Elections 2010 Dr. Slaa mgombea urais 2010 kupitia CHADEMA

Elections 2010 Dr. Slaa mgombea urais 2010 kupitia CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Wakoritho endelee kujipa moyo tu, lakini nina habari mbaya kwenu njii hii kamwe haitatawaliwa na Padri
 
Aisee wewe mkuu una akili sana, unafaa kuwa mshauri wa masuala ya kisiasa wa wanasiasa wote Tanzania maana unaweza kusoma maandishi ya watu na kujua fikra zao .......... ohhh fcku it ...... kimekuchoma sana moyoni kuona Kikwete akipata upinzani wa nguvu.

Hivi nyie,,,, nani kawaambia kuwa huu ni upinzani wa nguvu?! Nani hasa amewakoroga akili kihivyo? Duh!. Nimeacha. Maana huu ni ubishi. Un-organised discussion and not fact finding mission..
 
mkuu ndoto zingine sio muhimu sana kuziweka kichwani.
uchaguzi nchini kwetu sio wa haki na ndio nina uchungu wa nchi yangu na ni vizuri wapinzani wajaribu kupata msaada kwa mabalozi
hili hili swala liweze kurekebishwa la sivyo ni kupoteza mda tu kwenye nafasi ya uraisi.

Duly noted

analysis yangu ni bomba na ndio maana dk slaa kutoka bungeni si muhesabu mtu mmoja kama wewe,dk slaa kwangu mimi pale bungeni ni zaidi ya wabunge 50 wa ccm wanao sinzia hovyo hovyo na kucheka cheka hovyo hovyo wakati wana nchi waliowapa nafasi wana matatizo chungu mzima.

Kwa nini pia usiangalie possibility ya kushinda uraisi? kwani nani kasema kuwa uraisi ni kwa wanaccm pekee?

hakuna kosa kuweka nguvu yoyote kwenye uraisi + ubunge tatizo ni timing mbovu.wangejaribu kusaidiana kwa nguvu zote na mali kuongeza wabunge wa upinzani kwani hio inasaidia kuweza kuwafikia wananchi zaidi hapo mbeleni tukipata mgombea mwenye sifa zote kama Dr Slaa.

Kuna tofauti gani kwa Slaa kugombea uraisi au ubunge when it comes to kusaidia wengine kupata ubunge? Slaa ni mtu mmoja, hii bado haizuii chadema kuweka wabunge wengi bungeni kama wanataka/weza.

sasa hivi ccm wameshika majimbo kibao wewe unaenda kuwataka wamchague Dr Slaa watakuelewa vipi wakati ccm imewateka akili? haya majimbo ya ccm tukiweza kuyateka kwenye nafasi za ubunge kwa kufanya kampeni za nguvu na kufanikiwa uchaguzi ujao utakuwa rahisi sana kupata kura za hawa wananchi na itakuwa vigumu kwa ccm kufanya madudu yao inawapa hesabau ya mgombea wao kuchagulia kwa asilimia 80 ya watanzania.

Bado hujasema kuwa kugombea uraisi kunazuia vipi kupata wabunge zaidi

Nguvu zaidi zipelekwa vijijini huko uchaguzi sio dar es salaam peke yake.

Uliwahi kusikia operesheni sangara iliyokwenda vijijini?
 
Hivi nyie,,,, nani kawaambia kuwa huu ni upinzani wa nguvu?! Nani hasa amewakoroga akili kihivyo? Duh!. Nimeacha. Maana huu ni ubishi. Un-organised discussion and not fact finding mission..

fact finding mission after the ..... well .... fact?
 
Bila kujali kama atashinda ama atashindwa, ukweli ni kuwa CCM watafahamu kwamba wakicheza watakwenda na maji. Kitakachofaa sasa ni kuchagua Watu kadhaa kugombea ubunge kwa ticket ya Chadema na kuhakikisha wanashinda. Hawa wachache wakiwa machachari basi CCM watafahamu kuwa mwaka 2010 unakuja na hawatafanya lele mama na kuwa Watalii wa dunia wakati upinzani unajiandaa.

Amini usiamini, hata kama Slaa atabaki nje ya bunge, lakini atamkalia Kikwete kooni na wala hatampa kuhema. Slaa atakuwa free kumkosoa kila mara. Kama bunge kakaa term 3, ni muda sasa wa kupanda cheo au kuachia ngazi. Hadi leo zaidi ya kufichua siri kafanya nini? CCM hawana aibu kabisa na pamoja na kufichuliwa siri zao, wala hawaabaiki. Hebu ona hawa Ma dr. Feki bado ni mawaziri. Magufuli hadi anatukana uzembe wa Waziri wa mambo ya ndani, lakini CCM wala. Majambazi wanazidi kutesa, CCM wala. Unafikiri CCM wanamuogopa tena Slaa kama mbunge? Hell no.

