Aisee wewe mkuu una akili sana, unafaa kuwa mshauri wa masuala ya kisiasa wa wanasiasa wote Tanzania maana unaweza kusoma maandishi ya watu na kujua fikra zao .......... ohhh fcku it ...... kimekuchoma sana moyoni kuona Kikwete akipata upinzani wa nguvu.
Wakoritho endelee kujipa moyo tu, lakini nina habari mbaya kwenu njii hii kamwe haitatawaliwa na Padri
mkuu ndoto zingine sio muhimu sana kuziweka kichwani.
uchaguzi nchini kwetu sio wa haki na ndio nina uchungu wa nchi yangu na ni vizuri wapinzani wajaribu kupata msaada kwa mabalozi
hili hili swala liweze kurekebishwa la sivyo ni kupoteza mda tu kwenye nafasi ya uraisi.
analysis yangu ni bomba na ndio maana dk slaa kutoka bungeni si muhesabu mtu mmoja kama wewe,dk slaa kwangu mimi pale bungeni ni zaidi ya wabunge 50 wa ccm wanao sinzia hovyo hovyo na kucheka cheka hovyo hovyo wakati wana nchi waliowapa nafasi wana matatizo chungu mzima.
hakuna kosa kuweka nguvu yoyote kwenye uraisi + ubunge tatizo ni timing mbovu.wangejaribu kusaidiana kwa nguvu zote na mali kuongeza wabunge wa upinzani kwani hio inasaidia kuweza kuwafikia wananchi zaidi hapo mbeleni tukipata mgombea mwenye sifa zote kama Dr Slaa.
sasa hivi ccm wameshika majimbo kibao wewe unaenda kuwataka wamchague Dr Slaa watakuelewa vipi wakati ccm imewateka akili? haya majimbo ya ccm tukiweza kuyateka kwenye nafasi za ubunge kwa kufanya kampeni za nguvu na kufanikiwa uchaguzi ujao utakuwa rahisi sana kupata kura za hawa wananchi na itakuwa vigumu kwa ccm kufanya madudu yao inawapa hesabau ya mgombea wao kuchagulia kwa asilimia 80 ya watanzania.
Nguvu zaidi zipelekwa vijijini huko uchaguzi sio dar es salaam peke yake.
Hivi nyie,,,, nani kawaambia kuwa huu ni upinzani wa nguvu?! Nani hasa amewakoroga akili kihivyo? Duh!. Nimeacha. Maana huu ni ubishi. Un-organised discussion and not fact finding mission..
hongera sana mkuu na nakumbuka kampeni yako na mimi nilikuwa katika kundi la kupinga na kama nilivyo kwambia kipindi kila na sasa hivi sababu yangu kubwa ni uchaguzi sio wa haki.Bila kujali kama atashinda ama atashindwa, ukweli ni kuwa CCM watafahamu kwamba wakicheza watakwenda na maji. Kitakachofaa sasa ni kuchagua Watu kadhaa kugombea ubunge kwa ticket ya Chadema na kuhakikisha wanashinda. Hawa wachache wakiwa machachari basi CCM watafahamu kuwa mwaka 2010 unakuja na hawatafanya lele mama na kuwa Watalii wa dunia wakati upinzani unajiandaa.
Amini usiamini, hata kama Slaa atabaki nje ya bunge, lakini atamkalia Kikwete kooni na wala hatampa kuhema. Slaa atakuwa free kumkosoa kila mara. Kama bunge kakaa term 3, ni muda sasa wa kupanda cheo au kuachia ngazi. Hadi leo zaidi ya kufichua siri kafanya nini? CCM hawana aibu kabisa na pamoja na kufichuliwa siri zao, wala hawaabaiki. Hebu ona hawa Ma dr. Feki bado ni mawaziri. Magufuli hadi anatukana uzembe wa Waziri wa mambo ya ndani, lakini CCM wala. Majambazi wanazidi kutesa, CCM wala. Unafikiri CCM wanamuogopa tena Slaa kama mbunge? Hell no.
Dr. Slaa, kampeni tumeanza. Tutawasiliana na ndugu na jamaa katika familia zetu na tuna imani watasikiliza maombo yetu.
Baada ya hii habari nilimpigia mmoja wa wana CCM, yeye anasema Slaa sio tishio kwa sababu Chadema haina network vijijini, tujadili hili pia
Je, ungempigia simu Makamba, Malecela au Tambwe Hiza, wao ungetegema waseme nini, kuwa Chadema ni tishio ? Subutu. Unakumbuka walisemaje huko Tarime, Busanda au Biharamulo ? Umejiuliza kama ingetokea Mbowe kahamia CCM, je TBC na michuzi wangekuwa kimya hadi sasa ? Saharavoice ndugu yangu, hili jambo linawaumiza wengi na kama alivyosema mchangiaji moja leo huko Ulaya hata kuku hatafuniki.
Tukirudi kwa huu uamuzi wa Dr. Slaa kugombea Uraisi, subiri uone changamoto itakayotokea na mori watakayokua nayo wanachama wa Chadema na wananchi kwa ujumla. Amini usiamini wagombea ubunge kutoka Chadema tayari betri zao zimewekwa chaji na indiketa zao zimewashwa. Najua humu JF itakakuwa rahisi sana kuwatambua wale wasindikizaji na wanafiki ambao hiki kitendo bado kimewapiga sindano ya ganzi.
Najua pia rafu sasa zitachezwa kikwelikweli na si ajabu vyombo vya dola vikatumika kuwaathiri wagombea kwa kuwashusha majukwaani. Lakini ole wao wakifanya hivyo safari hii kwani kama nyuma walipambana na mvua za rasha rasha, safari hii watapambana na dhoruba - yaani nguvu ya wananchi waliochoka kunyanyaswa na kuibiwa. Hii ni kwa sababu mwishowe amejitokeza kiongozi jasiri asiyeyumbishwa na asiyetetereka.
Wakoritho endelee kujipa moyo tu, lakini nina habari mbaya kwenu njii hii kamwe haitatawaliwa na Padri
Nonsense.
Angekuwa Sheikh Yahya ndo ungefurahi?
Huko unakotaka kuelekea ndiko kutamu na CCM walio welevu hawataki hata kupagusia maana ni moto kote kote.Wakoritho endelee kujipa moyo tu, lakini nina habari mbaya kwenu njii hii kamwe haitatawaliwa na Padri
Naona wewe ungekuwa kocha wa Ghana ungewaambia wasishiriki kombe la dunia maana uwezekano wa wao kushinda ni mdogo, lakini tumeona matokeo yake walifika robo fainali.we ndugu wewe. Huwezi ukaomba kufanya UE wa physics wakati wewe ni ngwine per se. Hiki ndiyo kimetokea hapa. Kumbuka kuwa hata wanaomchekea Slaa usije ukadhani wote wanamfurahia. In fact wengi wanamcheka.
Nani aliyekwambia mwaka huu kutakuwa na idadi kubwa ya wabunge wa Chadema ku-warrant kuteuliwa wengi? Wabunge wa kuteuliwa hawaiingii tu bungeni kwa miguu au kwa ku-drive. Kuna mchakato wake. Let us be realistic kwa level ya JF.