Dr. Slaa: Kikwete mmiliki wa DOWANS...

Dr. Slaa: Kikwete mmiliki wa DOWANS...

Dowans yawajibu LHRC


na Happiness Katabazi, Maswa


amka2.gif
KAMPUNI ya Dowans Holding SA na Dowans Tanzania Ltd, zimeiomba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam itupilie mbali mapingamizi waliyowekewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na wengine, kwa madai kuwa hawana haki ya kisheria kupinga tuzo waliyopewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) isajiliwe na mahakama hiyo.
Mbali na LHRC, wengine walioweka mapingamizi ya kutaka Mahakama Kuu ya Tanzania isisajili tuzo hiyo ni mwandishi wa habari mwandamizi, Timothy Kahoho, Lawyers Environment Action Team na Sikika Company.
Ombi hilo la kutaka mapingamizi hayo yatupiliwe mbali liliwasilishwa hivi karibuni mahakamani hapo na wakili wa Kampuni ya Dowans, Kennedy Fungamtama, kwa madai kuwa LHRC na wengine wanaopinga tuzo hiyo hawana haki kwa sababu hawakuingia nao mkataba wa kufua na kuzalisha umeme.
Nakala ya mapingamizi hayo ya Dowans ambayo Tanzania Daima inayo, inaeleza kuwa wenye haki ya kupinga tuzo hiyo ni TANESCO ambao waliingia nao mkataba na si watu, ama taasisi nyingine.
Nakala hiyo ya Dowans imechambua kuwa; Kahoho hana haki wala masilahi yoyote ya kisheria yanayompa nguvu ya kisheria ya kupinga tuzo, kwa sababu mkataba uliingiwa na pande mbili ambazo ni Dowans na TANESCO na kuongeza kuwa hata TANESCO ilipovunja mkataba huo ni Dowans ndiyo ilikwenda ICC kuifungulia kesi TANESCO na hatimaye Oktoba 15 mwaka jana, mahakama hiyo ilitoa hukumu ambapo Dowans ndiyo ilishinda kesi hiyo.
Wakili huyo wa Dowans, Fungamtama anadai kuwa hata katika mkataba walioingia Dowans na TANESCO , Kahoho hawakuwa sehemu ya mkataba huo (Power Off –Take Agreement (POA) ambapo kwa mujibu wa mkataba huo, pande hizo mbili zilikubaliana kuwa endapo itatokea tofauti miongoni mwao, mgogoro wao utatatuliwa na Mahakama ya ICC.
Alisema pande zote zilikubaliana kwamba mkataba huo ni mzuri na kwa mazingira hayo, Mahakama ya Tanzania haitakuwa na mamlaka ya kuona mkataba huo ni batili, hivyo wapingaji hao hawana mamlaka ya kuupinga.
Kuhusu hoja ya Kahoho kwamba Dowans isilipwe, Fungamtama alidai kuwa si ya msingi na haina mantiki kisheria, kwani tayari Mahakama ya ICC ilishatoa hukumu yake na ikaiamuru TANESCO kuilipa fidia Dowans, ikiwa ni hasara waliyoipata baada ya TANESCO kuvunja mkataba kinyume cha makubaliano.
Aidha, kuhusu mapingamizi ya LHRC, Lawyers Environment Team na Sikika Company Ltd, dhidi ya Dowans, kwanza Fungamtama alihoji uwezo wao kisheria, uwakilishi wao kwa watu wasiofahamika kama walivyodai kuwa wanawawakilisha wananchi na kuongeza kuwa hawana sababu ya kisheria ya kusema kuwa wao ni wawakilishi wa wananchi wanaopinga tuzo hiyo isisajiliwe na kulipwa.
Wakili Fungamtama alidai kuwa walalamikaji hao walikosea kutaja kiwango cha tuzo aliyoshinda mteja wake. Tuzo aliyoshinda mteja wake ni dola za Marekani 65,812,630.33 na si dola 123,223,270.98 kama walivyoainisha kwenye hati yao ya madai na kuongeza kuwa si kwamba mkataba ulioingiwa na TANESCO na Dowans hauwabani .
Baada ya mahakama kupokea mapingamizi hayo ya Dowans, iliitaka TANESCO ijibu pingamizi lililowekwa dhidi yake na Dowans Mei 27, mwaka huu.
Kadhalika LHRC na Kahoho nao wajibu mapingamizi waliyowekewa na Dowans Mei 20 mwaka huu, na kwamba majibu yote hayo yajibiwe kwa njia ya maandishi na akaiahirisha kesi hiyo hadi Julai 28 mwaka huu, ambapo kesi hiyo itakuja kwa ajili ya kutajwa.
Januari 25 mwaka huu, Dowans iliwasilisha ombi lake la kutaka Mahakama Kuu ya Tanzania iisajili tuzo waliyopewa na Mahakama ya ICC na siku chache baadaye TANESCO, LHRC na Kahoho wakawasilisha hati ya nia ya kupinga ombi hilo la kutaka tuzo hiyo isajiliwe.
Mahakama ya ICC, ilitoa hukumu ya kesi ya Dowans dhidi ya TANESCO, Novemba 15 mwaka jana, ambapo mahakama iliitia hatiani TANESCO kwa kosa la kuvunja mkataba na Dowans na ikaiamuru iilipe fidia ya shilingi bilioni 94, hukumu ambayo imezua mjadala mkali hapa nchini kuanzia kwa viongozi wa serikali, vyama vya siasa na makundi mengine, ambapo wengine wanataka Dowans ilipwe huku wengine wakitaka kampuni hiyo isilipwe.
 
