Kwa wanaopenda kusikiliza na kuyajadili mafundisho ya kikristo ya huyu mwalimu tukutane hapa. Mimi si mtu wa kuvutwa au kukubaliana kirahisi na hawa walimu wa biblia wa siku hizi ila kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa nimesikiliza mafundisho na vipindi vyake vya maswali na majibu huko YouTube na Facebook na nakiri ni mafundisho na hoja zinazofikirisha. Nimepita kwenye shule nyingi na mirengo tofauti ya kitheolojia na ningependa wale wote wenye ujuzi katika maandiko na hata wale waumini wa kawaida tu ambao wameisoma biblia na kubaki tu katika kutatizwa na fasiri walizopewa na viongozi wa makanisa basi tumsikilize Dr. Mwalusambo na Kama kuna hoja kinzani (refutation) au kuna uungaji mkono basi tuyalete yote hapa.