Nimesoma pia leo ktk Jambo Leo kwamba Chadema wameahirisha kuwasilisha pingamizi lao dhidi ya JK le ili kuwapa nafasi wanasheria wake walinoe zaidi. lakini habari kutoka kwa swahiba wangu katika uongozi wa ndani ya Chadema zinasema kuwa wanasheria hao wanataka kuhakikisha kwamba Tendwa hapati escape route yoyote ya ki-hoja ya kulitupilia mbali pingamizi hilo -- isipokuwa tu ibakie ile ya kuibeba tu CCM!
Kama kweli ameongelea tetesi la pingamizi basi Tendwa kachemka vibaya mno.
Mgombea wa CCM kwenye kiti cha urais, Mh JM Kikwete amewekewa pingamizi na Chama cha Demokrasia na maendeleo kwa kukiuka sheria aliyoisaini yeye mwenyewe. Imedaiwa kuwa ameongeza mishahara kwa wafanyakazi kinyume na taratibu za nchi kiyu ambacho kisheria kinaonekana ni rushwa. Je kweli Tendwa ataweza kusimamia haki?

Duh! Jamani sasa habari za chadema tutakuwa tunapata wapi maana naona kuna hatari tv zote zisitangaze hizi habari!! Nakumbuja ofisi ya AG kupitia TBC ilivyokanusha kikwete kufunguliwa kesi ya kupingwa kugombea urais, japo haikutoa maelezo mengi ila walikataa kabisa kuwa hamna kitu cha namna hiyo lakini ukweli kesi ipo na walitaka itupiliwe mbali japo mahakama imekataa! Naona hakuna habari za chadema tutakazo sikia. Chanel ten wameshaanza tayari kwenye taarifa yao kulikuwa na habari za kampeni za kikwete na malalamiko ya makamba nikajua chadema bado wanakula fungate kumbe leo walikuwa moro, napingamizi limewekwa!! Chadema plz tunahitaji altenative hapa hali itakuwa mbaya!
Source please..!