Elections 2010 Dr. Slaa mgombea urais 2010 kupitia CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Sasa hapo tunaanza kupata upinzani CCM, nadhani hapo hata mimi mwanaCCM nitampa kura yangu. Hongera mh Rais Mtarajiwa kupitishwa kugombea nafasi hiyo, maana sasa hakika watz tumepata mtu wa kutupa vitu tunavyotaka. Tanzania nakupenda, mungi bariki tanzania, mungu mbariki Rais Dr. W Slaa.


Chadema daima!
 

Dina uko sahihi kuwa watu waeneze Elimu kwa kila mtu as much as possible, lakini nadhani hauko sahihi kusema kuwa sisi wavijijini hatuna elimu ukilinganisha na nyie wa mjini na wenye access na internet na media. Nasema hauko sahihi kwasababu katika wabunge karibu 40 wa upinzani hakuna hata mmoja anayetoka kwenye majiji makubwa (Dar, Arusha, Mbeya, Mwanza) Hata miji Ukiondoa mji wa Moshi. Kwa hiyo ukitumia statistics hizo unaweza ukaona tunahitaji nguvu kubwa zaidi mjini kuliko vijijini, unaweza ukashangaa hata vijana kama akina Manyika wanashindwa kupata Ubunge Ubungo jimbo lenye wapiga kura wengi kutoka UDSM. Msitulaumu wa vijijini, nadhani sisi tumeamka kuliko nyie wa mjini, hata chaguzi ndogo za Busanda, biharamulo, Tarime zilikuwa na changamoto kuliko zilizofanyika mijini kama wa Mbeya Vijijini (sehemu kubwa ni mji)
 
MSAADA WA KISHERIA NA KIMAWAZO
Natafuta namna ya kumpigia Kampeni J. Kikwete kwa kutengeneza T-shirt kama 100,000 zenye maneno "SIHITAJI KURA ZA WAFANYAKAZI" alafu naweka PIcha yake na Jina lake. Nawezaje kukamilisha huu mradi wangu ndani ya miezi ya kampeni? Je nitakuwa navunja sheria? au kama nitafanya kama ni bidhaa za biashara ya kawaida hazina uhusiano na kampeni na chama chochote zitauzika na kukubalika kuwa mitaani?
 
Tatizo liko CCM ata akipata kura nyingi watazinyakua tuuu.
Hasara kwa bunge lijalo halitakuwa na msisimko jamaniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
Si wangemteua mtu mwingine wa kuongoza chama.Dah tumekosa mtu wa kutupigania bungeni
 
Kwa uteuzi wa mh. Silaa kuwa mgombea urais wa chadema, ni dhahiri kuwa chadema ni kijogoo kwa idadi ya wabunge, mungu tunakushukuru kwa kutuletea silaa, mlinde, mtunze, muwezeshe katika kujinadi na kuwanandi wabunge wengi ili udhalimu huu uishe, zaidi ajiandaa kupambana na fisadi papa 2015.
 
Natamani sana mdahalo utakaomshirikisha Kikwete na Dr. Slaa hapo ndipo tutakapoona pumba na mchele. Dr. Slaa is a higher level material atamfanya Kikwete aonekane a novice.
 
Nami yangu kwsa huyo huyo Dr S. Nilitaka kumpa Prof wa CUF, lakini naona Dr S ni imara kweli kweli katika vita ya ufisadi.
 
Jamani -- wanaochukia ufisadi tumpe kura Doctopr Slaa. Hurrah Doctor!
 
Hii ni nafasi adimu kwa watanzania kufanya mabadiliko ya uongozi, ili kupata uongozi bora chini ya Dr Slaa.

Ila kwa unafiki na ubabaishaji wa watanzania, nina mashaka tutabakia kupiga miayo tu tukitamani uongozi bora, huku mikononi tumekumbatia bora uongozi.
 
mbona hakuna aliyedhibitisha kuwa dr slaa atasimama kwa nafasi ya urais haya si ni maneno ya mitaani

mwenye source ya uhakika kuhusu tamko hilo aweke hapa,wote ni porojo tu
 
Natamani sana mdahalo utakaomshirikisha Kikwete na Dr. Slaa hapo ndipo tutakapoona pumba na mchele. Dr. Slaa is a higher level material atamfanya Kikwete aonekane a novice.

Safari hii atakubali?
 
Unaweza hata kutumia hii ya kwangu. Watengeneza GREEN VEST ZA KIJANI kwa Dar wako wengi tu. Kazi kwako.


 

Attachments

  • green%20tshirt.jpg
    30.4 KB · Views: 248
Unaweza hata kutumia hii ya kwangu. Watengeneza GREEN VEST ZA KIJANI kwa Dar wako wengi tu. Kazi kwako.
Asante sana mzee mwenzangu wa Sikonge, duu T-shirt imetoka vizuri sana, hiyo ni front side, tupate mawazo ya wadau nyuma iwe vipi, hatuna popular phrase nyingine fupi inayofaa kuwa nyuma. Nakumbuka "Ukitaka kula sharti uliwe" siipendi sana hii, haiteleweka, Nakumbuka "Asilimia 70 ni wafuata Upepo" hii inakuja kuja lakini sijui kama itamatch vizuri na ujumbe wa mbele.

KURA KWA DR. Slaa tusihame mada ha ha ha
 
Tushakujua we mvurugaji tu. Haya baba we endelea tu kuwachagua wenye uzoefu wa ufisadi!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…