haya mambo ni kwamba kuna mijitu mitanzania inashabikia CCM

Kwa taifa makini lenye watu makini huyu so called ........... angesha uwawa muda sana mana sijui hata kazi yake ni nini?
ki uhakika tunahitaji mabadiliko na mabadiliko ya kweli yani kung'oa hawa watu na kama ingewezekana wafie gerezani na kama mimi ningekuwa ndo kiongozi yani ningewawajibisha kwa vitanzi.
 
Hii ndiyo ile ambayo kamati ya Dr. Mwakyembe alisema mengine hawakuyatoa hadharani kwa sababu za kiusalama ( wa Taifa)!!!! Hivi usalama wa Taifa ni usalama wa Kikwete au wa wananchi? Ni usalama gani wa taifa wakati mkulu mwenyewe ndiye anayetusaliti?

Wakuu huyu Jk na serikali yake kila nnavyozama ktk fikra pana zaidi kuhusu ishu za dowans, IPTL, Ugumu wa maisha, ripoti ya CAG, na kero nyingine nyingi hitimisho langu ni kuwa yale yanayowakuta akina Gabgo'.. Yanakaribia Tz tena kwa kishindo kikuu na dunia itashangaa..
 
Serikali ilishinikiza uteuzi wa Richmond - Shahidi

Imeandikwa na Na Regina Kumba; Tarehe: 11th April 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 27; Jumla ya maoni: 0








SHAHIDI wa kwanza wa Serikali katika kesi ya kughushi na kutoa taarifa za uongo serikalini
inayomkabili mfanyabiashara Naeem Adam Gile, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, jinsi Serikali ilivyoing'ang'ania Kampuni ya kufua umeme ya Richmond.

Akitoa ushahidi jana, shahidi huyo Nicolous Suke (55) aliyekuwa Katibu wa Bodi ya zabuni ya Shirika la Umeme (Tanesco), alidai alipokuwa akijibu maswali ya wakili wa mshitakiwa Alex Mgongolwa kuwa Bodi hiyo ilipewa siku 10 na Serikali kukamilisha mchakato wa kumpata mzabuni, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Alidai kuwa Wizara ya Nishati na Madini ndiyo iliyotoa agizo hilo, na kwamba kama wataalamu waliona sheria inavunjwa na kulikuwa na malumbano kati ya Tanesco na Serikali
kama zitumike siku 10 zilizoamuliwa na wizara au ifuatwe sheria inavyosema ambayo inatamka ni siku 45.

Alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Waliarwande Lema, baada ya kuona sheria haifuatwi waliwasiliana na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) nao walishauri itumike
njia nyingine ya siku 14, Bodi ya Tanesco iliijulisha Serikali, lakini ilisisitiza agizo lao la siku 10 lifuatwe na hivyo mchakato kuendelea.

