Daftari la wapiga kura liboreshwe kabla ya kura ya maoni!

Mkuu hili ni jukumu la serikali kupitia hela za walipakodi, ni wajibu wa wabunge wetu kushinikiza hilo lifanyike na sio ombi!
 
UDASA waanzishe Mdahalo kuhusu Daftari la wapiga kura

Wadau waitwe yaani vyama vya siasa, msajili wa vyama, NEC, JWTZ, Polisi, TAMISEMI, Wanaharakati
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, amesema chama chake hakitakubali kura za maoni za Katiba mpya kufanyika bila ya kuboreshwa daftari la Wapiga kura.

Alitoa kauli hiyo wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mwendakulima wilayani Kaliua mkoani Tabora.

“Chadema haitakuwa tayari kuingia katika kura za maoni za katiba mpya bila daftari la wapiga kura kuboreshwa kwa kisingizio cha gharama na ukubwa wa nchi,” alisema.

Dk. Slaa alisema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) haipaswi kuogopa gharama za kufanya maboresho hayo kwani demokrasia yenyewe ndiyo gharama na suala hilo ni sheria siyo hisani.

Alisema Daftari la Wapiga kura linapaswa kufanyiwa marekebisho mara mbili katika kipindi cha kumalizika uchaguzi mkuu na kuingia uchaguzi mkuu mwingine kama sheria inavyoelezwa.

Dk. Slaa alisema anafahamu kinachoendelea katika suala la uboreshaji wa daftari la wapiga kura na kwamba kauli za tume kudai haina fedha za kufanya maboresho hayo siyo za kweli bali zinatokana na kuwapo kwa mvutano wa baina ya serikali pamoja na tume.

“Serikali inajua Daftari hili likiandikwa upya vijana wengi wataandikishwa na kupata fursa ya kupiga kura hivyo CCM itashindwa katika uchaguzi mkuu ujao,” alisema.

Alitoa mfano kuwa katika chaguzi mbalimbali mfano ule wa Arumeru Mashariki jumla ya vijana 14,000 walishindwa kupiga kura kutokana na kutokuandikishwa katika daftari la wapiga kura.

Dk. Slaa amemaliza ziara yake katika mikoa ya Shinyanga, Kigoma na sasa anaendelea katika mkoa wa Tabora kabla ya kuingia mkoa wa Singida.

CHANZO: NIPASHE
 
Hili ni wazo jema sana lakini inasikitisha sana pale ambapo hoja ya namna hii inapingwa na CCM kwa manufaa yao binafsi ya kifisadi.
You are absolutely right! Tena subiri uone baadala ya kuongelea hoja hii iliyoko mbele yetu, Team ya Mwigulu wataingia hapa kwa kuweka hoja kando na kuanza kum-attack Dr Slaa personally. Very sad!!!!
 
Hii iwe mijawapo ya agenda za mikutano ya Dr. Slaa n m4c. Bila kusukumwa magamba hayavuliki.
 
Heri kura za maoni zichelewe ili daftari la wapiga kura liboreshwe! Tunakimbilia wapi
 
Kuboreshwa kwa daftari la wapiga kura ni muhimu sana na hatutakubali huu ubakaji wa demokrasia.Mimi mwenyewe nilijiandikisha Ngara na kwa sasa nipo jijini Mwanza hivyo sikubaliani na huu upuuzi wa mizigo kupoka haki yangu ya kikatiba.
 
Hii iwe mijawapo ya agenda za mikutano ya Dr. Slaa n m4c. Bila kusukumwa magamba hayavuliki.

Upo sahihi mkuu, DR.SLAA aifanye agenda kuu huko anakopita ili kuwaandaa wananchi kuidai na kuipigania haki yao hii ya kikatiba yaani kupiga kura kuchagua viongozi wao wanaowataka.
 
Wazo zuri kabisa, wahusika wachukuwe hatua tafadhali. hii ndiyo matokeo ya kuwa na tume ya uchaguzi isyohuru.
 
mzee comed
mzee wamatamko amehamisha mada ya maoni ya katiba kwenda kwenye dafari la wapiga kura.
Kwani ameambiwa daftari la wapiga kura halita boreshwa?
Huyu mzee anaweweseka kama juha
kila kukicha anazidi kushuka kiwango
atakuwa alilishwa limbwa.ta na yule mash.....mbu....zi.
 
