Elections 2010 Dr. Slaa TV & Radio Ad - First Take

Kuna tatizo la audio maana kuna mikwaruzo mingi..., sauti ya shujaa inabidi itoke 'loud and clear' hiyo peke yake ni ujumbe tosha kwamba tuna uhakika na tunachohubili (bila kuumauma maneno). Vilevile picha ya Chenge akielekea mahakamani kwenye kesi yake ya makosa ya barabarani sioni kama ni relevant, Yakilekebishwa hayo inaweza kuwa bonge la campaign Ad, great idea..!
 
Nimefurahia mapendekezo ya wadau mbalimbali.. tatizo tulilonalo ni lile lile.. we have to work with what we got online.. ila kuna watu mapro- wanafanyia kazi the real deal... so natumaini wakikamilisha kutakuwa na matangazo mazuri tu. Tungekuwa na clips nzuri na za uhakika we could have used those.. lakini mbuzi hula kamba inapofika.
 
Huyu mzee ameshashinda... :eyeroll2:

Kwa bahati mbaya kwa wengine hajashinda na hawatapenda ashinde kutokana na hoja na uzalendo wake aliounesha Bungeni kitaifa na jimboni kwake so far... sababu tu mgombea mwenza wataja yu' darasa la saba!!

Says a lot for some whom their nationalistic interests are based on association... na kupiga kura ni kwa kujuana pia!!
 
Mmmh Mwanakijiji.
Hapa umemaliza, CHADEMA wangepata TV ya kuweka hii ad si ajabu Makamba angepatwa na pepofisi na si pepopunda.
 
Wanajamii Dr. Slaa ametuomba tusambaze hii mp3

View attachment 13557
41784_148053981881068_35_q.jpg

Mnaweza kurekodi hii kwa simu zenu na kuwapatia rafiki zenu au kutuma kwa simu. Asante MM kwa jitihada zako: http://www.box.net/shared/ln73fxu780

wote walio kwenye contacts zangu kwenye simu (241) nimewatumia kasheshe wengine ni makada wa CCM wanarudisha dhihaka kwangu ila ujumbe wameupata
 
Nawauliza Chadema vipi mutaleta mabadiliko Tanzania ikiwa mumesimamisha wagombea wa ubunge wasiozidi mia moja ?
wakati wabunge wote wa tanzania wanazidi 250 ?
Mageuzi hayo ni ukulu tu kuna bishara gani Ikulu ?
ningemshauri DR Slaa kuwapigia kampeni wagombea wengine wa upinzani kampeni kwenye majimbo anayotembelea ambayo CHADEMA hawakusimamisha wabunge hapa nitamuona Slaa kweli anataka mageuzi ya Kweli.
 
.

Tunaziiita hizi ni Pumba! Hujui hata idadi ya wabunge! Headless chick
 
Nawauliza Chadema vipi mutaleta mabadiliko Tanzania ikiwa mumesimamisha wagombea wa ubunge wasiozidi mia moja ?
wakati wabunge wote wa tanzania wanazidi 250 ?
Mageuzi hayo ni ukulu tu kuna bishara gani Ikulu ?
ningemshauri DR Slaa kuwapigia kampeni wagombea wengine wa upinzani kampeni kwenye majimbo anayotembelea ambayo CHADEMA hawakusimamisha wabunge hapa nitamuona Slaa kweli anataka mageuzi ya Kweli.

Mlekwa inaonekana ndugu yangu hujui siasa vizuri nina mashaka.. unapoondoa wingi wa wabunge wa CCM (kuondoa zaidi ya theluthi mbili) manake ni kuwa hakuna bajeti, mswada wa sheria ambayo yatapitwa bila kuhusisha majadiliano na wapinzani.. kwa kufanya hivyo CCM haitoweza tena kufanya ipendalo.
 
Nawauliza Chadema vipi mutaleta mabadiliko Tanzania ikiwa mumesimamisha wagombea wa ubunge wasiozidi mia moja ?
wakati wabunge wote wa tanzania wanazidi 250 ?
Mageuzi hayo ni ukulu tu kuna bishara gani Ikulu ?
ningemshauri DR Slaa kuwapigia kampeni wagombea wengine wa upinzani kampeni kwenye majimbo anayotembelea ambayo CHADEMA hawakusimamisha wabunge hapa nitamuona Slaa kweli anataka mageuzi ya Kweli.
wewe nani amekutuma? kwa taarifa yako chadema imesimamisha wagombea ubunge 172, na wengine waliowekewa mapingamizi na ccm tume imewaruhusu waendelee mfano nyamagana, kwa hiyo chadema ina wagombea at least 172, katika bunge lilopita kulikuwa na majimbo ya uchaguzi 232, kwa hiyo baada ya tume kuongeza majimbo 7 mwaka huu, hivyo jumla ya majimbo ni 239, sasa ukichukua 172 kwa 239 utaona kwamba angalau imesimamisha wagombea ubunge kwa asilimia 72. hata hivo hiyo imechangiwa na hujuma zilizofanywa na wasimamizi majimboni ya kuwanyima fomu wagombea wa chadema na mara nyingine kuwaengua bila sababu za msingi, pia imechangiwa na ccm kuwarubuni baadhi ya wagombea kwa rushwa kama kule musoma vijijini kwa nimrod mkono pamoja na singida(kaskazini?). Vipi upo hapo
 
Mmmh Mwanakijiji.
Hapa umemaliza, CHADEMA wangepata TV ya kuweka hii ad si ajabu Makamba angepatwa na pepofisi na si pepopunda.

chadema wangekuwa wanalipa kama CCM we could make some real stuff for them.. lakini ndiyo hivyo tena ukata...
 
wewe nani amekutuma? kwa taarifa yako chadema imesimamisha wagombea ubunge 172, na wengine waliowekewa mapingamizi na ccm tume imewaruhusu waendelee mfano nyamagana, kwa hiyo chadema ina wagombea at least 172, katika bunge lilopita kulikuwa na majimbo ya uchaguzi 232, kwa hiyo baada ya tume kuongeza majimbo 7 mwaka huu, hivyo jumla ya majimbo ni 239, sasa ukichukua 172 kwa 239 utaona kwamba angalau imesimamisha wagombea ubunge kwa asilimia 72. hata hivo hiyo imechangiwa na hujuma zilizofanywa na wasimamizi majimboni ya kuwanyima fomu wagombea wa chadema na mara nyingine kuwaengua bila sababu za msingi, pia imechangiwa na ccm kuwarubuni baadhi ya wagombea kwa rushwa kama kule musoma vijijini kwa nimrod mkono pamoja na singida(kaskazini?). Vipi upo hapo

kwa kuongezea majimbo mengine 50 ni ya Zanzibar ambayo kuna vyama vilikwisha jigawia kwa misingi wanayojua wao wenyewe. na mengine ya bara kwa mizengwe ya CCM kuogopa upinzani wapite bila kupingwa
 
Nimefurahia mapendekezo ya wadau mbalimbali.. tatizo tulilonalo ni lile lile.. we have to work with what we got online.. ila kuna watu mapro- wanafanyia kazi the real deal... so natumaini wakikamilisha kutakuwa na matangazo mazuri tu. Tungekuwa na clips nzuri na za uhakika we could have used those.. lakini mbuzi hula kamba inapofika.
Kazi nzuri MMJ, hata kama kamba yako ni fupi lakini ulifanyalo linaonekana na ni uzalendo ulitukuka. Kila mtu akifanya lililo ktk uwezo wake hakika hakuna litakaloshindikana hata ije dhoruba ya aina gani. Thanx mkuu
 
Ila sasa CCM nao wakija na posho ya kazi ngumu na kutaka tuwatengenezee clip bora zaidi inakuwaje....? Au ndio itakuwa kupokea fedha za "kifisadi" hata kama ni za halali?
 
Nimefurahia mapendekezo ya wadau mbalimbali.. tatizo tulilonalo ni lile lile.. we have to work with what we got online.. ila kuna watu mapro- wanafanyia kazi the real deal... so natumaini wakikamilisha kutakuwa na matangazo mazuri tu. Tungekuwa na clips nzuri na za uhakika we could have used those.. lakini mbuzi hula kamba inapofika.
Vile vile ni vema picha zitakazo onyeshwa ziwe zile za kuonyesha hali halisi ya umasikini uliopo sasa. Nyumba mbovu za walimu,wanafunzi wanaokaa chini wakisoma, hali ya mahospitalini kulala chini au wagonjwa watatu kitanda kimoja,uozo wa mabehewa TRL nk ili kuwaonyesha watanzania tofauti ya maisha yao na yale kama ya majengo wanaojengewa vigogo wa BOT, magari ya kifahari ya viongozi na vitu kama hivyo.
 
Nimefurahia mapendekezo ya wadau mbalimbali.. tatizo tulilonalo ni lile lile.. we have to work with what we got online.. ila kuna watu mapro- wanafanyia kazi the real deal... so natumaini wakikamilisha kutakuwa na matangazo mazuri tu. Tungekuwa na clips nzuri na za uhakika we could have used those.. lakini mbuzi hula kamba inapofika.

Nampa heko aliyetengenezai. Ila ninavyoona inabidi muweke nguvu zaidi. Tumieni videos za campaign na sio file pictures tu. Pamoja na hayo campaign ad iwe na baadhi ya sera zinazovutia za chama - sio tu kuwa'attack CCM. It just needs to be short, 30 secs is more than enough, and much cheaper than a 2 minute video.

Tazama Docu ya Makamba muone. Au tazama

Let us think big:

Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom