Geofrey Nyang'oro na Lilian Mazula-Mwananchi
SHERIA ni msumeno na sasa mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete atalazimika kufanya kazi ya ziada isimdhuru baada ya Chadema kumwekea pingamizi rais huyo wa serikali ya awamu ya nne.
...................................................................[deleted]
"Sehemu ya tano ya sheria hiyo sura ya 21.-(1) inaweka bayana vitendo vinavyokatazwa wakati wa uteuzi wakati wa kampeni za uchaguzi na inasomeka:
"(a)Kila mtu ambaye kabla au wakati wa kipindi cha kampeni, moja kwa moja au kwa namna nyingine yoyote, kupitia kwa mtu mwingine yeyote au kwa niaba yake, anatoa, anakopesha au anakubali kutoa au kukopesha, au anatoa, anaahidi au kumpatia au anajaribu kumpatia fedha yoyote au kitu chochote chenye thamani, mpiga kura au kwa ajili ya mtu yeyote kwa niaba ya mpiga kura yeyote au kwa ajili ya mtu mwingine yeyote kwa nia ya kumshawishi kupiga kura, au kuacha kupiga kura au kumrubuni mtu yeyote kutendo hicho kwa niaba ya mpiga kura huyo kupiga kura au kuacha kupiga kura katika kura za maoni au uchaguzi wowote;
.................................................[deleted]
"CCM wametumia Sh1.5 bilioni kutengeneza mabango nje ya nchi kwa kutumia fedha za serikali pia ankara ya malipo "invoice" inaonyesha imeandikwa 'VAT INVOICE' kitu ambacho hakieleweki," alisema Dk Slaa.
Alisema kuwa ni muhimu CCM kutoa ufafanuzi juu ya hilo kwa kuwa ushahidi upo na unaonyesha kuwa kuna mchezo mchafu umeanza kufanywa.