Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Vita vya muda mrefu na ukosefu wa amani mashariki mwa Congo(DRC) nyakati hizi kwa kiasi kikubwa vinachangiwa na udhaifu wa dola ya DRC kudhibiti nchi pamoja biashara ya madini adimu mbalilmbali yenye mahitaji makubwa duniani kwa sasa. Baada ya Waafrika wenyewe kuushindwa huo mgogoro bila shaka mwenye uvumbuzi wa haya matatizo aliyebaki ni "beberu" Marekani na wenzake wa Ulaya kwa sababu wao ndio wanaoshikilia mpini wa mfumo wa fedha ulimwenguni kwa sasa na ndio wenye uwezo ya kumdhibiti jirani au majirani wanaodaiwa kujinufaisha pia na huo mgogoro.
DRC iwaangukie hawa mabeberu kuiponya nchi yao. SADC, EAC na AU watulie tu wasitoe milio ya kuingiliwa na mabeberu wazee wa kazi watakapoingia mzigoni, zaidi wawape ushirikiano mkamilifu. Pia Wazalendo uchwara waache kelele za kusema West ndio wanawapa silaha waasi kwa sababu ni kuwavunjia heshima "mabeberu" wenye ufunguo wa mgogoro wakati hata hizo tuhuma zenyewe zinaweza kuwa sio za kweli au hazithibitishiki.
Wanachohitaji mabeberu ni sabubu nzito za maslahi ili kuhusika kikamilifu kuumaliza huo mgogoro. DRC wao watalipia gharama kwa kuwapa mabeberu mikataba exclusive na minono ya miaka 30 ya madini adimu na muhimu, faida igawanywe pasu kwa pasu 50/50 kati ya Congo na Mabeberu.