Hata hivyo, shahidi huyo alidai baada ya zabuni kutangazwa na kampuni nane kushiriki ikiwamo Richmond, kamati iliyoongozwa na mtu aliyemtaja kuwa Boniface Njombe
wakisaidiana na wataalam wawili kutoka nchini Ujerumani, waliweka wazi kuwa hakuna mshindi wa zabuni hiyo aliyepatikana.

Suke alidai Bodi ya Zabuni ya Tanesco ilipelekewa taarifa ya matokeo ya kamati hiyo, kwa sababu Serikali ilikuwa katika matatizo ya umeme, alidai Bodi ya Tanesco kupitia Menejimenti
iliagiza kamati ya uchunguzi kuangalia kama kati ya kampuni hizo nane kuna yenye unafuu na kubainika tena hakuna inayofaa.

Baada ya hapo, shahidi alidai Bodi iliijulisha Serikali kuwa zabuni hiyo haina mshindi, nayo ikaelekeza ipelekewe nyaraka za kampuni zilizoshiriki zabuni. IIibidi Bodi ya Zabuni ya Tanesco ifute zabuni ile na kupeleka nyaraka serikalini. Alidai Serikali iliunda kamati yake maalumu na kuendelea na mchakato.
 
Richmond did not meet tender requirements- Witness

By JULIUS BWAHAMA, 11th April 2011 @ 12:00, Total Comments: 0, Hits: 143

A PROSECUTION witness testified before the Kisutu Resident Magistrate's Court on Monday that Richmond Development Company LLC did not meet the requirements for the tender floated by TANESCO to produce 100 Megawatts (MW) of electricity in the forgery case against Naeem Giire.

Mr Giire, who was the first person to be arraigned in court in connection with the Richmond scandal that led to the resignation of former Prime Minister Edward Lowassa, is charged with five counts of forgery and uttering forged documents to the Tanzania Electric Supply Company Limited (Tanesco) tender board, regarding the capability of the company to produce 100MW of electricity.

Mr Nicholas Suke (55), the prosecution witness and who was also TANESCO's Procurement Manager and the Tender Board Secretary in 2006 told the court that there were eight companies bidded for the TANESCO's tender, but all of them failed to meet the requirements set by the tender board.

Apart from Richmond, other companies include Gapco, Adreko, Apgum, Quantus and Recmo.
"In 2006 as the tender board secretary for Tanesco, I made a tender notice number TC/10/TC 006 of providing generators to produce 100MW of electricity which was advertised in different local newspapers.

"After taking the notice to TANESCO's tender board, it was approved and adverts made on February 2006. But out of all eight companies that submitted their bids, none managed to meet the requirements after evaluation by the special evaluation team," explained Suke.

According to Mr Suke, the evaluation team was chaired by Mr Boniface Njombe and was assisted by two consultants from Lamahya Company from Germany.

Mr Suke said that the reason why TANESCO made the tender offer was simply because of the urgent need for the country to generate more electric power following prolonged droughts at the Ruvu and Mtera dams.

He also said the companies were given 10 days to submit their tender bids instead of the legal minimum required time of 45 days because the then Minister for Energy and Minerals, Dr Ibrahim Msabaha, had ordered so, a decision that was disputed by the Public Procurement Regulatory Authority (PPRA).

According to Mr Suke, after the bidder had submitted the tender bid at TANESCO's head office, he was registered or his company in the registration book, after the bidders' names and tender bid documents were read for the public.

"On March 20, 2006, in the registration book, Richmond Development Company LLC was represented by two individuals called Nolen Fiim and Nizar Paka. The power company had followed all the required procedures for registration but only failed to meet the requirements to get the tender," Mr Suke told the court.

He said that the tender documents submitted at TANESCO's office by Richmond included among others a proposal form for the tender, a power of attorney, brochures for the generators, a contract with PERRA Witney Power Systems, technical specifications for the generators.

It is alleged that the accused represented his brother, Mr Mohamed Gire, chairman of the Richmond Development Company LLC, at the opening of bids and subsequent evaluation and negotiation process.

The prosecution alleged that to justify the said representation, the accused forged a power of attorney deed dated March 13, 2006, purporting to show that it was signed by his brother and authorizing the accused to perform some duties on behalf of the company in Tanzania.

