Elections 2010 Dr. Slaa mgombea urais 2010 kupitia CHADEMA

Elections 2010 Dr. Slaa mgombea urais 2010 kupitia CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Nimebahatika kumwuliza hivyo, akasema tumtumie maswali au tutume mwandishi wetu Ijumaa wiki hii ili ajibu maswali yote na ikibidi kama tuna mapendekezo atatoa ufafanuzi kwa mapana.

Mambo ya Kubembelezana haya ndio maana siku zote tunakuwa kama Makondoo! CHADEMA nao wamwage Mboga tu watengeneze fulana na Mabango wayasambaze halafu wamsikilize Tendwa! Mwaga Mboga nimwage Ugali Ndicho kilichobaki ukimsema Umngojee Tendwa amkemee aliyemteua ni kupoteza Muda tu
 
Ni move nzuri kwa democracy Tz kwani ana uwezo mzuri na anakubalika kwa waelewa. Kushinda siyo rahisi ila kikubwa hapa ni elimu kwa wapiga kura kwani ana uwezo mkubwa wa kuelimisha jamii katika mambo ya msingi yanayogusa maisha ya kila mtanzania.
Nampongeza pia kwa kuwa ameamua kusacrifice ubunge kwa kuwa tunahitaji watu kama yeye kutoa changamoto kwenye uchaguzi wa urais kwani ni muhimu kwa mustakabali wa TZ.
Tutammiss sana kwenye bunge lijalo!
 
Mimi naona kuwa Dr Slaa kugombea urais ni serious miscalculation. Dr Slaa ametufaa sana katika nchi hii katika nafasi ya ubunge. Nina uhakika mchango wake baada ya uchaguzi huu utakuwa mchango finyu sana na tena usio na nguvu yoyote maana atakuwa anazungumza kama mgombea urais aliyeshindwa, atakachosema itahesabiwa ni 'maneno ya mkosaji', na ataingia rasmi katika fungu la 'wapuuzwa' akina Mrema, Lipumba etc. What a wrong move ya kutusababisha kumkosa Dr Slaa bungeni! Yaani hapo tutakosa vyote, urais hapati na ubunge keshautema! Too bad! I am mourning!
 
JMushi na Wana JF,{ Dr Slaa akijibu hoja ya JMushi 24th june 2010}
Nadhani askari anayeenda vitani kwa kukata tamaa ameshindwa hata kabla vita haijaanza.i) Tuwe na ujasiri, tunaoelewa tuwaelimishe na kuwatia ujasiri wale ambao au hawaelewi au hawajui uhusiano kati ya kura yao moja moja na hali mbaya ya maisha au maisha magumu wanayoishi. Watanzania kwa uzoefu wangu ni watu wasikivu sana, na ndiyo maana pamoja na nguvu ya Taifa ya CCM na Serikali hali ya ushindi ilikuwa wazi kabisa Bussanda na Biharamulo. Sisi wenyewe tuchukue hatua, tuwe "proactive" kila mmoja alipo na kwa kupitia marafiki zake. Multiplier effect principle ikitumika mabadiliko yatatokea katika nchi hii. ii) Kura zinahitaji tu kulindwa. Hakuna short cut, wala hakuna dawa wala uchawi katika hili. Hatutazuia rigging kwa maneno. We need to strategise and take action. We did it in Biharamulo and Bussanda and the results were visible. Wote wenye kukataa ufisadi, tusiukatae kwa maneno bali tuukatae kwa matendo. Wangapi kwa maneno tunaupiga vita lakini kugombea kila kukicha tunatangaza nia kupitia CCM. Kwa hali hii tusiwalau watanzania wa vijijini, kwani kama hata wasome bado wanaona ubunge unapatikana kupitia CCM tu, basi safari bado ni ndefu sana. Mabadiliko radical yanatakiwa kwetu sisi kabla ya wananchi, ambao wengi kukitokea Leadership watafuata bila wasiwasi. iii) Kimsingi mabadiliko yanaletwa na Rasilimali watu. Fedha ni nyenzo muhimu lakini, pre condition ni rasilimali watu. Kama wote wanaoandika kwenye jamvi hili tungelikuwa proactive, na kuamini kwa dhati tunayoandika, nina hakika mabadiliko yatatokea kwa sababu chachu muhimu sana na rasilimali watu inayofahamu Taifa linahitaji nini, Taifa linaelekea wapi na namna gani tuliepushe kutoka kwenye hatari hiyo. Lets play our part it can be done. Kukata tamaa ni dhambi mbaya isiyosameheka.

bila shaka Tanzania tumepata mkombozi . sasa ni juu yetu every body to play his /her part , naamini he is a very visionary and strategic leader kutokana na maneno yake na pia vitendo
 
Uteuzi wa Dr. Slaa ni strategic; mbali na kuwatoa jasho CCM na kuchangamsha kampeni, vilevile itasaidia kuwapa CHADEMA na upinzani wabunge wa kutosha kuongeza nguvu ya upinzani bunge lijalo.

Kushinda uraisi?? sina hakika kama Chadema wana mtandao wa atawi wa kutosha nchni kulinda kura zao ZISIIBIWE. Dr Slaa, tuko nyuma yako katika hili ingawa vilevile haitakuwa vizuri kuliachia jimbo la Karatu liende CCM?
 
I am so happy to hear this i like Dr

Natamani sana na naomba sna ili Dk Slaa ashinde. Kwa mtazamo wangu anafaa na anakubalika kwa wasomi wengi na wenye hekima wengi wa Tanzania hofu yangu ni je? ni Watanzania wangapi hutumia haki ya kura zao kuchagua viongozi bora na si bora viongozi. maana ukifuatilia nyanja za siasa utashangaa jinsi Watanzaia bado ni watu wakudanganywa na kofia ,vitenge,vilemba,kanga,t-shirts na nyama za ngombe na mbuzi. Ingawa si kwamba nimekata taamaa ila naamini Kuwa Dr ataleta Ushindani mkubwa sana kama si Kushinda kabisa. Laiti tungekuwa na tume huru ya Uchaguzi!
 
Mimi naona kuwa Dr Slaa kugombea urais ni serious miscalculation. Dr Slaa ametufaa sana katika nchi hii katika nafasi ya ubunge. Nina uhakika mchango wake baada ya uchaguzi huu utakuwa mchango finyu sana na tena usio na nguvu yoyote maana atakuwa anazungumza kama mgombea urais aliyeshindwa, atakachosema itahesabiwa ni 'maneno ya mkosaji', na ataingia rasmi katika fungu la 'wapuuzwa' akina Mrema, Lipumba etc. What a wrong move ya kutusababisha kumkosa Dr Slaa bungeni! Yaani hapo tutakosa vyote, urais hapati na ubunge keshautema! Too bad! I am mourning!

Mtu B nakubaliana na wewe katika hili..ILA naona pia kwamba wameshapiga mahesabu faida na hasara za DR. Slaa kugombe Urais mwaka huu...Muhimu ni kwamba kuna uwezekano mupinzani ukapata nguvu zaidi na wabunge wakaongezeka zaidi bungeni kutoka upinzani..ambalo ni la muhimu pi. Ikumbukwe kuwa pamoja na umuhimu wa Dr Slaa bungeni bado kura yake inabaki kuwa ni MOJA tu kulinganisha na zaidi ya 200 za CCM.

Hilo la kupooza baada ya uchaguzi itategemea mipango ya CHADEMA na upinzani kwa ujumla.....wana mikakati gani ya kuendeleza wimbi hilo baad aya uchaguzi? Maana kama CCM wana mikakati tayari for 2015, sioni ni kwa nini upinzani usiwe na mikakati hiyo kuanzia sasa..na mi nadhani, hili ni sehemu ya mikakatgi hiyo....kwa sababu mojawapo ni kwamba wananchi wengi wamelewa CCM...amini usiamini inahitajika nguvu kubwa kuwashawishi kinyume chake hasa mwaka huu unapoumzungumzie mtu kama JK mwenye kila kitu at his disposal! So mtu kama Dr. Slaa, ana uwezo mkubwa wa ushawishi wa kwanz akuwaelimisha watu na pia kuwaaamsha kutoka usingizini ili ikifika 2015 walau wawe wameelewa na iwe kazi rahisi kuleta mabadiliko

hapa mi naangalia zaidi 2015.......
 
