Sijakuelewa Nyambala. Unataka wale waliopo nje ya nchi wasikae?
Slaa anakubalika kwa karibu Watanzania wote walioko nje, na wale walio nyumbani pia. Utawala wa JK ndio unafanya Watanzania wengine wasiwe hata na shauku ya kurudi nyumbani.
Unataka tufanye nini? Jieleze.
Sijapiga kijijini, nimempigia kada nguli wa CCM kujua mtazamo wake.
Ukiweka ushabiki wa JF bila kuwa realistic na hali halisi haitusaidii kuleta mabadiliko ya kweli. Katika post yangu moja nimetoa angalizo kuhusu kuwa na Mawakala waaminifu, Nalijua hili na ndio mtaji mkubwa wa ushindi wa CCM, eneo lingine ni Vijijini ambako elimu ya mageuzi bado iko chini na vyama vyetu vingi havina network huko, sasa haya ndiyo tuyafanyie kazi kama tunataka ushindi, vinginevyo tutaishia kushabikia humu JF huku mkulima kule mwanarumango hajui kinachoendelea wala maana ya mageuzi
So pessimistic, we do not necessarily want to have people like you when we campaign for change. Nobody ever thought kwamba America would have a Black president in the name of Obama. We have him today against all odds.Well - nilikuwa bado na "hang-over" ya JackD lakini sasa najisikia nafuu
This might not necessarily mean kuwa Dr Slaa atakuwa the next President But at least some voters have got "a person" to vote for kwenye presidential position.
Kwa mtazamo wangu, Dr Slaa angegombea ubunge wa jimbo la Karatu, unless kwa sasa hakubaliki tena huko. Kama walikuwa na lengo la kumteua agombee urais basi yangekuwa ni maandalizi ya 2015 rather than now (hata Mbowe mwenyewe angekuwa na nafasi nzuri pia). Hii inaweza kuwa habari njema kwa CCM, kwani wanaweza kuweka nguvu kwenye jimbo hilo wakalichukua kirahisi sana. Naamini Dr Slaa ataiweza nafasi ya urais vilivyo, lakini hofu yangu ni kuwa chances za yeye kuitwaa kofia ya urais ni very slim.
Kwa kifupi, sitamani Dr Slaa agombee urais naona dalili za yeye kukosa vyote, hivyo tukakosa kiungo muhimu sana bungeni....
Hii ni habari njema kwa watu wote kila nikiwaza utawala wa Kikwete nazidi kukosa matumaini ..............