Resident Magistrate Mustafa Siyani adjourned the case to today when prosecution witnesses shall continue testifying.
 
Mhandisi Tanesco aieleza mahakama walivyoikataa Richmond

Imeandikwa na Na Regina Kumba; Tarehe: 12th April 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 43; Jumla ya maoni: 0








MHANDISI wa Shirika la Umeme (Tanesco), Simon Julima ameieleza mahakama kuwa chanzo cha kukataliwa kwa Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond (LLC) ni kushindwa kueleza mitambo yao ilipo.

Akitoa ushahidi mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Kisutu Dar es Salaam Jumanne, Walialwande Lema, shahidi huyo alidai kampuni hiyo mbali na kushindwa kueleza wapi ingetoa mitambo hiyo, pia haikuweka wazi nani angeruhusu mitambo hiyo kutumika.

Pamoja na kasoro hizo, Julima ambaye ni shahidi wa tatu katika kesi hiyo ya kughushi na kutoa taarifa za uongo serikalini, alidai hata baada ya kampuni hiyo kupewa mkataba, ilileta
mtambo tofauti na waliyoahidi kuileta.

Kwa mujibu wa madai ya mhandisi huyo, kampuni hiyo ilitakiwa kuleta mtambo wa Pratt Whittney, lakini wakaleta mtambo aina ya GE Electric na yeye alipewa taarifa ya mabadiliko hayo na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati huo, Dk. Ibrahim Msabaha.

Julima aliyedai aliteuliwa na Bodi ya Zabuni ya Tanesco katika kamati ya tathimini akiwa na wenzake 11, pia alidai alishiriki kuzikataa kampuni nane zilizoomba kupata zabuni hiyo baada
ya kuzitathimini.

Katika kesi hiyo ya kughushi inayomkabili mfanyabiashara Naeem Adam Gire, mhandisi huyo alidai hata baada ya kupewa maelekezo warudie kutathimini ili kupata kampuni yenye unafuu kwa sababu nchi ilikuwa katika matatizo ya umeme, kamati hiyo ilitoa matokeo kuwa hakuna kampuni kati ya hizo yenye vigezo.

Mbali na kuzikataa kampuni hizo ikiwemo ya Richmond kwa mara ya pili, Julima alidai pia walipendekeza serikalini zabuni hiyo itangazwe upya; hivyo hajui Richmond ilishindaje
zabuni hiyo, ila alipata uteuzi mwingine kuwa Mhandisi Mkuu kusimamia ufungaji mitambo ya kampuni hiyo.

Katika uteuzi huo, alidai alipewa mkataba uliosainiwa na Kampuni ya Richmond na Tanesco na kwa mujibu wa mkataba huo, kampuni ya Richmond alileta mitambo yake nje ya
muda waliokubaliana.

Akijibu swali la wakili wa mshitakiwa, Alex Mgongolwa, shahidi huyo alidai hakumbuki kama walijiridhisha ni muda gani ulitumika katika mchakato wa zabuni hiyo. Alimkumbusha kuwa shahidi aliyetoa ushahidi juzi, Nicolous Suke alidai walitumia siku 10 kwa shinikizo la
Serikali kinyume cha sheria inayotaka zitumike siku 45.

Mahakama imepanga kuendelea kusikiliza kesi hiyo Mei 9 na 10, mwaka huu.
 
Shahidi:Richmond haikukidhi matakwa ya kufua umeme Send to a friend Tuesday, 12 April 2011 20:34

Tausi Ally
KAMPUNI ya Richmond Development Company LLC ya Texas nchini Marekani haikukidhi matakwa ya zabuni ya kununua mashine ya kufulia umeme wa Megawati 100 baada ya kutokea kwa tatizo la ukame nchini na kusababisha kuwapo kwa upungufu wa umeme nchini.Alisema haikukidhi mahahitaji kwa sababu haikuonyesha mitambo ya kuzalisha umeme na pia wahusika hawakusema kwamba inapatikana wapi na nani angeileta nchini.

