DRAFT ONLINE: Sisco vs Mkulima

Ronaldo nae Yuko vizuri na hii mechi kutokana na fittnes yake katoka kumpiga Noel 3 bila wat walijua anaenda kushinda,hii mechi wat wamepandia Hadi milioni, ila yule dogo sio mtu kabisa akiitaka mechi,kwa Sasa kwa nchi hii hakuna anaeweza kukalia nae benchi
 
Kuna Mzee pia anaitwa Mzee Rama wa Kilimanjaro, huyo pekee ndio alitoa sare 2 na Msomali

Sasahv Msomali yupo hapo Dar, ila anasubiriwa Arusha fainali Julai hii hii

Ila Mzee anajua sanaa
Wachezaji wa mikoani ambao wako vizuri kwa Sasa ni kili tanga na msomali.
Sisco alikua na ziara tanga majuz apa wachezaji wote wakubwa wa tanga kapiga 7.
yule mtoto ana matatzo kwa Sasa.
 
Wachezaji wa mikoani ambao wako vizuri kwa Sasa ni kili tanga na msomali.
Sisco alikua na ziara tanga majuz apa wachezaji wote wakubwa wa tanga kapiga 7.
yule mtoto ana matatzo kwa Sasa.
Sasa mbona sisco anapigwa na mkulima, tena sisco anaambiwa atafute sare, kama mkulima anatumia software, ni software gani inacheza draft kubwa (Tanzania rules) kama la mkulima? ilala yetu
 
Sasa mbona sisco anapigwa na mkulima, tena sisco anaambiwa atafute sare, kama mkulima anatumia software, ni software gani inacheza draft kubwa (Tanzania rules) kama la mkulima? ilala yetu
Huyo mkulima hajawai kuonekana Wala hataki kuonekana,Sasa hatuwezi kuzungumzia watu wasioonekana haijulikani ni binadamu au mzimu.
 
aonekane asionekane mimi ni shabiki wa mkulima namba moja

kaka mm nlipitia game za mkulima karibhni zote asee kibinaadam kwel mtu huwezi kosea hata kidogo? game alizofungwa mkulima ni either muda au ameamua kuswitch side kwaiyo atajiloozisha.
amefungwa game moja tu kihalali katika loose zote zile unazoziona apart from akichezaga chineese,,tena iyo game kafungwa na david mbeya ukipata muda kama bado ipo kaipitie..

Ndio maana umu nlishawai sema huu mkataba wa sare akipewa cr7 na mkulima atabeba ela cr7,, kwasababu cr7 kule anajiita ashkelon na ndo alisema hii ni program.. kwaiyo ukicheza nae usiishambulie cheza nayo kawaida..

nlisema umu baada ya wiki akapewa mkataba na mkulima akatoa sare nae ila kumfunga mkulima ni ngumu mno..
sisco kumfunga mkulima ni ngumu sisco anakushambulia tu na kukuvizia.

Sisco kwa sasa ni Beast wa draft TZ anamazoezi sanaaa kama kalipitie goli lake la tege kwa cr7 utaamini adi cr7 akashangaa.

namkubali mkulima ila bro game zaidi ya 1000 ufungwe 1 tuu atakukosea bahati mbaya?
 
Ningekuwa na hela ningedhamini Gemu ya Ronaldo na mkulima irudiwe, sharti michezo 24, cr7 apate sare au ashinde basi fresh
 
ndio maana hataki kujulikana kwa sababu anajua sanaa

Program gani anatumia isiyofungwa na watu wote hao aliocheza nao
 
cr7 anatoa droo bro anamjua.. unless kama mkulima kaja na version mpya apo itakua balaa
Nimekuwa nikifatilia gemu za mkulima, nimegundua mkulima hanaga copy, na harudiagi michezo, yani mfano leo akicheza aina hii ya kavimba kesho atacheza aina ingine kabisa ya kavimba, yani anaweza anza kete yoyote na kujibu kutumia kete yoyote, mkulima anaweka kete ambayo hujawahi chezewa, na ukikosea anakupiga na finishing kali, kina cr7 na sisco wanafungwa sababu wanapoteana, kina sisco wamekariri copy, sasa mkulima anaenda na mguu tofauti, ukijichanganya anakufunga, ukicheza vizuri mkulima anatoa sare ya nguvu basi fresh Ganja ni dawa
 
Msomali anakuja Sana manyanya pale hata mechi na Sisco hawez omba Wala kupangiwa..sio uzani wake,,...huyo anahangaishana na kina Ally white wachezaji uzani flani wa katkat ao wa mabao
Mimi huyo Msomali namfunga Huku nimefumba macho na hata sare hapati.
 

kaka kama umecheza draft no dought kukariri ni muhimu mnoo na uwezo ni muhimu

kwa ulowaona ivi kuna mtu anapiga draft la akili kama mzee noel? ila anapoteana coz hali copy mpya mara nying
sisco anacheza draft kabisa unaona ili amelikariri na ndo kinamsave mnoo anacheza anacheka cheka njonjo kibao
 
RATIBA RASMI YA MASHINDANO YA DRAFTI KITAIFA IMESHATOKA.
YATAANZA RASMI TAREHE 30 AGOSTI 2023 HADI 01 SEPTEMBA 2023.

