Elections 2010 Dr. Slaa mgombea urais 2010 kupitia CHADEMA

Elections 2010 Dr. Slaa mgombea urais 2010 kupitia CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Hongera sana Dr. Slaa. nimefarijika sana baada ya kupokea habari ya kwamba umetangaza nia kugombea Urais wa JMT. unasitahili kwa asilimia 100 kutuongoza watanzania.Bado ninaikumbuka hotuba yako ya mwembeyanga kuhusu orodha ya mafisadi, tangu wakati huo nilifuatilia kwa makini sana kuona ukweli wa hotuba yako uliyoitoa na baadaye ukweli pasipo shaka nimeuona. hivi sasa ninakuona wewe ni mtu muhimu sana ktk ukombozi wa Taifa hili. Sijawahi kupiga kura lakini safari hii ni lazima nikapige kura wewe nitumaini lililorejea tena!!!
 
I WISH DR SLAA AWE RAIS WETU,MUNGU MTANGULIE NA AFANYE MIUJIZA, Halafu tufanye yafuatayo:
1. Tuishinikize tume ya uchaguzi kutoa majina ya wapiga kura mapema kwa kila eneo walilojiandikisha ,make wana mchezo wa kupeleka jina sehemu nyingine( hasa sehemu ambazo ni tishio kwa CCM)ukienda kuangalia jina lako unakuta halipo, wanasema watashughulikia mara saa kumi na mbili inafika muda wa kupiga kura unaisha unakuwa umekoswa haki yako ya kupiga kura, hivyo watoe majina mapema na kwa usashihi ili wapiga kura wajue mapema kama majina yao yapo kwenye kituo walichojiandikishia.
2.Serikali iruhusu wanafunzi wa vyuo vikuu wapige kura za kumchagua Rais majumbani kwao kwani wengi wamejiandikisha kwenye vyou vyao( DSM,Morogoro,Dodoma ,Iringa na mahala pengine) lakini Vyuo vitafunguliwa baada ya uchaguzi hivyo watashindwa kupiga kura huko majumbani kwao watakapokuwa likizo.
3.CUF na NCCR Mageuzi viunganishe nguvu na CHADEMA,Lipumba amuachie Dr Slaa kwani kwa sasa nyota ya Dr Slaa inang'ara sana kuliko Lipumba,Dr anakubalika sana kwa sasa, tuachane na vyama vingine waganga njaa( TLP,UDP na vingine vilivyopo tu kwenye orodha ya msajili wa nyama,havijulikani kabisa nchini).
4. Sisi wenye uelewa na machungu ya nchi hii tuwahamasishe ndugu zetu(Kila mmoja ahamasishe ndugu zake huko vijijini )waache woga kwamba vyama vya upinzani vikiongoza nchi kutatokea ukosefu wa amani.Hizo ni propaganda tu za akina makamba na CCM yake.

Hapo ndipo penyewe, sasa tuangalie maslahi ya nchi na si vyama. Chonde chonde CUF kubalini ukweli, tumpe Dr Slaa. Prof wangu Lipumba tafadhali ungana na Slaa tuikomboe nchi yetu.
 
Habari zilizopatikana sasa hivi zinasema kwamba Dk. Slaa ndiye mgombea urais wa Chadema mwaka 2010.

9036dj.jpg

Kikao kilichomchagua Dr. Slaa kuwa mgombea urais wa CHADEMA

More to come

hakishindwa katika uchaguzi huu wa raismbasi tena bungeni hayupo!ccm itatawala bungeni
 
Mie nningependa sana Dr. Slaa achukue uraisi toka kwa Jk ila ukweli ni kuwa atashindwa tu hata kwa tofauti ya asilimia 1 kamalivyokuwa kwa uchaguzi wa Zanzibar 1995. Labda achukue uzoefu wa mwaka huu then ajipange kwa uchaguzi wa 2015 maana wakulu wa CCM watafanya kila liwezekanalo JK awe raisi kwa mara nyingine tena.
 
Anagombea shingo upande -- hakuwa anataka. Kama alivyosema Baba wa Taifa, Mwl Nyerere -- wanaogombania kwenda Ikulu waangaliwe sana...kwani Ikulu ni mzigo mzito ....huenda wanakimbilia mambo mengine.

Hurrah.. Dr Slaa!!! Ingawa umeonyesha reluctance, inabidi ujitose tu.. kwani umeonyesha mfano mzuri kwa wanaowania nafasi hiyo. Kwa kiwango fulani, utaikisa CCM. Lakini pia hakikisha unamuachia mgombea mzuri hapo Karatu, na umpigie kampeni kali.
 