Mhandisi katika kitengo cha uzalishaji umeme cha Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Simon Jilima jana aliyaeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Waliarwande Lema wakati akitoa ushahidi wake dhidi ya kesi ya kughushi na kutoa taarifa za uongo kuhusu umeme wa Richmond, inayomkabili mfanyabiashara, Naeem Gire.

Jilima alidai kati ya kampuni nane zilizojitokeza kushiriki kwenye mchakato wa kutafuta mzabuni, hakuna kampuni hata moja iliyoshinda zabuni ikiwamo Kampuni ya Richmond kwa kuwa katika nyaraka zake haikuonyesha mitambo yao ingepatikana wapi na nani angeiruhusu kuileta nchini.Kwa mujibu wa sheria ili mzabuni aweze kuleta mitambo nchini ni lazima aonyeshe imepatikana wapi na nani atahiruhusu kuileta nchini.

Alisema kutokana na mapungufu hayo baada ya kutathimini walitayarisha ripoti kwenda bodi ya zabuni ya Tanesco kuileza kwamba hakuna kampuni yoyote kati ya nane, iliyojitokeza na kushinda zabuni hiyo.Shahidi huyo wa upande wa mashtaka alidai licha ya kupeleka taarifa hiyo, pia walipendekeza tenda hiyo itangazwe upya na bodi hiyo iliipokea na kukubali mapendekezo hayo.

Jilima alidai baada ya hapo hakujua tena kilichoendelea, lakini aliteuliwa kuwa Msimamizi Mhandisi wa Kufunga Mitambo iliyoletwa nchini na kampuni ya Richmond na kukabidhiwa mkataba wa kufunga mitambo hiyo.
"Baada ya kukabidhiwa mkataba huo, majukumu yangu yalikuwa ni kusimamia mitambo hiyo iliyoletwa na Richmond, lakini kwa kuchelewa kwa sababu katika mkataba ilipangiwa muda maalumu wa kuletwa na kufungwa,"alidai Jilima.
Alidai awali mtambo wa Richmond ilikuwa uletwe nchini na kampuni ya Pratt & Whitney, lakini kutokana na mazungumzo yaliyofanywa na Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Ibrahim Msabaha walitaarifiwa kuwa yametokea mabadiliko na kwamba utaletwa na kampuni ya G. E. Electric.Baada ya kumaliza kutoa ushahidi huo, Hakimu Lema aliiahirisha kesi hiyo hadi Mei 9 na 10 mwaka huu itakapoendelea tena kusikilizwa.

Kwa mujibu wa kesi hiyo, Gire anadaiwa kutoa taarifa ya uongo kwamba kampuni ya Richmond ina uwezo wa kuzalisha megawati 100 za umeme wakati akijua sio kweli.Kesi hiyo ilifunguliwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo Januari 13, 2009 na ikachukua zaidi ya mwaka mmoja na miezi mitatu upelelezi kukamilika.

Gire yuko nje kwa dhamana, kwa mara ya kwanza alipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka matano ambayo anadaiwa kuwa kati ya Machi 13, na Juni 2006 jijini Dar es Salaam, aligushi na kumruhusu Mohamed Gire Mwenyekiti wa Richmond Development Company LLC ya Texas nchini Marekani kufanya shughuli za kampuni hiyo nchini.

Pia anadaiwa kuwadanganya wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwamba kampuni ya Richmond ina uwezo wa kuzalisha megawati 100 za umeme nchini Tanzania ili kampuni hiyo, ipendekezwe na wajumbe hao.
 
