Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imepiga marufuku vyombo vya habari nchini humo kuripoti kuhusu shughuli za aliyekuwa Rais, Joseph Kabila, pamoja na kufanya mahojiano na wanachama wa chama chake cha siasa. Amri hii inajiri wakati kukiwa na mvutano mkubwa wa kisiasa kati ya Bw. Kabila na mrithi wake, Rais Félix Tshisekedi.
Mamlaka ya udhibiti wa vyombo vya habari nchini humo (CSAC), kupitia kwa mkuu wake, Christian Bosembe, imetangaza kuwa chombo chochote cha habari kitakachokiuka agizo hili kitakabiliwa na adhabu ya kusitishiwa shughuli zake.
Hatua hii imechukuliwa kufuatia kurejea kwa Bw. Kabila nchini humo mwezi uliopita, hali iliyozidisha wasiwasi wa kisiasa uliokuwepo. Serikali ya sasa inashinikiza kumfungulia mashtaka Bw. Kabila kwa tuhuma za uhaini na madai ya kuwa na uhusiano na kundi la waasi la M23, ambalo limekuwa likipambana na jeshi la serikali mashariki mwa nchi. Hata hivyo, Bw. Kabila amekanusha madai hayo hapo awali.
Mvutano kati ya pande hizi mbili umekuwa ukiongezeka tangu Rais Tshisekedi aingie madarakani, na kuvunja muungano wa kisiasa uliokuwepo baina yao. Serikali ya Tshisekedi imekuwa ikimshutumu Kabila kwa kujaribu kuyumbisha utawala wake, huku upande wa Kabila ukidai kuwa serikali ya sasa inakandamiza demokrasia na haki za binadamu.
Marufuku hii ya habari imezua gumzo miongoni mwa wanahabari na watetezi wa haki za binadamu, wanaoiona kama njama ya kunyamazisha sauti za upinzani na kuminya uhuru wa habari nchini humo. Wanaeleza kuwa hatua hii inarudisha nyuma maendeleo ya kidemokrasia ambayo taifa hilo limekuwa likijitahidi kuyafikia.