Uteuzi wa Dr. Slaa ni strategic; mbali na kuwatoa jasho CCM na kuchangamsha kampeni, vilevile itasaidia kuwapa CHADEMA na upinzani wabunge wa kutosha kuongeza nguvu ya upinzani bunge lijalo.

Kushinda uraisi?? sina hakika kama Chadema wana mtandao wa atawi wa kutosha nchni kulinda kura zao ZISIIBIWE. Dr Slaa, tuko nyuma yako katika hili ingawa vilevile haitakuwa vizuri kuliachia jimbo la Karatu liende CCM?
Kwa uchungu na masikitiko makubwa, jimbo la Karatu litarudi CCM rasmi maana mwenyewe kaachia lindo! Too sad!
 
Mambo ya Kubembelezana haya ndio maana siku zote tunakuwa kama Makondoo! CHADEMA nao wamwage Mboga tu watengeneze fulana na Mabango wayasambaze halafu wamsikilize Tendwa! Mwaga Mboga nimwage Ugali Ndicho kilichobaki ukimsema Umngojee Tendwa amkemee aliyemteua ni kupoteza Muda tu
Koas moja halihalilishi jingine..CHADEMA tutafuata taratibu zote zilizowekwa.Tunaenda hatua kwa hatua biula kuvunja kanuni zilizopo.
 
Nini kinaweza kusababisha Chadema ishindwe nafasi ya urais kwa kunmsimamisha Dr Slaa? Na nini kitaifanya CCM ishinde urais kwa kumsimamisha Kikwete?
 
MS, suala la dini ni suala binafsi kati ya mtu na muumba wake, hivyo kutuletea hoja za udini katika mambo yanayohusu ustawi wa Taifa letu ni kuturudisha nyuma katika enzi za wagawe uwatawale. Wewe shida yako ni jk aendelee kuwa rais kwa vile ni muislamu mwenzako, lakini ujuwe kuwa yeye hajasaidia uislamu kwa lolote na kamwe hakuna rais atakaye saidia uislamu au dini yoyote,dini zitaendeshwa na waumini wenyewe, vuka mstari wa dini ufike kwenye utaifa , udini haukusaidii lolote.
 
Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki CHADEMA
Mungu akubariki, akulinde, akupatie ushindi na hatimaye utupatie yale tunayotumaini kwako

Safari ni ngumu laikini utashinda, jipe moyo.

Kura nitapiga pia
 
Koas moja halihalilishi jingine..CHADEMA tutafuata taratibu zote zilizowekwa.Tunaenda hatua kwa hatua biula kuvunja kanuni zilizopo.

Ni Kweli Kosa Moja Moja Halihalalishi Jingine lakini Ni Ukweli Kwamba Sometimes hilo Kosa Lingine Laweza kurekisha Kosa la Kwanza! the Ishu ni Kwamba CCM are doing campaing na Tume ya Uchaguzi is just Quiet
 
Mtu B nakubaliana na wewe katika hili..ILA naona pia kwamba wameshapiga mahesabu faida na hasara za DR. Slaa kugombe Urais mwaka huu...Muhimu ni kwamba kuna uwezekano mupinzani ukapata nguvu zaidi na wabunge wakaongezeka zaidi bungeni kutoka upinzani..ambalo ni la muhimu pi. Ikumbukwe kuwa pamoja na umuhimu wa Dr Slaa bungeni bado kura yake inabaki kuwa ni MOJA tu kulinganisha na zaidi ya 200 za CCM.

Hilo la kupooza baada ya uchaguzi itategemea mipango ya CHADEMA na upinzani kwa ujumla.....wana mikakati gani ya kuendeleza wimbi hilo baad aya uchaguzi? Maana kama CCM wana mikakati tayari for 2015, sioni ni kwa nini upinzani usiwe na mikakati hiyo kuanzia sasa..na mi nadhani, hili ni sehemu ya mikakatgi hiyo....kwa sababu mojawapo ni kwamba wananchi wengi wamelewa CCM...amini usiamini inahitajika nguvu kubwa kuwashawishi kinyume chake hasa mwaka huu unapoumzungumzie mtu kama JK mwenye kila kitu at his disposal! So mtu kama Dr. Slaa, ana uwezo mkubwa wa ushawishi wa kwanz akuwaelimisha watu na pia kuwaaamsha kutoka usingizini ili ikifika 2015 walau wawe wameelewa na iwe kazi rahisi kuleta mabadiliko

hapa mi naangalia zaidi 2015.......