MASHINDANO YA KUMTAFUTA BINGWA WA DRAFT TANZANIA 2023



WASHIRIKI

KUNDI A
Sisco
Gaby
Monster
Dogo shuku
Ngapulila

KUNDI B
Dilima
Digi Digi
Aradini
Dogo yassin
Matongo

KUNDI C
Noel
Mwasapile
Mbeya city
Dogo janja
Mawazo

KUNDI D
Mamba
Keny hisabati
Nungwi
Gaidi
Hemed Arusha

KUNDI E
Rama Arusha
Dany Mbeya
Dogo Athuman
Kwata mwivi
Lissu

KUNDI F
kiwembe
Stive Mbeya
Dogo Hans
Rama singida
Dogo Ally

KUNDI G
Simba Dom
Shaban Mbeya
John kipaji
Kili mnyama
Zaidi

KUNDI H
Nduli
Babu songea
Amani Siri
Hussein tanga
Kavimba

16 BORA
A1 vs E2
D1 vs. H2
B1 vs. F2
C1 vs G2
E1 vs A2
H1 vs D2
F1 vs B2
G1 vs C2

Robo fainali
Mshindi 1 vs 2
Mshindi 3 vs 4
Mshindi 5 vs 6
Mshindi 7 vs 8

Nusu fainali
R1 vs R2
R3 vs R4

Mshindi wa 3
Fainali

Zawadi
1. 2,000,000/=
2. 1,000,000
3. 500,000





MATANGAZO ( Watarusha wenyeji wa Mbeya )


WARATIBU
1. Adamu wa Goba
2. Dullah Mabao
3. Zaidi
4. Mtemi
5. Eng kitova
6. Mohamed Ismail
7. Paul Jackson



SHERIA ZA MASHINDANO KUMTAFUTA BINGWA WA DRAFT TANZANIA 2023.

1. Kufikiria sekunde 60 + Kumi za kuesabu baada ya hapo kamisaa atavuruga bao na kumpa mpinzani ushindi

2. Ikitokea umeshangilia hadi bao kuvurugika basi kamisaa atamkabidhi ushindi mpinzani wako.

3. Mchezo ukishaanza lazima uishe kwanza ndo ruhusa ya kwenda chooni itatolewa.

4. Hairuhusiwi kutumia simu wakati mchezo unaendelea.

5.Mwenye kingi moja anamamlaka ya kumvalisha mwenye kete tatu popote pale.

6. Mchezo au steps zitakazojirudia rudia mfano tatu gomea nk basi yule anayetafuta kushinda atapewa dakika tano tu endao ile kete ikishatoka step moja basi mchezo utaendelea kama kawaida.

7. Mfumo wa uchezaji kwenye Hatua ya Mtoano ( yaani 16 ) itapigwa Omary John Mshindi akipatikana mchezo umeisha, ila kama hawajafungana watacheza tege mbili ( 2 ) za muda wa kawaida nazo zikiisha sare, ndipo zitapigwa tege nne ( 4 ) goli la dhahabu mtu atakapofungwa mchezo utakuwa umeisha lakini endapo nazo zitaisha bila mshindi kupatikana sasa wataongezewa tege kwa goli la dhahabu huku wakipunguziwa muda kwa sekunde kumi tu hadi mmoja afe.


8. Kwenye Makundi endapo wachezaji watafanana points
Vitaangaliwa vigezo cmvifuatavyo
1. Tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa
2. kigezo cha matokeo yao walipokutana ( Head to Head )
3. Idadi ya magoli ya kufunga mwenye mengi ataenda
4. Kama kote huko wamefanana basi italazimika mechi ichezwe tena kati ya hao waliofanana.

9. Kitendo /vitendo vitakavyoashiria ushirikina haviruhusiwi katika mashindano na endapo mchezaji atabainika kujihusisha navyo na kamati ikijiridhisha anaweza kuondolewa katika mashindano.

10. Mchezaji hataruhusiwa kuwekea kete kivuli au kuashiria kucheza kete fulani, hesabu zote zipigwe nje ya uwanja, endapo kamisaa atajiridhisha kwamba imejengewa kivuli atakiwa kuicheza kete hiyo.

11. Endapo Mchezaji akichelewa kwa zaidi ya muda uliopangwa kamati itawasubiri kwa muda wa nusu tu, baada ya hapo atakuwa amejiondoa mwenyewe kwenye mashindano mpinzani wake ataendelea round inayofuata.




MFUMO WA UCHEZAJI
( hatua ya makundi )

Kwenye mzunguko kutakuwa na makundi manane (8) na wanatakiwa kupita wachezaji wawili (2) kila kundi,,

Katika kila kundi wachezaji watakutana wote yaani kila mchezaji atacheza na kila mchezaji mwenzake kwenye kundi lake,,


Kwenye Makundi michezo ni minne tu Yaani miwili kawaida na miwili tege.



Hatua ya Mtoano Zitapigwa Omary John kwa kufuata sheria namba 7 hapo juu


Wachezaji wa mikoani wafike MBEYA CHUNYA siku moja kabla ya mashindano yaani tarehe 29.8.2023

Ligi Itaanza Rasmi Siku ya juma Tano tarehe 30/08/2023, hadi 1/09/2023Mwezi wa tisa , Saa mbili kamili Asubuhi kwenye CLUB ya chunya (chunya arena) , na Siku ya kwanza kutakuwa na ufunguzi wa mashindano ambapo Tunatazamia kuwa na mgeni rasmi (............. ) Atafungua mashindano rasmi.πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…