Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Vilevile wengi zinawafanya waonekane wako rough yaani sio smartHabarini wakuu,
Nimewakumbuka,
Kwanza nafaurahi kurudi JF baada ya muda,
Twende kwenye mada tajwa hapo juu, ni ukweli kwamba dread locks ni nywele nzuri hasa kwa wanaojua kuzitunza na zinawapendeza.
Lakini dread locks sio kila mtu zinampendeza zinachagua uzuri wa sura, yani kuna wadada wako kama vikongwe kisa tu dread locks, sura zimewakomaa.
Ni vizuri kujijua kuwa unapendeza na aina gani ya nywele, kwenda na wakati huku wanashindwa kuangalia sura zao, hiihupelekea kupoteza muonekano.
Mwisho dread locks ni nywele nzuri ila sio kila mtu zinampendeza
[emoji2960][emoji119][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]khaaa eti komwe linawambwaDread locks zinaongeza komwe jamani [emoji1787][emoji1787]
Wakitokaga kuzitreat komwe linawamba kinyamaaa.
Sasa ukute una nywele chache mbele, ndiyo huko kuzeeka mtoa mada anakosemea.
KhaaaNi ukweli usiona Shaka nilikaa na dread miaka kumi na mbili nimenyoa sasa kwakweli najiona nimerudi ujana [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] sijui nilizipendea nini [emoji19][emoji19][emoji19][emoji19]
Mmh acha niendelee na nywele zangu tu[emoji1787]Au ukute kaweka dread kwenye uso wenye paji la uso pana [emoji1787][emoji1787]
Akitoka kuzitengeneza ni ka msala hapo usoni
[emoji2960][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Tuwekee picha tuone
Ila nahisi zinawauma Atari Mana Kuna demu wangu siku moja nilimpa hela akaenda kusuka usiku tumelala akamka akaanza zikuna nakuuliza Veep akasema zinauma akazimwagia maji lkn wapi baadae akaanza Lia akasema nimfumue daa nilizikatakata vibaya mno na likisu Ila iliniumq balaa Mana hela ya kusikia me ndo nilikuwa nmempa
🤣😅😅Jamani kuna ambao tuna dreads narural kabisa, Nyembamba na safi muda wote.
Halafu kuna hizi mnazoingelea ambazo zinabandikwa saloon ' fake dreadlocks' ambazo zimejaa mtaani wanazibana kichwani kama kata utadhani mtu anaenda kuchota maji. Hizo ndo nyingi hazipendezi.
Lakini pia kwa ambao tuna dreads kabisa tunahitaji usafi sana na maintenance. Maana dread ukiziacha kidogo tu zikachafuka unaonekana kama chizi alotoroka milembe🙈😃.
Dreads ni nzuri ila unahitaji kuwa msafi na kuzihudumia na hapo pote ni pesa..uzioshe kila wiki, uzisokote, zikioteana katikati ufanye treaming walau kila mwezi nk. unahitaji pia kuwa na kofia nzuri ya kulalia material zinazofaa . Au ukilala bila kofia uwe tayari kuwa unazigharamia tena kutolewa nyuzi nyuzi zinazoingia kwemye nywele..otherwise ndo ile unaonekana smart kwa mbali halafu mtu akizisogelea dreads anaona zina kama mautango anadhani ni uchafu kumbe ni nyuzi za nguo. Hapo ndo shida inakuja na wengi wanafanya wenye dreads waonekane wachafu..natural dread usiwe bahili ..
Hizo fake dreads aisee zimevamia sana mtaani...na hazipendezi kama natural dreads. Na natural dreads ni safari ya uvumilivu wa hali ya juu sana..natural dreads sio za kila mtu aisee
Aseeee 🤣🤣🤣🤣
Huyu ni mimi, sa mbona umenipost humu?🙄
Namaanisha sampleNazipenda na sina mpango wa kuzitoa kuliko kusuka nywele zingine ni bora nibakie nahizi naongezea na wigs Basi.
Changamoto yangu ni staili jamani kichwa changu ni kidogo na nywele sio ujazo kiviili [emoji275] naombeni samble ya staili zakuweka.
Ila kiukweli hii nywele inabana bajeti sanaaa mimi nikiwa na mafuta basi kwa mwezi natumia 10k tu.