My cent mheshimiwa, nakubaliana nawe, though its a bitter pill to swallow.
Tena kwa 2015, hata CCM wenyewe watakuwa na maruweruwe na mgombea wao manake naye atakuwa mpya machoni kwa wapiga kura!
 
Nimebahatika kumwuliza hivyo, akasema tumtumie maswali au tutume mwandishi wetu Ijumaa wiki hii ili ajibu maswali yote na ikibidi kama tuna mapendekezo atatoa ufafanuzi kwa mapana.

Dah hapa tusitegemee lolote.
Huyo Tendwa kaajiliwa na hao hao tusitegemee kama anaweza wapiga ngumi za usoni kwa rafu wanazocheza.
 
Du!,
Nimepata tetesi sasahivi wanamuandaa Prof. Mwesiga Beregu!. Kama kweli ni Dr. Slaa, CCM ikubali isikubali, JK mwaka huu, kazi anayo.

Lakini kwani CCM ya mwaka huu imeokoka? Hakuna mwaka CCM wameshinda bila kuiba kura na kunyanyasa wapinzani? Hicho kishindo umekielewa wanachokisema kila wakati? Tafsiri yake ni "Piga ua". Kwa hiyo ukisikia CCM itashinda kwa kishindo maana yake itashinda kwa kutumia njia zozote unazozijua na usizozijua.

Ndio maana alishasema hana haja na kura za wafanyakazi milioni tatu na ndugu zao, kwani ameshinda hata kabla kura hazijapigwa. Hujasikia mtu anashiba hata kabla hajaanza kula? Ndiyo ccm ya jana na leo, siijui ya kesho. Kwa hiyo nakubaliana na wachangiaji wanaosema Slaa atasaidia kuikomaza chadema lakini hata kama kura zake zitakuwa nyingi kuliko za ccm ajiandae kuwa na leso ya kufutia machozi kwani ati Ikulu ni trade mark ya ccm, subiri uone kama unabisha.
 
Lakini nashangaa sana. Wakati wa vikao vya ccm tv zilikuwa zinaongelea habari za ccm na kuwaonyesha wakikata viuno pale dodoma mpaka walipofunga. Sasa mbona chadema tunasikia hitimisho tu na hakuna hata tv moja iliyozungumzia kuwako kwa kikao hicho????? Wapinzani kwa sasa kuingia ikulu ni sawa na muvi za kinigeria, hata kama wataunganisha nguvu kuwa na mtu mmoja, kwa sababu kila chama kinatumia wasaa huu kujulikana hadi vijijini na wala malengo yao sio kweli kwenda ikulu kama kipaumbele. Uchaguzi ukiisha kuna vyama ambavyo hata majina yao yanakuwa magumu kuyataja, maana ni kama huwa havipo. Chadema is very strong bara na cuf kule visiwani. Lau kama wangeungana hawa wawili, kishindo kinachoshindiliwa na ccm kingepata shida si haba.
 
Bravo Dr, nimefurahi sana na hili, jana ktu nilikuwa nawaambia watu hapa Ndola, kuwa itakuwa suprise kwa JK na timu yake pale mtanzania mzalendo wa kweli atakapo tangazwa kuwa mgombea wa uraisi, am very sad kuwa kura yangu haitakuwa counted, tarehe 31 october sitakuwepo home, haya maisha jamani yanasababisha mtu kukosa ujenzi wa taifa lako, lakini am sure kama sitapiga kura then nitatatoa mchango wangu wa dhati kuhakikisha tunasonga mbele
 
Huyu jamaa huwa ananinyevua sana...
Itabidi tupige kura za maoni wangapi hawampendi Maralia Sugu.

Tumpigie kampeni kila analosema wote tunajibu kwa neno moja tu "PUMBA" baasi ataacha kutuchafulia hewa humu..!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom