mshale21
JF-Expert Member
- Apr 8, 2021
- 2,126
- 5,068
Habarini wanabodi JF!
Nikionacho Mimi, Hii drama ya mtu na shemeji yake Ni mbinu ya CCM kuwapoteza CHADEMA na wafuasi wake kuhusu sakata la Mbowe na Katiba Mpya!
Ikumbukwe kuwa baada tu ya kushikiliwa kwa M/kiti wa CHADEMA. Mh. Mbowe, ndoto ya sakata la Katiba Mpya ikafia hapo, nguvu zote zikaelekezwa katika namna ya kumnasua Mbowe katika kesi ya Ugaidi inayomkabili!
Wakati hayo yakiendelea, huku wanaharakati na watetezi wa haki za Binadamu wakielezea masikitiko yao juu ya mwenendo wa kesi ya M/kiti Mbowe huku wakipaza sauti kuwa Haki itendeke kwa m/kiti huyo, ghafla linatokea sakata la Dr. Gwajima VS Pst. Gwajima !
Sakata hili limeonekana kuzua gumzo nchini, huku likiteka fikra za Wafuasi , wanachama na Viongozi wa CHADEMA , ambao Sasa wamejisahau kuwa Kuna suala la Katiba Mpya na kesi ya m/kiti wao bila kujua Ni mtego uliotegwa nao wamenasa katika mtego huo!
Umewahi kuona ugomvi wa mtu na shemeji yake katika maswala yaliyo nje ya mambo ya kifamilia?
Umewahi kujiuliza chama kinampa onyo mwanachama wake lakini bado anakaidi maelekezo?
Katika maswali hayo Kuna uwalakini!
Muda ni Msema kweli, mtaurejea uzi huu!
Wito Wangu!
CHADEMA Kama kweli mmeamua kudai katiba mpya, fanyeni hivyo.
Na Kama kweli mmeamua kumtetea m/kiti wenu fanyeni hivyo pia!
Tofauti na hapo, mtademshwa na upepo wa matukio ya kisiasa mtakuja kukumbuka , saa mbovu,!!