Dr. Slaa, kampeni tumeanza. Tutawasiliana na ndugu na jamaa katika familia zetu na tuna imani watasikiliza maombo yetu.
hongera sana mkuu na nakumbuka kampeni yako na mimi nilikuwa katika kundi la kupinga na kama nilivyo kwambia kipindi kila na sasa hivi sababu yangu kubwa ni uchaguzi sio wa haki.

wapinzani wanatakiwa wa step up sana kwenye hili swala la kuhesabu kura uchaguzi huu na ikiwezekana waombe msaada kutoka nchi za nje kwenye hili swala.
 
Baada ya hii habari nilimpigia mmoja wa wana CCM, yeye anasema Slaa sio tishio kwa sababu Chadema haina network vijijini, tujadili hili pia

Je, ungempigia simu Makamba, Malecela au Tambwe Hiza, wao ungetegema waseme nini, kuwa Chadema ni tishio ? Subutu. Unakumbuka walisemaje huko Tarime, Busanda au Biharamulo ? Umejiuliza kama ingetokea Mbowe kahamia CCM, je TBC na michuzi wangekuwa kimya hadi sasa ? Saharavoice ndugu yangu, hili jambo linawaumiza wengi na kama alivyosema mchangiaji moja leo huko Ulaya hata kuku hatafuniki.

Tukirudi kwa huu uamuzi wa Dr. Slaa kugombea Uraisi, subiri uone changamoto itakayotokea na mori watakayokua nayo wanachama wa Chadema na wananchi kwa ujumla. Amini usiamini wagombea ubunge kutoka Chadema tayari betri zao zimewekwa chaji na indiketa zao zimewashwa. Najua humu JF itakakuwa rahisi sana kuwatambua wale wasindikizaji na wanafiki ambao hiki kitendo bado kimewapiga sindano ya ganzi.

Najua pia rafu sasa zitachezwa kikwelikweli na si ajabu vyombo vya dola vikatumika kuwaathiri wagombea kwa kuwashusha majukwaani. Lakini ole wao wakifanya hivyo safari hii kwani kama nyuma walipambana na mvua za rasha rasha, safari hii watapambana na dhoruba - yaani nguvu ya wananchi waliochoka kunyanyaswa na kuibiwa. Hii ni kwa sababu mwishowe amejitokeza kiongozi jasiri asiyeyumbishwa na asiyetetereka.
 
Hii ni habari njema lakini ambayo ina ubaya wake pia.

Uzuri wake ni kama akifanikiwa kuongeza idadi ya wabunge itachangia chaguzi zijazo watu wengi kujitokeza kugombania kwa kupitia upinzani na itawatia moyo wabunge kiduchu wa ccm wanaopiga vita ufisadi.

Ubaya akishindwa kuongeza idadi ya wabunge matokeo yake itavunja watu wengi moyo na itachangia kuongezeka kwa mafisadi.Itadhibitisha Watanzania wengi tunaunga mkono ufisadi.Itampa kichwa Kikwete na kumfanya aweke pamba masikioni.
 
Je, ungempigia simu Makamba, Malecela au Tambwe Hiza, wao ungetegema waseme nini, kuwa Chadema ni tishio ? Subutu. Unakumbuka walisemaje huko Tarime, Busanda au Biharamulo ? Umejiuliza kama ingetokea Mbowe kahamia CCM, je TBC na michuzi wangekuwa kimya hadi sasa ? Saharavoice ndugu yangu, hili jambo linawaumiza wengi na kama alivyosema mchangiaji moja leo huko Ulaya hata kuku hatafuniki.

Tukirudi kwa huu uamuzi wa Dr. Slaa kugombea Uraisi, subiri uone changamoto itakayotokea na mori watakayokua nayo wanachama wa Chadema na wananchi kwa ujumla. Amini usiamini wagombea ubunge kutoka Chadema tayari betri zao zimewekwa chaji na indiketa zao zimewashwa. Najua humu JF itakakuwa rahisi sana kuwatambua wale wasindikizaji na wanafiki ambao hiki kitendo bado kimewapiga sindano ya ganzi.

Najua pia rafu sasa zitachezwa kikwelikweli na si ajabu vyombo vya dola vikatumika kuwaathiri wagombea kwa kuwashusha majukwaani. Lakini ole wao wakifanya hivyo safari hii kwani kama nyuma walipambana na mvua za rasha rasha, safari hii watapambana na dhoruba - yaani nguvu ya wananchi waliochoka kunyanyaswa na kuibiwa. Hii ni kwa sababu mwishowe amejitokeza kiongozi jasiri asiyeyumbishwa na asiyetetereka.

Kujua mtazamo wa yule unayetaka kuchuana naye ni jambo jema. ninachosisitiza hapa ni kuwa realistic na siasa za Tanzania. siasa za Tanzania zimejaa ushabiki mwingi bila vitendo, na ndicho ninachokiona hata hapa JF. vinginevyo tukiamua sote kwa Vitendo Mabadiliko ni lazima.
 
Hongera kwa Mheshimiwa Slaa. Mimi siyo mshabiki wa Chadema wala chama chochote cha upinzani ila itikadi za kichama pembeni natambua umhimuwa huyu mzee. Najua fika kwamba akifanya vizuri katika uchaguzi huu hata kama siyo kushinda basi ata leta matumaini mapya na mazingira ya kisiasa Tanzania yana weza yaka badilika ghafla bin vuu. Nasema tena hongera mheshimiwa Slaa na nakutakia kila la heri kwenye uchaguzi. Mabegani mwako hauja beba matumaini ya Chadema tu bali wapenda maendeleo na mabadiliko wote wa Tanzania. 2010 just got interesting.
 
Daaa, hiii kweli ni goood newwwwwwz!!

Mpka sasa Dr. nakuhakikishia kura 15 za chap chap, 5, toka mji wangu, 10 toka kwa ndugu na jamaa nilio ongea nao ana kwa ana!
Muujiza waweza tendeka, Go Dr. go.. tuko nyuma yako tunasue kwenye makucha ya mafisadi!
 
Kura yangu ni kwa Dr Slaa. Nimeshaanza kampeni ya kutuma sms kwa watu wote walio katika simu zangu wapatao mia tano nikiwahamasisha wamchague huyu ndiye kama tumaini letu jipya Tanzania.

Nitaendelea kumpigia kampeni wakati wa uchaguzi mkuu wakati na mimi nitakuwa kilingeni kugombea............... Safari hii haiibiwi kura ya mtu. Msitishike ni uongo na wakae sawa. Yeyote, narudia Yeyote hata kama ni wakala wa Chadema atajaribu kucheza mchezo huu safari hii ataona cha mtema kuni. Natoa onyo mapemaaaaaaaaaaaaaaaaa.

Slaaaaaaaaaa oyeeeeeeeeeeeeee. na Mungu atabaki upande wa haki daima.
 
naona mkuu itabidi akanushe usemi wake kwamba azihitaji kura za wafanyakazi.
 
Wakoritho endelee kujipa moyo tu, lakini nina habari mbaya kwenu njii hii kamwe haitatawaliwa na Padri
Huko unakotaka kuelekea ndiko kutamu na CCM walio welevu hawataki hata kupagusia maana ni moto kote kote.
 
Thanks be to God. Nimefarijika sana kupata habari hizi. Kuna siku Dr. Slaa alinishauri hapa JF nisiwe nakata tamaa. Sasa nimemwelewa.

(1)Slaa kugombea Urais kutaongeza sana idadi ya wabunge wa Chadema kwani kutaongeza umaarufu wa Chadema kwa ujumla.

(2) Kuna uwezekano mzuri wa kupata AWAMU ya pili. Tumekuwa na awamu ya chama kimoja kwa miaka 50. Chadema kushika usukani ndiyo itakuwa awamu ya pili.

(3) Kikwete is very beatable. CCM is beatable. Ni kama KANU na UNIP zilivyoshindwa kwenye uchaguzi. Watanzania sio wajinga. Wanajua tumetawaliwa na hawa "wenzetu" kwa miaka 50 bila kupata maendeleo. Watataka kuanza awamu ya pili ya miaka 50 na chama tawala kingine.

(4) Wako vigogo wa CCM watakaojiunga na Chadema kutokana na kunyimwa kugombea ubunge. Watakuwa ni wapiga debe wazuri wa Chadema.

Ningekuwa Tanzania ningepiga kura (for the first time in my life). Hata hivyo, nitawaandikia ndugu na marafiki zangu wote (kama watu 20) kuwasihi wampigie kura Dr Slaa na waunge mkono Chadema.
 
Congratulations Dr. Slaa, we have been waiting for a credible candidate for a while. Now what you need is a strong message to counter Kikwete and his ineffectiveness in the last 5 years in addition to you promise to relieve Tanzanians of a heavy economic burden that has continued to leave them poor under CCM reign!
 
we ndugu wewe. Huwezi ukaomba kufanya UE wa physics wakati wewe ni ngwine per se. Hiki ndiyo kimetokea hapa. Kumbuka kuwa hata wanaomchekea Slaa usije ukadhani wote wanamfurahia. In fact wengi wanamcheka.
Naona wewe ungekuwa kocha wa Ghana ungewaambia wasishiriki kombe la dunia maana uwezekano wa wao kushinda ni mdogo, lakini tumeona matokeo yake walifika robo fainali.
Pili tulitegemea Brazili, Argentina, Ujerumani, uingereza kufanya vizuri, lakini matokeo yake sote tunayajua, labda kama wewe huyajui, au huyatambui.
 
Nani aliyekwambia mwaka huu kutakuwa na idadi kubwa ya wabunge wa Chadema ku-warrant kuteuliwa wengi? Wabunge wa kuteuliwa hawaiingii tu bungeni kwa miguu au kwa ku-drive. Kuna mchakato wake. Let us be realistic kwa level ya JF.

Je kuna aliye kwambia kwamba wengi wa ccm watashinda? labda kama wewe umekuwa Sheikh Yahya
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom