- Wananchi wamewaongeza wabunge wengi Upinzani, lakini bado wakachagua majority wabunge wa CCM, ni FACT it has nothing to do na anything na ni wabunge wa CCM ambao ni majority bungeni, ndio wenye kauli ya mwisho kuhusu ishu zote muhimu za taifa na ndio Demokrasia yenyewe.
William.
Kaka William!
Naomba tusitoane macho bure wakati tunatafuta kitu chenye manufaa kwetu sote na vizazi vinavyokuja. Swala la katiba umiliki wake unatokana na wananchi wakiwemo wenye vyama kama wewe na wasio navyo kama mimi.
Mchakato wa uundwaji (sio marekebisho) wa katiba unapaswa kujumuisha makundi yote na ndipo unapounda Bunge la katiba si kwamba unageuza lile linaloexist bali unaunda chombo chenye uwakilishi wa makundi haya (dini, wafanyakazi, siasa, wanazuoni, watoto, vijana, NGOs n.k).
Utaona kwamba makundi haya hayapo Bungeni, kule kuna wana siasa tu.
Kaka hatuhitaji katiba yenye mawazo ya CDM/Slaa, tunataka yenye mawazo yetu wananchi. Nyerere (CCM no. 1) aliwahi kusema katiba yetu inaweza kumfanya kiongozi kuwa dikteta hata bila yeye kutaka.
Kwa hali ilivyo sasa hata CCM (Mkapa, Chiligati, Sitta, Warioba etc) wameongelea need ya katiba mpya kwa hiyo sio swala la wingi wa wabunge wa CCM tena.
AG wa Zanzibar juzi kasema tunaka katiba mpya itakayoaddress maswala ya muungano wetu. Ni ukweli usiopingika kwamba katiba ya sasa ina kigugumizi juu ya mambo mengi sana.
Concern ya watu wengi, kwa uzoefu, juu ya bunge letu lenye idadi kubwa ya wanaCCM ni kwamba wakifika kule wanatanguliza maslahi ya chama kwanza na si ya Taifa. Kaka chaguzi zetu hazijakuwa huru sana kuweza kusema hawa wote ni wawakilishi wa wananchi maana mizengwe mingi sana. Sisemi wabunge wote wa CCM wameshinda kwa mizengwe, la hasha. Lakini pia hata pale mwanaCCM ana mawazo tofauti na wenzake hawezi kusema maana kuna hofu ya kufukuzwa kwenye chama.
Kama utakumbuka kabla ya mwaka 1992 maoni ya watanzania yalikusanywa 80% hawakutaka tuingie kwenye siasa ya vyama vingi. Uwezekano ni kwamba tume iliyoundwa iliwafikia zaidi watu wenye mtazamo fulani tu. Kama si nguvu ya Nyerere hicho unachoita demokrasia (wengi wape) basi tusinge ruhusu siasa ya ushindani.
Mimi ningeomba tusitukuze sana vyama CDM, CCM, CUF n.k lakini tukubali kwamba kwenye hivi vyama na makundi mengine kuna watu wanazungumza lugha ya wananchi na wengine lugha ya watawala. Katiba ni ya wananchi si ya watawala, tuache wananchi wazungumze!!
Naomba kuweka pause kaka!!!!!!!!! Alamsiki