Shahidi: Serikali iliibeba Richmond


na Happiness Katabazi


amka2.gif
MTAALAMU wa manunuzi wa Shirika la Umeme (TANESCO) Nicholaus Suke, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam kuwa kamati maalumu iliyoundwa na shirika hilo kuchambua washiriki walijitokeza katika zabuni ya kununua mashine ya kufua umeme wa megawati 100 ilibaini hakuna aliyekidhi vigezo vilivyowekwa ikiwemo Kampuni ya Richmond Development Company LLC.
Suke ambaye ni shahidi wa kwanza wa upande wa Jamhuri mbele ya Hakimu Mkazi, Waliarwande Lema, alitoa maelezo hayo jana wakati akiongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali Fredrick Manyanda kutoa ushahidi wake katika kesi ya kutoa taarifa za uongo kwa maofisa wa serikali kuhusu Kampuni ya Richmond inayomkabili Naeem Gire.Shahidi huyo alidai kuwa licha ya kamati hiyo kuchambua makampuni yale, ilibaini hapakuwa na kampuni yenye nafuu kwa vigezo.
Alidai kuwa mwaka 2005 alikuwa Ofisa na Katibu wa Bodi ya Zabuni na kwamba anaitambua kampuni hiyo ambayo mwaka 2006 ilikuwa ni miongoni mwa makampuni nane yaliyojitokeza kuomba zabuni hiyo iliyotangazwa na serikali baada ya taifa kukumbwa na tatizo la umeme.
Mbali na Richmond, aliyataja makampuni mengine yaliyoomba zabuni hiyo ya wazi na ya kimataifa kuwa ni Aggreco, Real Energy, Gapco, Apgum, Quatus, Recno.
Shahidi huyo alidai kuwa zabuni hiyo ilitangazwa kwa siku 10 kinyume cha sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2004 inayotaka iwe ya siku 45 na ilifanyika hivyo kutokana na maelekezo ya aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Ibrahim Msabaha. Alidai siku ya ufunguzi wa zabuni hiyo, kulikuwa na malumbano baina ya TANESCO na serikali na kudai kwamba Richmond ilifuata taratibu zote za kushiriki kwenye zabuni.
Shahidi huyo alieleza kuwa matokeo ya uchambuzi yaliweka wazi kwamba hakuna mshindi katika zabuni hiyo kwa kuwa hakuna kampuni iliyotimiza vigezo vilivyowekwa.
Yafutayo ni mahojiano baina ya shahidi huyo na wakili wa mshitakiwa, Alex Mgongolwa:
Wakili: Ulisema kulikuwa na malumbano kati ya TANESCO na serikali ni malumbano gani?
Shahidi: Yalikuwa ni ya aidha zabuni itangazwe ya siku 10 au ifiatwe sheria ya manunuzi inavyosema... malumbano hayo yalikuwa ni kuhakikisha sheria inafuatwa. Alidai TANESCO baada ya kuona sheria inavunjwa walitaarifu Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) ambayo ilishauri kufuatwa kwa njia nyingine ya kutangazwa kwa siku 14.
Hata hivyo baada ya kuitaarifu wizara, ilisisitiza agizo lao na siku 10 litekelezwe.Shahidi wa pili kwenye kesi hiyo alikuwa Wakili wa kujitegemea, Silvester Shayo, ambaye alidai Machi 13, 2006 alikuwa shuhuda wa waraka wa kuteua mwakilishi baina ya Kampuni ya Richmond na Gire ambaye aliteuliwa kuwa mwakilishi wa kampuni hiyo.
Alidai waraka huo aliletewa ofisini kwake na karani wa wakili mwenzake Emmanuel Kisusi na kwamba hakuutilia shaka kwa kuwa anamuamini wakili huyo. Hakimu Lema aliahirisha kesi hiyo hadi leo, ambapo shahidi wa tatu atapanda kizimbani kuanza kutoa ushahidi wake.
 
Tanzania ya watanzania inaamka na sasa watanzania watakuwa na tanzania yao na si tanzania ya viongozi wasiogusika na wajionao hawagusiki. dhamana ya watanzania iko kwao wao na si kwa viongozi wachache. kuifikia hali hii mapambano lazima yatokee na hatimaye wema huushinda ubaya na lilo nzuri kwa watanzania litadumu milele
 
Kamati ya Bunge kuhoji ufisadi Tanesco Send to a friend Wednesday, 27 April 2011 21:39

Exuper Kachenje
MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Januari Makamba amesema kamati yake italihoji Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco), kuhusu upotevu wa mabilioni ya fedha kama ilivyoonyeshwa katika taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi, Dar es Salaam jana, Makamba alisema taarifa hiyo ya ufisadi ndani ya Tanesco iliyotolewa na CAG imemsikitisha na kwamba hawezi kukaa kimya.

Taarifa ya CAG iliyoishia Juni 30, 2010 ambayo ilitolewa katika Mkutano wa Tatu wa Bunge uliomalizika karibuni, ilibaini kuwa Tanesco imeilipa kampuni ya Dowans Sh1.8 bilioni ikiwa ni gharama ya kusafirisha mitambo ya kampuni hiyo kuja nchini kwa ndege badala ya Sh180 milioni.

Matumizi hayo ya ziada yanayokadiriwa kufikia Sh1.4 bilioni yaliingizwa katika akaunti ya Dowans kulipia gharama za usafirishaji mitambo hiyo kimakosa.

CAG alisema hadi sasa, Tanesco imeshindwa kumpelekea ripoti ya matumizi ya fedha hizo alizoziita kuwa ni ufisadi.
Jana, Makamba alisema: "CAG ameona madudu ndani ya Tanesco na sisi kama Kamati ya Bunge tunaona ni muhimu Tanesco watoe maelezo. Tutadai watoe maelezo ya kuridhisha kuhusu ufisadi huo."

AlisemaTanesco inashangaza kwa kufanya madudu hayo na kukaa kimya muda mrefu kana kwamba haijui ilichofanya au haina ukaguzi wa hesabu.

Alisema ingawa anatambua kuwa jukumu la kuhoji hesabu ya mashirika ya umma ni la Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma iliyo chini ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kamati yake itadai maelezo hayo kwa kuwa inahusika na shirika hilo.Hata hivyo, katika taarifa yake ya ukaguzi CAG pia ameitaka Tanesco impelekee mchanganuo wa matumizi ya Dola
4,865,000 sawa na Sh6.8 bilioni.
 
Who can trust this an executive parliament to investigate her own mess in the government? Give us a break..........we are very jaded with these roller-coaster distractions in our own living rooms.............
 
Hongera Dr. Slaa kwa kazi nzuri nikitathimini sioni kama habari inaendana na title na isitoshe iki kilio Dr. amekilia sana sana kwenye vyombo vingi vya habari. Naona ni marudio ni bora wakati umefika tuchukue hatua hizi kelele naona kama hazisaidiiiiii kitu.!!! Naomba katika katiba mpaya silaa (AK 47) zimilikiwe na wananchi jamani tusisahau kipengele hiki muhimu sana.
 
Mitambo ya Dowans yauzwa Send to a friend Saturday, 21 May 2011 09:50

Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Marekani ya Symbion Power, imethibitisha kuwa imenunua mitambo ya kufua umeme ya Kampuni ya Dowans Tanzania Limited.

Hata hivyo, habari zaidi kuhusu mauzo hayo hazikutolewa kwa kuwa Dowans imepewa nguvu ya sheria ya kuzuia mtu kupewa siri za ndani za mipango hiyo bila idhini yake.

"Makubaliano yetu yamebanwa na vipengele vinavyozuia kuelezwa ovyo hadharani bila ruhusa ya muuzaji," alisema Mtendaji Mkuu wa Symbion Power, Paul Hinks.

Hinks aliwaambaia waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam kuwa tayari kampuni yake imesaini makubaliano ya ununuzi wa mitambo hiyo na Dowans na kwamba itatumika hapa nchini.


Dowans ndiyo iliyorithi mkataba wa kampuni tata ya Richmond Development LLC ambayo ilipewa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura nchini mwaka 2006 lakini ikashindwa kutekeleza mkataba huo.

Dowans iliingiza mitambo nchini na kuzalisha megawati 120 lakini mwaka 2008, Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco) liliamua kuvunja mkataba huo kwa kile kilichoelezwa kuwa ni ukiukwaji wa sheria katika uhamishaji wa mkataba.

Hata hivyo, Dowans iliishtaki Tanesco kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Biashara (ICC) ambayo iliamuliwa kuwa mkataba huo ulivunjwa kimakosa hivyo ikaamuliwa Serikali iilipe kampuni hiyo fidia ya Sh94 bilioni.

Tatizo la upungufu wa umeme limeendelea kulikabili taifa katika vipindi tofauti ikiwamo sasa na mara zote limekuwa likiibua mjadala kuhusu mitambo hiyo ambayo wakati fulani serikali ilitaka kuinunua bila ya mafanikio.


