The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inawasilisha muswada kwa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kutaka uchunguzi ufanywe katika kile inachokiita ni ukiukaji mkubwa wa haki katika mji wa Goma.
Balozi wa Congo katika baraza hilo Paul Empole Losoko Efambe aliwaambia waandishi habari kwamba kutokana na ukiukaji huo wa haki za binadamu wanahitaji mtu katika mfumo wa Umoja wa Mataifa achunguze hali hiyo.
Muswada huo unaotaka kuundwe tume maalumu ya uchunguzi na kukusanya taarifa na ushahidi utawasilishwa katika kikao cha dharura cha baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva.
Mzozo wa vita nchini Congo unaendelea huku Umoja wa Mataifa ukitoa miito ya amani. Kundi la waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wameendelea kusonga mbele katika eneo la mashariki mwa Congo na walionekana wakijiandaa kuuteka mji muhimu wa kimkakati, wakati katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akitaka pawepo amani.
Akizungumza katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Guterres amesema ni wakati wa kuufikisha mwisho mgogoro huo.