Dr. Slaa: Kikwete mmiliki wa DOWANS...


Majibu marahisi kama kawaida yetu...
 
- Nje ya mada mkuu, na sina muda wa kupoteza!, halafu ni heshima tu kwa Dr. Slaa ndio maana sikuichambua post nzima., otherwise rudi kwenye mada kama unaweza tuelimishane!

William.

Mbona sisi wenye akili zetu timamu, ambao hatujawa brain washed tunakuona kabisa unamuda wa kupoteza sana tena kwa kuandika upupu mtu hapa.
 
Mbona sisi wenye akili zetu timamu, ambao hatujawa brain washed tunakuona kabisa unamuda wa kupoteza sana tena kwa kuandika upupu mtu hapa.

- Upupu ni kuamini kwamba katiba ya jamhuri inatakiwa kurekebishwa kwa matakwa ya Dr. Slaa na Chadema, huo ndio hasa upupu kwa sababu wabunge wengi ni wa CCM, meaning wanakilisha mawazo ya wananchi wengi na ndio wenye upperhand ya uamuzi wa mwisho kwa kila kinachopita bungeni, kufikiri tofauti ndio upupu wenyewe unaousema mkuu!

- Halafu tutakuja kusikia kilio cha kuchakachua on the ishu ambayo toka sasa iko wazi kwamba it wont happen!

William.
 

Labda siuelewi mjadala, au mgongano wa mawazo. Are we talking about due process? Kwamba hata Kikwete mwenyewe hawaamini wabunge wake ndio maana anaunda CRC? Really?

Kama tunaamua kuunda katiba, na tuunde katiba. Mi sio mtaalam wa mambo ya Bunge, ila napenda kuamini muda huo kinachozungumziwa ni katiba ipi wananchi wanaihitaji, na wabunge wanakaa kama kamati maalum kufanikisha mchakato huo.

William, sipendi kuamini una tatizo na Dr Slaa/Chadema, ila ni jambo jema kutambua jinsi vuguvugu la katiba lilivyoendelezwa na Chadema kwa siku za karibuni.
 
Heko Mkuu Wacha1, you struck the nail right on the head ! Dili Uingereza zilianza kutiwa mchanga na hivyo kuhamishiwa USA. Mama Maajar kaingia kwa kishindo na juzi tu katembelea California na kufikia kwa jamaa !

Mh, mmenikumbusha jambo hapa. Ktk liquidations (ktk kusimamia utekeleza wake) kwa yale mashirika mengi ya Serikani yaliyotakiwa eidha kubinafsishwa, kuuzwa au kuwekwa ubia, taasisi ya kisheria iliyopewa kazi yote ilikuwa IMMA & MAAJAR Law associates. Mnaweza kufuatilia ktk Liquidations nyingi za serikali, mtapata majibu ya jambo nalosema hapa.

Jibu linakuja ni,..IMMA Laws Assoc. ya Lau Masha ambapo yupo Riz1 kama galikipa na upande wa MAAJAR Laws Assoc. ya balozi Maajar, yupo mama mwenyewe anahakiki kuwa fungu litokalo serikalini, linazunguka vyema 'kuingia mfuko wa pili wa baba wa golikipa' wa IMMA.
Hivyo hapa tunagundua jambo moja kuwa hii ni 'timu moja' inatenda kazi kamili waliyopanga.
 

Kuna principle inasema hivi inakuwa vigumu sana kumuelewesha mjinga wa kwanza katika vigezo vya ujinga kuliko yule wa mwisho, na opposite is true kwa mwerevu(mwenye akili). Kwa akili na ufahamu wako mawazo ya katiba mpya ni ya Slaa tu na wananchi walio wachache?
 
chezo kwishnei!!!...sasa yule aliyempa power of attorney``fisadi Mkubwa wa Tanzania ameshaanikwa hadharani kama ana maelezo ya kina yanayoweza kututhibitishia Watanzania kwamba yeye si mmiliki wa kampuni ya kifisadi ya richmond (Dowans) ayaweke hadharani na kutwambia ni nani mmiliki wa kampuni hiyo. Na isitoke hata senti tano toka TANESCO au Hazina ili kuwalipa mafisadi hawa.
 

Kikwete asiunde Kamati ya katiba! Kazi ya kuunda tume ya katiba iwe ya Bunge na sio ya Kikwete. Suala la mabadiliko ya katiba haliko katika ilani ya uchaguzi ya CCM. Hivi basi Kikwete ajiondoe katika kuteua tume. Nina wasiwasi hiyo tume haitakuwa tofauti na tume ya uchaguzi ambayo ni ya CCM. Wateule wa rais watawajibika kwa rais, lakini wateule wa bunge watawajibika bungeni, bunge ambalo ni la wananchi wenyewe.

Watanzania kuweni macho, ndio kwanza uchakachuaji mwingine wa katiba unaanza. Kikwete asiingilie mchakato wa katiba kwa masilahi binafsi ya kulindana. Hiyo tume itaundwa na akina nani? Kinana, Makamba na Lowasa? Kikwete acha bunge la wananchi liwe huru kuendesha mchakato wa katiba mpya. Acha bunge liwe na uhuru kamili wa kuteua watu wa kada mbalimbali Hivi kweli kama JK angeunda tume ya kuchunguza Richmond, Ukweli ungepatikana? Kama Suala dogo tu la mgombea binafsi JK amecheza na mahakama. Akina EL wala wasingejiuzulu.
KULINDANA MTINDO MMOJA. KATIBA NI WANANCHI SIYO YA RAISI.
 