Iliwahi pia kuripotiwa kuwa serikali ilikuwa inafanya mkakakti wa kubadili Sheria ya Ununuzi wa Umma ili iruhusu ununuzi wa vitu vilivyotumika kwa lengo la kujenga mazingira mazuri ya kununua mitambo hiyo.

Kwa sababu hiyo, hatua ya kampuni hiyo ya Kimarekani kununua mitambo hiyo inafuta uwezekano wa serikali kuitwaa.

Katika mkutano huo na waandishi wa habari hakukuwepo na mwakilishi wa Dowans na hata kwenye taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Symbion Power haikutaja jina kampuni hiyo imbayo imezusha mijadala mingi nchini.

Hinks alijigamba kuwa kampuni yake ni miongoni mwa zile zinazofadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia mpango wake wa Millennium Challenge Corporation (MCC).

Isitoshe, akasema kampuni yake imeingia mkataba na Serikali ya Tanzania katika mpango mahsusi wa kuzalisha umeme vijijini chini ya Tanesco.Hata hivyo, alisema kuna uwezekano mkubwa wa kutumia mitambo hiyo kuzalisha umeme na kutatua tatizo la umeme linalokuwa linaikabili serikali mara kwa mara.

Alisema lengo la kampuni yake ni kuhakikisha kuwa Watanzania wanaendelea kupata umeme hata wakati ule ambao nchi inakabiliwa na upungufu wa nishati hiyo.Hata hivyo, alikiri kuwa kampuni yake inazo taarifa kwamba mzozo kati ya Dowans na Tanesco bado haujamalizika lakini akasema wanaamini ununuzi huo hauwezi kuingiliana na taratibu za kisheria na mahakama.

Alisema pamoja na mikwaruzano hiyo, jambo la kufurahisha ni kwamba kampuni yake imeamua kuingia katika mikakakti mizito ya kuwekaza Tanzania.

"Tunaunga mkono mikakati ya Wizara ya Nishati na Madini ya kutoa fursa za uwekezaji katika mpango wa ushirikiano wa kuzalisha nishati ya umeme," alisema.
 
Tanzania haijawahi kuongozwa na kilaza kama huyu anayejiita mkwe're, bogas kabisa
 
Welcome to Tanzania.

You are a real stranger that you need Dr. Slaa to spoon-feed you with evidence so that you undertand your national major problems and the key people around them.

I welcome you again so that you can have time to learn about Tanzania.

It does not need Dr. Slaa, the JF will sufficiently enrich you with all the evidences that you want. Just ask!!



Nadhani anamaanisha by implication hana evidence. It is a political game
 
uesday June 07, 2011
Local News
No deal signed yet between Simbion and TANESCO



By ORTON KIISHWEKO, 6th June 2011 @ 12:00, Total Comments: 0, Hits: 218

SYMBION Power has said the much awaited deal between them and the Tanzania Electric Supply Company (Tanesco) has not yet been sealed but expressed optimism for "good news" to come soon.

The Symbion Power Country Director, Mr Christopher Camponovo, told the 'Daily News' on Monday that in case the two parts signed a contract, the firm would produce up to 112MW.

Mr Camponovo, however, could not divulge details of the ongoing negotiations between the two parties but noted: "There have been no further developments since Sunday but we are hopeful of some good news very soon."

He confirmed that gas supply issues are being addressed by the concerned parties to allow the firm to operate according to TANESCO's requirements.

The firm had announced on Sunday that even as they were ISO rated at 112MW, they could only produce a maximum of 75MW due to the lack of gas.

He added: "Right now we are testing the machines and since we do that in stages we are only producing around 40MW of power. The 112MW rating is at the local design conditions, taking account of the temperature etc."

Asked whether Symbion would invest in more power generation soon, he said they were already working on the options that are available to increase power output.

"Once we have clear solutions in place we will make a proposal to increase capacity to TANESCO," said Mr Camponovo.

The firm announced that it switched on Ubungo turbines at its 120MW power plant in Dar es Salaam on trial basis and has been connected to the national grid since last Friday.
 
From Richmond to Symbion.......via Dowans...........kweli CCM wanajua namna ya kujivua gamba ............lakini tatizo sumu ya nyoka ipo palepale au hata imeongezeka.............
 
Back
Top Bottom