I WISH DR SLAA AWE RAIS WETU,MUNGU MTANGULIE NA AFANYE MIUJIZA, Halafu tufanye yafuatayo:
1. Tuishinikize tume ya uchaguzi kutoa majina ya wapiga kura mapema kwa kila eneo walilojiandikisha ,make wana mchezo wa kupeleka jina sehemu nyingine( hasa sehemu ambazo ni tishio kwa CCM)ukienda kuangalia jina lako unakuta halipo, wanasema watashughulikia mara saa kumi na mbili inafika muda wa kupiga kura unaisha unakuwa umekoswa haki yako ya kupiga kura, hivyo watoe majina mapema na kwa usashihi ili wapiga kura wajue mapema kama majina yao yapo kwenye kituo walichojiandikishia.
2.Serikali iruhusu wanafunzi wa vyuo vikuu wapige kura za kumchagua Rais majumbani kwao kwani wengi wamejiandikisha kwenye vyou vyao( DSM,Morogoro,Dodoma ,Iringa na mahala pengine) lakini Vyuo vitafunguliwa baada ya uchaguzi hivyo watashindwa kupiga kura huko majumbani kwao watakapokuwa likizo.
3.CUF na NCCR Mageuzi viunganishe nguvu na CHADEMA,Lipumba amuachie Dr Slaa kwani kwa sasa nyota ya Dr Slaa inang'ara sana kuliko Lipumba,Dr anakubalika sana kwa sasa, tuachane na vyama vingine waganga njaa( TLP,UDP na vingine vilivyopo tu kwenye orodha ya msajili wa nyama,havijulikani kabisa nchini).
4. Sisi wenye uelewa na machungu ya nchi hii tuwahamasishe ndugu zetu(Kila mmoja ahamasishe ndugu zake huko vijijini )waache woga kwamba vyama vya upinzani vikiongoza nchi kutatokea ukosefu wa amani.Hizo ni propaganda tu za akina makamba na CCM yake.