Tanzania ni nchi inayosifika kwa Amani, Lakin inaminya Demokrasi, vijana waliofikisha umri wa kupiga kura ni zaidi ya Milion 12.5
Uwoga wa CCM ni kuwa Vijana watataka Mabafiliko na Mabadiliko hayo yako Chadema Pekee.
 
mzee comed
mzee wamatamko amehamisha mada ya maoni ya katiba kwenda kwenye dafari la wapiga kura.
Kwani ameambiwa daftari la wapiga kura halita boreshwa?
Huyu mzee anaweweseka kama juha
kila kukicha anazidi kushuka kiwango
atakuwa alilishwa limbwa.ta na yule mash.....mbu....zi.
Hapo kwenye red, iwapo huna data ni vema ukakaa kimya, uache wanaume wajadili hoja kuliko kuropoka!!!! Kwa kukusaidia tu hebu soma habari hii hapa chini:


Hofu imeanza kutanda kwa baadhi ya Watanzania kuhusiana na ushiriki wao katika zoezi la kupiga kura ya maoni kwa ajili ya mabadiliko ya katiba mpya.

Maelezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) ambayo ndiyo itakayosimamia zoezi hilo ndiyo yanayoelekea kuwachanganya baadhi ya Watanzania. Kwamba, kamwe haitaweza kuboresha daftari la wapiga kura kwa wakati na hivyo, litakalotumika ni daftari lililotumika wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.

Maelezo zaidi ya Nec, kupitia taarifa iliyomkariri mwenyekiti wao jana, yalifafanua zaidi kuwa tume hiyo hivi sasa haina fedha kwani kumekuwa na urasimu mkubwa kuzipata.
Na kama hiyo haitoshi, Nec imedai kuwa Tanzania ni nchi kubwa na hivyo, kamwe haitawezekana kuboresha daftari la uchaguzi ili litumike katika upigaji wa kura za maoni kwa ajili ya katiba mpya.

Sisi tunaona kuwa miongoni mwa majibu yaliyotolewa na Nec ni mepesi. Hayalingani na suala lenyewe ambalo ni muhimu sana kwa hatma ya nchi.

Kwa kukumbushia, ni kwamba kitendo cha kutaka kutumia daftari lisiloboreshwa la uchaguzi kinamaanisha kuwa siyo Watanzania wote wenye sifa watakaokuwa na nafasi ya kutekeleza wajibu wao wa kupiga kura ili kupitisha au kuzuia ujio wa katiba mpya.

Na hili liko wazi. Kama hakutakuwa na utaratibu mwingine ambao hadi sasa haujawekwa wazi, basi Watanzania waliokuwa na umri chini ya miaka 18 wakati daftari hilo likiboreshwa miaka mitatu iliyopita hawataweza kutimiza wajibu wao huo wakati wa kura za maoni.

Kwa mfano, yule aliyekuwa na miaka 17, kamwe hatakuwa na fursa ya wazi ya kupiga kura ingawa mapema mwakani wakati zoezi hilo likitekelezwa tayari atakuwa na miaka 21.

Ni wazi kwamba kuna Watanzania wengine wameshapoteza sifa ya kupiga kura kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo ya kufariki dunia.

Kwa kuzingatia yote hayo, sisi tunaona kuwa baadhi ya sababu zilizotolewa na mwenyekiti wa Nec katika kuhalalisha matumizi ya daftari la wapiga kura la mwaka 2010 hayana mashiko hata kidogo.

Ni mepesi mno na kamwe hayalingani na uzito wa suala lenyewe ambalo kimsingi, litawagusa Watanzania kwa miaka mingi ijayo. Katiba ya nchi si jambo dogo hata kidogo.

Kwa mfano, maelezo kuwa nchi hii ni kubwa na hivyo tume hiyo haiwezi kuboresha daftari lake katika kipindi kilichobaki kabla ya kupigwa kwa kura ya maoni mapema mwakabni hayaonekani kuwa na mashiko.
Ni kwa sababu katika dunia ya sasa; dunia ambayo watu huunganishwa pamoja kupitia teknolojia ya mawasiliano, haitarajiwi hata kidogo kusikia kwamba kuna jambo muhimu kitaifa linashindwa kufanyika kwa ufanisi wa asilimia mia moja kwa sababu tu ya ukubwa wa nchi.

Katika dunia hii ya digitali, kazi nyingi zilizoonekana kuwa ngumu sana hapo kabla zimerahisishwa mno.

Tunadhani kwamba hata uchukuaji na uhifadhi wa taarifa muhimu za wapiga kura siyo jambo gumu, hasa kwa tume ambayo inachohitaji kufanya ni kuboresha tu taarifa na kuwaongeza Watanzania waliofikisha umri wa miaka 18 baada ya kukosa sifa ya kuandikishwa miaka mitatu iliyopita.

Siku hizi, alama za vidole huchukuliwa kielektroniki, picha huchukuliwa kielektroniki na hata taarifa huchukuliwa kwa njia hiyo. Kila kitu ni digitali. Hakuna ugumu kama zamani.

Nec, ambayo kimsingi hutegemea zaidi taarifa mbalimbali za wapiga kura katika kuendesha shughuli zake, inapaswa kuwa mstari wa mbele katika kuchangamkia fursa ya ukuaji wa teknolojia.
Haipaswi kujitetea kwa maelezo kuwa nchi ni kubwa sana kwani kadri inavyoonekana sasa, kutakuwa na kipindi cha walau miezi mitatu mbele kabla ya zoezi la kupiga kura ya maoni.

Tume hii ya uchaguzi ilipaswa kuwa kinara wa kuchangamkia fursa za ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano. Ilipaswa kuiweka Tanzania nzima kwenye kiganja. Haipaswi hata kidogo kufanya mambo yake kwa mtindo wa zimamoto.

Nec haipaswi kueleza kirahisi kuwa wanashindwa kuboresha daftari lao kwa vile muda uliobaki ni mfupi. Na kama ukweli ni huo, basi walitarajiwa kueleza hilo kwa kina ili wapewe muda wa kutekeleza jukumu hilo kwa ufanisi.

Nec haipaswi kusuasua katika zoezi hilio la kuboresha daftari ambalo mwisho wa siku litawasaidia pia wakati wa kufanyika kwa uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015.

Tume hiyo pia ilipaswa kueleza kwa kina juu ya hatua zilizochukuliwa kutafuta fedha za kuboresha daftari badala ya kutoa maelezo ya jumla tu, kwamba kuna urasimu.

Nec itaje bila kificho ni nani anawakwamisha kupata fedha za kuboresha daftari hilo kwani kupitia taarifa kama hiyo, ndipo Watanzania watamjua anayekwaza dhamira nzuri ya kuwa na katiba mpya iliyopigiwa kura na Watanzania wote wenye sifa.

Ni vyema Nec ikawa na utaratibu wa kujiandaa kwa majibu yanayojitosheleza kutokana na masuala muhimu kama hili la kura za maoni kwa ajili ya katiba mpya.



SOURCE: NIPASHE
 
Kama kuna jambo ambalo CDM wanatakiwa watie shinikizo hata ikiwezekana kwa maandamano makubwa ni hili hapa....tuachane na akina zito tushinikize mambo makubwa kitaifa
 
Mkuu hiyo ya kutoboresha daftari ni janja ya CCM baada y kugundua kuwa vijana wengi wako kinyume nao ,kwa hiyo ili kupumua kwa muda ndo maana hawataki kuboresha daftari hilo. Fedha zipo kibaao,tangu lini serikali ikakosa fedha kwenye masuala yanayifeva?
 
Mnajua mnapokuwa mnataja kuboresha daftari la wapiga kura kila wakati mtafanya choo cha Mwigulu kijae baada ya muda mfupi? Maana kila anaposikia watu wanataka maboresho lazima jamaa liende kuharisha! Linajua siku zake na Ugaidi lililofanya lazima likapate mume Segerea na kutatuliwa marinda.
 
Fedha zipo, kwani Tume ya katiba ya Warioba imetumia mabilioni na cha kushangaza bado kwenye path hiyo hiyo ya kupata katiba mpya kimefikia kipengele cha kura ya maoni fedha zimekuwa hamna, ni jambo la kushangaza.

Anyway, waswahili wanasema njia ya mwongo fupi, Naunga mkona hoja wapenda demokrasia na mageuzi Tanzania tupige harambee tupate fedha ya kuboresha daftari tunaomba tusizuiliwe, tunataka kila mtu vijana kwa wazee washiriki tendo hili muhimu kwenye maisha yao. WANAHARAKATI PLEASE SUPPORT THIS VERY IMPORTANT ISSUE.
 
Back
Top Bottom