Wajameni asanteni sana kwa michango yenu kwenye hoja hii, mimi binafsi sijawahi kumkubali JK kama mtu serious kwenye kazi yake, hana uwezo wala ujasiri, ujasiri alionao ni wa kuchakua kura zetu tu. muda wake sasa unakwisha, miaka mitano siyo mingi jamani, wa kwanza ndio huo kufumba na kufumbua utakuwa umekatika, mimi nasubiri kuona zile meli alizokuwa anaa ahidi kila alipoona kidimbwi cha maji atazileta kweli. Jamani tufike mahala tuthamini utu wetu na Tanzania iheshimike, hivi jamani bado tuko wajinga kama zamani wazungu walipochukua rasilimali zetu na kutuachia shanga?
 
na sasa hivi mafisadi wapo hivi wansubiri 185bil kumeza dawa rushia moto wameze
 
Ukubali tu kuwa umezidiwa point? usibaki kungangania CCM majority.
 
 

Kikwete hachomoki hapa, hili analo! limepiga usoni moja kwa moja! puu puu tumpepee!
 
I honour you doctor! Thanks for telling the truth, if he is a clean man let him come out and defend him self.
 

- Mkuu sina tatizo na anybody ila ninajadili taifa langu kwa kuthamini realities na mazingara tuliyonayo kisiasa, hatuwezi kuunda katiba mpya ambayo haikubaliki na wananchi wote na hatuwezi kuunda katiba mpya kwa kuwasikiliza wananchi wachache, kama ni due process then CCM wanatakiwa na the upperhand kwa sababu ni wengi kwa uwakilishi bungeni,

- Unless tunataka kuunda katiba mpya nje ya katiba yetu ya sasa ya Jamhuri na kama hivyo ndivyo, ina maana tutafanya mabadiliko mengi sana kila kona ya taifa letu bila kupitia katiba yaani bungeni, eti mkuu unasema hilo linawezekana Tanzania ya leo?


William.
 

Kaka William!
Naomba tusitoane macho bure wakati tunatafuta kitu chenye manufaa kwetu sote na vizazi vinavyokuja. Swala la katiba umiliki wake unatokana na wananchi wakiwemo wenye vyama kama wewe na wasio navyo kama mimi.
Mchakato wa uundwaji (sio marekebisho) wa katiba unapaswa kujumuisha makundi yote na ndipo unapounda Bunge la katiba si kwamba unageuza lile linaloexist bali unaunda chombo chenye uwakilishi wa makundi haya (dini, wafanyakazi, siasa, wanazuoni, watoto, vijana, NGOs n.k).
Utaona kwamba makundi haya hayapo Bungeni, kule kuna wana siasa tu.

Kaka hatuhitaji katiba yenye mawazo ya CDM/Slaa, tunataka yenye mawazo yetu wananchi. Nyerere (CCM no. 1) aliwahi kusema katiba yetu inaweza kumfanya kiongozi kuwa dikteta hata bila yeye kutaka.
Kwa hali ilivyo sasa hata CCM (Mkapa, Chiligati, Sitta, Warioba etc) wameongelea need ya katiba mpya kwa hiyo sio swala la wingi wa wabunge wa CCM tena.
AG wa Zanzibar juzi kasema tunaka katiba mpya itakayoaddress maswala ya muungano wetu. Ni ukweli usiopingika kwamba katiba ya sasa ina kigugumizi juu ya mambo mengi sana.

Concern ya watu wengi, kwa uzoefu, juu ya bunge letu lenye idadi kubwa ya wanaCCM ni kwamba wakifika kule wanatanguliza maslahi ya chama kwanza na si ya Taifa. Kaka chaguzi zetu hazijakuwa huru sana kuweza kusema hawa wote ni wawakilishi wa wananchi maana mizengwe mingi sana. Sisemi wabunge wote wa CCM wameshinda kwa mizengwe, la hasha. Lakini pia hata pale mwanaCCM ana mawazo tofauti na wenzake hawezi kusema maana kuna hofu ya kufukuzwa kwenye chama.

Kama utakumbuka kabla ya mwaka 1992 maoni ya watanzania yalikusanywa 80% hawakutaka tuingie kwenye siasa ya vyama vingi. Uwezekano ni kwamba tume iliyoundwa iliwafikia zaidi watu wenye mtazamo fulani tu. Kama si nguvu ya Nyerere hicho unachoita demokrasia (wengi wape) basi tusinge ruhusu siasa ya ushindani.

Mimi ningeomba tusitukuze sana vyama CDM, CCM, CUF n.k lakini tukubali kwamba kwenye hivi vyama na makundi mengine kuna watu wanazungumza lugha ya wananchi na wengine lugha ya watawala. Katiba ni ya wananchi si ya watawala, tuache wananchi wazungumze!!

Naomba kuweka pause kaka!!!!!!!!! Alamsiki
 
 

- Very interesting!

William.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…