DRC yaanza kutoa chanjo ya Ebola baada ya wawili kufariki, 230 wakiambukizwa

DRC yaanza kutoa chanjo ya Ebola baada ya wawili kufariki, 230 wakiambukizwa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mama na mtoto.jpg

Mama aliye kwenye matibabu akitenganishwa na mtoto wake kutokana na kupata maambukizi ya Ebola

Dozi 200 za chanjo ya Ebola zimepelekwa Nchini DR Congo na nyingine zinatarajiwa kupelekwa katika siku zijazo baada ya watu wawili kuripotiwa kufariki kwa ugonjwa huo.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa ripoti hiyo baad aya vifo vya watu hao katika Mji wa Mbandaka wenye wakazi zaidi ya milioni moja ambako watu wanaishi karibu na barabara, maji na njia za anga kuelekea katika Mji Mkuu Kinshasa.

Wataalam wa chanjo wapo eneo la tukio wanaendelea kuchanja ambao wameshaambukizwa, takwimu zikidai idadi ya walioambukizwa ni 230.

Huu ni mlipuko wa 14 wa Ebola kwa jumla Nchini DR Congo tangu ilipotokea kwa mara ya kwanza mwaka 1976, pia imetokea mara sita tangu mwaka 2018.

Chanzo: UN
 
Hivi ndio ule ugonjwa alioufanyia utafiti yule Dr, (RIP)
 
Back
Top Bottom