Mkuu hapa tunazungumzia wanachama wa TAA kabla ya kuanzishwa TANU i.e before 1954. Rashidi Kawawa alikuja kujitokeza baadae kabisa kutoka kwenye vyama vya wafanyakazi, wala sishangai FireFOX anacho zungumza hapa - nakumbuka nilipo kuwa mtoto mdogo Bibi yangu mzaa Baba ambaye alikuwa ni MKATOLOKI aliwahi kuniambia kwamba ma Padri wa kizungu walikuwa wanawatisha wasijiunge na vyama/vikundi vinavyo pingana na utawala wa kikoloni? Walikwenda mbali zaidi kwa kuwatishia kwamba Wa Komunisiti ni mashetani, watu wa vijijini na elimu yao duni waliamini kwamba Ukomunisiti na (Prince of Darkness) i.e Lucifer walikuwa kitu kimoja, hata mimi niliamini hivyo hivyo!! Swali ni: Kwa nini baadhi ya Mapadri wa kizungu badala ya kueneza neno la BWANA walieneza vitisho kwa waumini wao kama mbinu za kutaka kuchelewesha ukombozi wa taifa letu?