Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hiyo nyekundu nakuelewesha kuwa, Hao mapadre wanasomea mambo mengi sana na ndiyo maana kuna Madaktari Bingwa wengi sana Masista na mapadre na hata nyanja zingine nyingi tu. Tambua kuwa kuna vyuo, mashule, na vitengo mbalimbali katika kanisa na pia tambua kuwa viongozi wengi wa mwanzo wa nchi hii wenye taaluma maalum wamesoma huko, ila sheria za kuwa mapadre hazikuwaruhusu na wakaja huku katika siasa.
Kanisa ndo lilianza mambo ya upendo, umoja, amani na ndo sera zake ambazo Tz bado inajivunia.
Katiaka Bold; Jamaa kainua kwanza mishahara kimya kimya mara tu alipomsikia DR. wa kweli akinukuu ile hotuba na "wazee wa DAR" Mimi pia nishtuka kuona mshahara umeongezeka ghafla. Hilo ni dili tu na ni rushwa kwa mtu mkubwa kama yeye. Siku ile alidiriki hata kuwatukana wafanyakazi kupitia mwakilishi wetu, leo anakataa eti atatufikiria wapi na wapi.
Dr. slaa na haki ya kupinga. JK katuhonga laivu ni kwa vile tu sisi ni watanzania ingekuwa kwa wenzetu yaani kashatoka saa nyingi!!!
SEMA TU CCM NDO KASHIKA MPINI NA ATAFANYA LOLOTE KUIGEUZA ISHU
kAMA MUONGO KUWA NI WAMAFIA BASI SUBIRI UONE!
Hiyo nyekundu ni ungo mkubwa. Dr. Slaa hiyo sheria kaisomea wapi au sheria ya kanisa ndio inamfanya kubobea kitaaluma katika sheria?
Nawasiwasi kama Dr. Slaa hana washauri wa kweli. kwani habari ya mshahara kuongezeka sio ya leo na wala hajaanza baada ya kampeni. watu wamesha kula mishahara miwili mpya na kampeni hazina hata wiki sasa hapo si ukilaza jamani. Hao FOS au FOD wanamshauri nini kama ndio anatuletea hizi pumba hata kabla hajaanza kampeni.
Mimi sikuzungumzia Udaktari wa Slaa, nilichokuwa na pinga ni habari iliyosema Dr. Slaa kabobea katika taaluma ya sheria.
Nimesoma habari hii kwenye Gazeti la Mwenyekiti wa Chadema Mbowe la leo-Tanzania Daima habari hii ya Padri Slaa ina walakini. na haieleweki anasema kuwa JK anatumia majukwaa ya mikutano yake kueleza mafanikio ya serikali na pale anatakiwa aseme mambo ya chama tu.Jk alipeleka Ilani ya Chama chake kwa wananchi 2005 akawaambia kuwa mkinipa kura zenu kwa kupitia Ilani hii nitaunda serikali kutekeleza ahadi hizi.sasa kwa vile ametekeleza ahadi hizo ni lazima apite tena kwa wananchi na kuwaeleza kuwa tayari ametekeleza ahadi na sasa wampe nafasi afanye mengine.sasa Slaa alitaka JK aseme kitu gani?
kwenye Hili la mishahara Slaa anasema wao yaani yeye na Mgaya walitaka kima cha chini kiwe laki 315,000 na JK ameongeza toka 104,000 hadi 235,000 kama asilimia 126% kama Slaa ana mapenzi na wafanyakazi angesema kuwa asilimia 126% imeongezwa ni jambo zuri.sasa sielewi analalamika kwa vile hazikufika laki tatu na 15 elfu? kama zingefika asingeweka pingamizi? Slaa anajua yeye ni Small Fish in the big sea na shughuli ya Urais ni kubwa hana elimu wala uwezo wa kuifanya anatafuta sababu . source Tanzania Daima - Sauti ya Watu
Hutuba ya bajeti ya mwaka 2010/11 [Wizara ya fedha]
55. Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Nne inatambua umuhimu wa kuwa na maslahi bora ya wafanyakazi katika kuongeza ufanisi na tija. Serikali inachukua hatua za kuboresha maslahi ya wafanyakazi katika mwaka 2010/11. Sanjari na hatua hii, utaratibu wa kuhakiki mishahara utaendelea ili kudhibiti malipo kwa wafanyakazi hewa.
(ii) Kupunguza kiwango cha chini cha Kodi ya Mapato kwa wafanyakazi kutoka asilimia 15 hadi asilimia 14 sambamba na nyongeza ya kima cha chini cha mshahara kitakachotangazwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma. Lengo ni kuwaongezea kipato na kuwapunguzia mzigo wa kodi watumishi wa umma wenye kipato cha chini;
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA:
44. Mheshimiwa Spika
mishahara ya Watumishi wa Umma itaongezwa kwa
kuzingatia makubaliano yaliyofikiwa katika Baraza la Majadiliano ya Pamoja KatikaUtumishi wa Umma.
Utumishi wa Umma. Serikali itaandaa mkakati wa utekelezaji wa Sera ya Malipo ya
Mishahara na Motisha Katika Utumishi wa Umma mara baada ya Sera hiyo
kupitishwa. Aidha, Serikali itakamilisha uanzishaji wa Bodi ya Maslahi na Tija katika
{Kamati ya kujadili bajeti ya wizara ya nchi, ofisi ya rais, menejimenti ya utumishi wa umma}
Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani wakati nasoma hotuba yangu nimesema kwamba Serikali imekubali kuongeza kima cha chini sawa na makubaliano yetu na Vyama vya Wafanyakazi. Kwa kufanya hivyo Bajeti ya mishahara mwaka huu imeongezeka kwa shilingi bilioni 558 ukilinganisha na ya mwaka jana
Tuambie wapi mishahara hajapitishwa na bunge?