Hapo ndipo penyewe, sasa tuangalie maslahi ya nchi na si vyama. Chonde chonde CUF kubalini ukweli, tumpe Dr Slaa. Prof wangu Lipumba tafadhali ungana na Slaa tuikomboe nchi yetu.
Hii hoja ya kuunganisha nguvu siipingi ila tuiangalie kwa upana wake zaidi.....Lazima tuwe na Ideology inayofanana maana tukisema Lengo ni Kuing'oa ccm then after that nn kifuate? Isije ikawa kama Kenya, Lengo la wapinzani lilikua kuing'oa KANU baada ya lengo Wakaparaganyika...kwa hiyo na sisi tusifuate mtazamo huo!! wapinzani wawe na Ideology inayo fanana na lengo lisiwe kuing'oa ccm tu bali kuistawisha nchi kwa maendeleo ya watanzania wote!!
 
mimi ninamaswala haya kwa dk slaa
1)endapo atashinda uchaguzi na kuwa rais nini atafanya katka kurudisha mahakama ya kadhi
2) vipi kuhusu swla la oic
3) vipi kuzibadilisha kuwa siku za mapumziko kuwa j3 na j4 badala ya j1 na j2 au kuongeza ijumaa?

Namba 3 sijaielewa, kuna rais aliyepita aliyefanikiwa hili?
 
Amejiandaaje kukaa miaka mitano kijiweni, simshauri kwa kuwa atapunguza msisimko bungeni

I am in a limbo! Ni uteuzi unaofaa sana ingawa huyu mtu tutamkosa Bungeni na kwa kuwa nafasi tya kuukwaa u-presidaa kwa sasa ni ngumu kwake, lakini ukweli ni kuwa ataiongezea CHADEMA chati na nadhani CHADEMA wanapiga hesabu kali za 2015. Uteuzi huu ni LITMUS paper kwa CCM, CUF na Watanzania kwa ujumla.

Maombi yangu ni kwamba Dk Slaa ashinde ingawa ni vigumu sana (kwa kuwa bado hatujafikia uchaguzi huru na wa haki
) maana CCM mentality bado iko kwa viongozi wengi sana hasa vijijini na hatuna Tume huru ya Uchaguzi.

Hata hivyo nabashiri kuwa Dk Slaa hatakosa lau nafasi ya pili na naweza kuona Prof Lipumba akirejea nyuma hatua moja.
 
Nimesha shawishika vya kutosha kura yangu nitampa Dr.
 
MABADILIKO NI LAZIMA
Mungu ibariki Tanzania. Juzi nilitabiri kuwa
Chadema 52%
Thithiem 39%
CUF 8%
TLP 1%
 
Nimefarijika sana na hatua ya CHADEMA kupitisha Dr Slaa kuwa mgombea wa nafasi ya urais kuptia chama chake, Na Mpongeza mno Bwana Slaa na kumsiha aanze kazi maramoja ya kukusanya kura za urais pia akitilia mkazo ushindi majimboni na wa bunge.

Nawaomba watanzania wote Tumjaribu ndugu yetu huyu, tunaweza pata sura mpya ya maendeleo yetu.
 
Mrs. Slaa ni kada wa ccm, diwani nafikiri, sasa sijui atam-join Mr au ataheshimu instructions za Sofia Simba?

Kwa maoni yangu Mrs Slaa ingefaa ahame chame - either to Chadema au Chama-less: haileti mantiki kuwa na "first-lady to be" in opposition camp!
 
can you think beyond the next meal lady!?

Am really trying hard, but I don't see any candle light at the end of the tunnel! Though 'if wishes were horses.......' if you know what I mean! Hesabu za haraka haraka my home villages (both), are 'blanketed' with the ruling party. Na hata wachangiaji wengi humu wako mijini, ukiwepo wewe pia, unless hii elimu and support mnayotoa hapa muipeleke kule pia. Kwa sababu wengi wetu mnaotushawishi through here, we know what we want, the majority ambao ndio wapiga kura wenyewe hawana a wala b! Na kibaya zaidi, wengi wenu(tu) wapiga debe you don't even line up for the real voting exercise on the D day, kisa you can't tolerate the hassles packed in the whole exercise.

Kwa hiyo ndugu fikiria jinsi ya kuwashawishi the majority kwanza, especially if you can do that ndani ya miezi iliyobaki.
 
Kwa maoni yangu Mrs Slaa ingefaa ahame chame - either to Chadema au Chama-less: haileti mantiki kuwa na "first-lady to be" in opposition camp!

Dr Slaa amekuwa hivyo alivyo akiwa na huyu mama. Sioni tatizo hapo. Hachanganyi siasa za chumbani na utumishi wake kwa Watanzania.
 
tawanyikeni mukaeleze na kuota elimu kwa watu,

ili wamchague mgombea huyu.

kuna yeyote kati yenu hapa jf bado hajarekebisha kadi yake ya kupigia?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom