Mi naumia sana jamani,hivi kweli Kikwete anaweza kutufanyia watanzania tuliomwamini kwa kura nyingi vile kipindi cha kwanza haya?maombi yote tunayomwombea shukrani ndo hiyo kweli?Mungu atajibu kabla hajaondoka hapa duniani.Tunaomba tu evidence Dr Slaa.MOYO WA MTU HAUSOMWI KWA TABASAMU!duh,bora nisingejua hili!
Dr Slaa at work..Kuna watu walilisikitika sana tulipompendekeza Dr Slaa kuwa mgombea Urais,walisema atakosa forum ya kuiwajibisha serikali,wakasahau kwamba yeye ni Katibu Mkuu wa chama na ni Public Figure,Tumaini la Watanzania..Huyo sasa yuko kazini.Hakuna cha hoja binafsi kupelekwa kwa spika wala kwa Katibu wa Bunge,maana inaweza ikakataliwa vile vile na hata Bungeni kwenyewe wakati wa kuchangia hoja unaweza ukakarishwa chini na spika vile vile.Lakini forum ya sasa ya Dr Slaa haina kauzibe,ni kuita waanidhi wa habari full stop,ni kuitisha mkutano wa hadhara,full stop hakuna longolongo.This is the forum nzuri and i believe Dr atatumia vizuri sana..Nadhani hii salamu ya Mwaka Mpya kwa Rais Kikwete
Hongera my President and am proud of you!!
safi sana dk slaa tulikuwa tuunaumia sana kukuona uko kimya kikwete lazima awajibike na sijui ni kwa nini ajazungumzia dowans
Jamani si mmeona kama dr angeapishwa kuwa rais ina maana angeanza na kikwete kwanza.
Upupu mtupu, unaongelea kodi? Unajuwa kuwa kwa miaka yote kabla ya Kikwete kodi inayokusanywa haikuchangia hata hamsini kwa mia ya bajeti yetu? Tumeona wakati wa Kikwete hali hiyo ikipanda hadi kufikia kuwa sasa tunachangia asilimia sitini ya bajeti yetu kama si zaidi. Tena kupunguka, bajeti imepanda maradufu! Au hilo hulioni?
Huyu Silaa anatafuta kuanzisha choko-choko za uvunjifu wa amani, kila analosema linaashiria kuwa si mwana-siasa bali ni limbukeni na sasa kapata sehemu ya malimbukeni wenzake nao wanamsikiliza bila kuhoji wala kupima. Akumbuke, hatuta ona amani ya Tanzania inavunjika kwa mtazamo wake hasi. Kama ana ushahidi wa hayo si apeleke bungeni na kama hana ushahidi na anaongea pumba ajuwe ndio mwanzo wa mwisho wa fitina zake. Atashughulikiwa kisheria.
Walisha kuwepo watu wa kanisa wenye choko choko kama yeye, mfano ni Mtikila, huyu kwisha nyamazishwa. Sasa huyu hayaoni hayo, na yeye inapaswa sasa anyamazishwe kama mtikila. Na hivyo ndivyo itavokuwa maana kushindwa kwake kura sasa analeta chokochoko.