Shiiiit, nigga has a PHD in theology and he is treated like he has the real PHD. You know, the ones that you actually have to earn them. Eti Dr. Slaa. Come oon people. He might be a heck of a leader and visionary or whatever you guys want to anoint him to be, but acting like he is a law guru is a stretch.
And its bad politics going after wafanyakazi salaries. The Makambas of the world will spin this around and mtanzania wa kawaida will made it to believe kwamba Chadema is against the salaries. In politics its not about making sense--its about selling it to voters. Whoever has the loudest mouth wins the contests.
Leta source vinginevyo hatutaki majungu humu
Amekurupuka huyo na washauri wake wako kisiasa zaidi badala ya kutafuta ukweli.kura hazitafutwi hivyo .
Niliwahi kusoma mahali kwamba Small Minds discuss People halafu zingne zina-discuss events na zingine bora au kubwa zinadiscuss IDEAS, sasa tuwahurumie hao wanaomwona Slaa ni Padre, ni Mkatoliki baadae watamwona sio handsome, watagundua anakunywa pombe watasema mlevi, watamwona amechukua mke watasema sijui nini, lakini hawaoni kingine, wanaweza hata wakasema akivaa nguo hazimpendezi, ni small minds hawa,
tena mahali pengine waliandika usijibishane na mpungufu maana wote mtaonekana mapunguani, jamani!
Wewe ndio mbumbumbu kabisa mishahara haiongezwi hivyo hizo ulizobandika ni kauli za kisiasa. Mishahara inaongezwa kwa kamati maalum za bunge kukaa, kujadili na kupitisha figures ambacho ndicho anachodai Slaa kamati gani ya bunge ilikaa na kupitisha.Hutuba ya bajeti ya mwaka 2010/11 [Wizara ya fedha]
55. Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Nne inatambua umuhimu wa kuwa na maslahi bora ya wafanyakazi katika kuongeza ufanisi na tija. Serikali inachukua hatua za kuboresha maslahi ya wafanyakazi katika mwaka 2010/11. Sanjari na hatua hii, utaratibu wa kuhakiki mishahara utaendelea ili kudhibiti malipo kwa wafanyakazi hewa.
(ii) Kupunguza kiwango cha chini cha Kodi ya Mapato kwa wafanyakazi kutoka asilimia 15 hadi asilimia 14 sambamba na nyongeza ya kima cha chini cha mshahara kitakachotangazwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma. Lengo ni kuwaongezea kipato na kuwapunguzia mzigo wa kodi watumishi wa umma wenye kipato cha chini;
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA:
44. Mheshimiwa Spika
mishahara ya Watumishi wa Umma itaongezwa kwa
kuzingatia makubaliano yaliyofikiwa katika Baraza la Majadiliano ya Pamoja Katika
Utumishi wa Umma. Serikali itaandaa mkakati wa utekelezaji wa Sera ya Malipo ya
Mishahara na Motisha Katika Utumishi wa Umma mara baada ya Sera hiyo
kupitishwa. Aidha, Serikali itakamilisha uanzishaji wa Bodi ya Maslahi na Tija katika
Utumishi wa Umma.
{Kamati ya kujadili bajeti ya wizara ya nchi, ofisi ya rais, menejimenti ya utumishi wa umma}
Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani wakati nasoma hotuba yangu nimesema kwamba Serikali imekubali kuongeza kima cha chini sawa na makubaliano yetu na Vyama vya Wafanyakazi. Kwa kufanya hivyo Bajeti ya mishahara mwaka huu imeongezeka kwa shilingi bilioni 558 ukilinganisha na ya mwaka jana
Tuambie wapi mishahara hajapitishwa na bunge?
Wafanyakazi ni watiifu kwa nani, hilo ni relative term sijui unamaanisha watiifu kwa TUCTA kwa Mwajiri(JK) au kwa Slaa. Ungeniambia ni waoga ningekuelewa lakini waone hivyo hivyo wanaakili sana hao unaweza kuwadanganya wakabaki wanakutizama na usijue wanafikiri nini.Wafanyakazi wa Tanzania hawako hivyo unavyowafikiria. Hawajui kugoma. Ni watiifu sana. Wengi wao wanaridhika sana anapopewa nafasi inayomwezesha kufanya ubadhirifu. Hawatamwelewa Dr Slaa hasa katika kipindi hiki ambacho CCM inaweza kucheza rafu yoyote ile ikiwemo hiyo nyongeza kinyemela ya mishahara. CCM wanajua marefa wote ni wao. NEC, RPP na vyombo vya DOLA.
Haya ndiyo mambo muhimu ya kuongolea, sheria zimevunjwa, pesa za umma kutumiaka bila utaratibu maalum. Masuala kama haya ndiyo yanayogusa moja kwa moja maslahi ya watanzania kuliko kuongelea personal issues za upadri wa Slaa ambao haunisaidii.Sasa nyie wasiwasi wa nini? Kama hajavunja sheria, Mahakama itaamua. Itajulikana kama alitoa hongo au laa.
Pia itabidi aseme, pesa ametoa wapi kama bunge halijaidhinisha.
Kazi mnayo mwaka huu......... Kwa mara ya kwanza CCM imeanza kujibu mashambulizi.
Na bado Slaa akianza kurusha mabomu yake 19. Moja limesharushwa.